Rasimu ya Mitaala Nchini: Umri wa kuanza darasa la kwanza ni miaka 6, elimu ya msingi mwisho darasa la 6
Taarifa inaeleweka ILA hapo kwenye LUGHA ya kufundishia huku MSINGI sio sawa hata kidogo..kuanzia Awali hadi Chuo Kikuu ,lugha ya kufundishia iwe KIINGEREZA..Sisi tunaihitaji Dunia zaidi kuliko yenyewe inavyotuhitaji..Kiingereza ndio KISWAHILI cha dunia

Pili mnawasababishia watoto ugumu wafikapo SEKONDARI

Hebu Mheshimiwa Waziri acheni kutuchezea SHERE Watanzania ..Mbona ninyi watoto wenu wote(Mawaziri, Wabunge et al) wanasoma English Medium..KWANINI?

Hofu ya NINI ikiwa sasa tuna Waalimu wengi wanaojua KIINGEREZA na MIUNDOMBINU IPO
N.B
NINYI ENDELEENI KUCHEZA NA MAISHA YA WATANZANIA, HAKIKA LAANA YA MUNGU ITAWASHUKIA MAANA MNAFANYA KWA MAKUSUDI ILI HALI UKWELI MNAUFAHAMU
 
Elimu ya msingi hadi sekondari kuwepo soma la Madini, uvuvi , kama walivyoweka kilimo.
2. Rasimu ionyeshe combinations kwamasomo ya kidato cha tano na sita ili vyuo vikuu vianze kufuta kozi za hovyo walizonazo.
3. Somo la sayansi kwa elimu msingi ni somo jipya au lipo kwa sasa linafundishwa?
4. Somo la kiarabu na kifaransa yafutwe kwa elimu msingi.
NAKAZIA hapo kwenye number 4...hizi ni lugha zisizo na faida Bora hat wafundishe kichina maana fursa nyingi za biashara ziko na wachina
 
Taarifa inaeleweka ILA hapo kwenye LUGHA ya kufundishia huku MSINGI sio sawa hata kidogo..kuanzia Awali hadi Chuo Kikuu ,lugha ya kufundishia iwe KIINGEREZA..Sisi tunaihitaji Dunia zaidi kuliko yenyewe inavyotuhitaji..Kiingereza ndio KISWAHILI cha dunia

Pili mnawasababishia watoto ugumu wafikapo SEKONDARI

Hebu Mheshimiwa Waziri acheni kutuchezea SHERE Watanzania ..Mbona ninyi watoto wenu wote(Mawaziri, Wabunge et al) wanasoma English Medium..KWANINI?

Hofu ya NINI ikiwa sasa tuna Waalimu wengi wanaojua KIINGEREZA na MIUNDOMBINU IPO
N.B
NINYI ENDELEENI KUCHEZA NA MAISHA YA WATANZANIA, HAKIKA LAANA YA MUNGU ITAWASHUKIA MAANA MNAFANYA KWA MAKUSUDI ILI HALI UKWELI MNAUFAHAMU

Kweli kabisa,kwenye hayo maoni ya mwisho hili waliweke sawa bila kuumauma maneno
 
Members yeyote mwenye Rasimu ya Mtaala wa Elimu na Rasimu ya Katiba Mpya (ya Warioba).
 
MAPENDEKEZO YA RASIMU YA RIPOTI YA KAMATI YA KITAIFA YA MABORESHO YA MITAALA AMBAYO YANAENDA KUBADILISHA MFUMO WETU WA ELIMU .

Na Baltazari Luhanga.

1. Mtihani wa darasa la saba utafutwa. Mwanafunzi akianza darasa la kwanza lazima amalize kidato cha nne.

2. Kutakuwa mtihani wa upimaji wa kitaifa wa darasa la sita (Standard Six National Assessment).

3. Mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza kidato Cha nne ili aweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza.

4. Lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwa kiswahili, Kiingereza kitakuwa Kama somo kwa shule za Kiswahili medium na lugha ya kufundishia English, kiswahili kitakuwa Kama somo kwa shule za English medium.

5. Elimu ya msingi itakuwa miaka 6. Mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka 6, tofauti na ya sasa miaka 7.

7. Elimu ya awali mwanafunzi ataanza akiwa na miaka 5.

8. Masomo ya elimu ya msingi yatakuwa KKK, Jiografia, kiswahili, Sanaa na michezo, hisabati, sayansi, historia ya Tanzania na maadili, dini na kiingereza na stadi za kazi itachopekwa.

9. Kiingereza kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiswahili na kiswahili kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwanza kwa shule za kiingereza.

10. Shule zenye uwezo zitafundisha walau somo moja la lugha za kigeni kama kichina au kifaransa.

11. Sekondari kutakuwa na mikondo 2, mkondo wa jumla na amali (ufundi). Mwanafunzi atachagua kutokana na
uwezo, matakwa na malengo yake ya badae.

12. Mkondo wa amali (ufundi) utakuwa na fani za:
-kilimo na ufugaji
-umakenika
-biashara na ujasiriamali
-sanaa bunifu
-elimu ya michezo
-ufugaji wa nyuki
-uchimbaji wa madini
-urembo

13. Mwanafunzi wa mkondo wa amali atatakiwa kuchukua masomo manne (4) ya jumla na moja la fani.

14. Masomo ya jumla la wanafunzi wa amali ni:
-hisabati
-elimu ya biashara
-kiingereza
-historia ya Tanzania na maadili

15. Wahitimu wa amali watapata vyeti viwili yaani:
-cheti cha ujumla cha elimu ya sekondari (NECTA)
-cheti cha amali (NACTVET)

16. Kila shule itakuwa na wakala wa VETA ili kusimamia maswala ya ufundi.

17. Kila shule haitakuwa na mikondo zaidi ya miwili ya ufundi, hii ni kwaajili ya ufanisi na fani ziwe zinaendana na fursa za eneo husika.

18. Kutaanzishwa somo jipya la mawasiliano ya kitaaluma (academic communication) katika A-level na ualimu.

19. Coding itafundishwa shule ya msingi.

20. Information and Computer Studies (ICS) itabadilishwa na kuitwa Computer Science. Somo limesukwa upya.

21. Civics itaunganishwa na historia ya Tanzania na maadili kwa O-level.

22. O-level masomo ya lazima yatakuwa 6 badala 7 ya Sasa.

23. Katika O-level masomo ya Biology na Geography yatakuwa masomo ya kuchagua pia kwasababu maudhui yake yamekuwa kwenye masomo ya jiografia na sayansi ya shule ya msingi kwa mfano afya ya jamii, afya ya uzazi, magonjwa ambukizi nk.

24. Civics, maarifa ya jamii, uraia na maadili yamefutwa. Maudhui yake yameingia katika somo la historia ya Tanzania na maadili.

25. General Studies (GS) katika A-level itafutwa na maudhui yake yatawekwa katika somo la historia ya Tanzania na maadili na mawasiliano ya kitaaluma.

26. Kufuta baadhi ya masomo kumefanyika ili kuondoa tatizo la kujirudia rudia kwa maudhui.

27. Michepuo katika elimu ya O-level imeongezeka kutoka minne (4) hadi tisa (9). Michepuko iliyoongezeka ni:
-sanaa
-lugha
-muziki
-michezo
-TEHAMA

28. Masomo ya O-level yatakuwa:
-biology
-physics
-chemistry
-history
-geography
-historia ya Tanzania na maadili
-hisabati
-kiswahili
-english
-elimu ya biashara
-utunzaji wa taarifa za fedha
-computer science
-bible knowledge
-elimu ya dini ya kiislamu etc

29. Astashahada ya ualimu itafutwa kisha itaanzishwa Stashahada (diploma) ya elimu ya awali, ualimu wa msingi na ualimu wa elimu maalumu. Watakaosoma Stashahada watakuwa waliomaliza kidato cha sita na itasomwa kwa miaka miwili.

30. Walimu wa sekondari wote watakuwa na Shahada (degree). Kwasababu nchi nyingi ndio wanaenda muelekeo huu.

31. Vyuo vilivyokuwa vinatoa Stashahada (diploma) ya ualimu wa sekondari vitatumika kutoa continuous professional development.

32. Walimu watakaofundisha mkondo wa amali (ufundi) watakuwa Wahitimu wa kozi mbalimbali za amali na watapewa astashahada
(cheti) ya ualimu huo kwa miezi 6.

33. Vyuo vya elimu ya juu vitaanzisha kozi za ualimu wa uandisi, urembo, uvuvi, sanaa bunifu nk. Hii itasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa walimu katika maeneo hayo ya ufundi.

34. Kutakuwa na internship kwa walimu kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kumaliza ualimu ili wawe
na umahiri zaidi. Kisha walimu watapata leseni.

35. Mafunzo kwa vitendo ya walimu tarajali yatafanyika katika shule zilizo karibu na vyuo vya ualimu ili zifanyike kwa umakini zaidi.

36. Kutakuwa na motisha kwa walimu na upandaji wa madaraja utakuwa kwa utaratibu mzuri.

37. Bodi ya usajili wa walimu itaanza kufanya kazi.

38. Utekelezaji wa mtaala mpya na sera ya elimu ya mwaka 2023 itaanza kwa awamu kwa darasa moja moja katika kila level. Hii itasaidia kwenda sawa na bajeti kwasababu kuanza kwa madarasa yote na levels zote ni gharama kubwa sana. Utekelezaji utaanza mwaka 2024 kama sera na mtaala zitapitishwa kama ilivyo.
 
Kuanzishwe mtaala maalumu wa vipaji kama michezo na sanaa kuanzia shule ya msingi, wanafunzi wenye vipaji hivyo wachaguliwe kujiunga na shule maalumu za vipaji za sekondari zitakazojengwa kila Mkoa, huko wafundishwe sanaa na michezo kulingana na vipaji vyao, kisha waongezewe masomo kama ujasiliamali katika sanaa na michezo pamoja na IICT, wakimaliza waende kutumikia vipaji vyao wakiwa bado ‘wabichi’ na wakiwa bado kwenye peak.

Wale watakaotamani kuendelea bila kupractice basi waende vyuo vya michezo kama Malya wafundishwe kwa ngazi za Diploma ili kupata waalimu kwenye shule za vipaji na wataalamu wengine kama makocha na wataalamu wa viungo, sanaa n.k.

Watakao taka kuendelea zaidi wajiunge vyuo vikuu kusoma kozi zinazoendana na career zao kama fine and performing arts na sports medicine ili tuwe na wabobezi kwenye maeneo hayo. Tukiweza hapa tutakuwa tumesaidia sana kuwa na wasanii na wanamichezo weledi kabisa na pia wataalamu mbalimbali badala ya kutegemea kuazima toka nje. Lakini pia tutakuwa tumesaidia kukuza vipaji vyao badala ya kuviua kwa kuwafundisha vitu ambavyo havina tija kwenye vipaji vyao.
 
View attachment 2616490
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda

Akizungumza na waandishi wa habari tarehe 9/5/2023, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 toleo la 2023 pamoja na Rasimu ya Mitaala Mipya ya Elimu ya Msingi, Sekondari na Vyo vya Ualimu zimekamilika, na sasa serikali imetoa rasimu hizo hadharani ili kupata maoni ya mwisho, na maoni hayo yawe yameshapokelewa kufikia tarehe 31/5/2023.

Akaongeza kuwa tarehe tarehe 10/5/2023 Wizara itafanya Semina na Wabunge kuwapitisha katika Rasimu hizo na tarehe 12/5/2023 mpaka 14/5/2023 kutakuwa na Kongamano Kubwa la Kitaifa la kujadili Rasimu hizo.

Rasimu hizo zinapatikanakatika Tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, lakini pia katika tovuti ya Idara ya Habari na Maelezo pamoja na tovuti ya Taasisi ya Elimu Tanzania.

Kwa maelezo zaidi unaweza kusoma kimbatisho hapo chini.

View attachment 2616524View attachment 2616525View attachment 2616527
View attachment 2616528
View attachment 2616529
View attachment 2616530View attachment 2616531
Lugha rasmi ziwe Kiswahili na Kiingereza; lugha za ziada daraja la pili ziwe ni French, Spanish; daraja la tatu ndio ziwe lugha zilizobaki na kubalansi waongeze Latin kwa ajili ya wakatoliki, na Hebrew kwa ajili ya walokole na wasabato kama ilivyo Arabic kwa waislamu

Nawasilisha
 
4. Somo la kiarabu na kifaransa yafutwe kwa elimu msingi.
Katila lugha hapo, ili kubalansi waongeze Latin (kilatini) kwa ajili ya wakatoliki, na Hebrew (kiyahudi/kiebrania) kwa ajili ya walokole na wasabato kama ilivyo Arabic kwa waislamu
 
Back
Top Bottom