Mtoto wa Shule
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 15,133
- 11,914
Mbowe amesusa shughuli zote za chama. Wafadhili na wadhamini watoa hela wamesusa kuchangia pesa za kuendesha chama wakisema hawamuamini Lissu na genge lake. Kaitisha vikao na vikao watu wamesusa ndio maana mpaka leo hajaongea chochote kwa wanachama wake. Leo eti wapewe dola.Hiki Chama ama kweli kimenivutia.
Hiki chama kweli kimeshakuwa na sasa kinaonesha ni chama kinastahili kuwaongoza Watanzania.
Walianza kwa kuwaonyesha Watanzania namna gani Uchaguzi huru na haki unapaswa kuwa kupitia uchaguzi wao wa Viongozi. Sasa Watanzania wote tunajua namna uchaguzi huru na haki unapaswa kuendeshwa.
Sasa wanawaonesha Watanzania namna gani siasa za nchi zinapaswa kuendeshwa.
Tangu Lissu amechaguliwa kushika uongozi wa Chama hatuoni tena siasa za kijinga. Tunaona siasa zilizoenda shule, siasa zinazoendana na Wakati.
Nimevutiwa sana na organizesheni na hotuba ya Mwenyekiti Lissu leo. Lissu ametoa hotuba murua ambayo kila mtanzania amemwelewa. Amechambua vizuri wanamaanisha nini wanaposema bila reforms hakuna uchaguzi na kusema kweli ameelezea vizuri na kueleweka vizuri sana namna mfumo wetu wa uchaguzi na katiba unavyotumiwa vibaya na chama cha mapinduzi.
Nimwevutiwa sana pia na namna walivyoanzisha mjadala kwa kuwaita wataalam kuchambua hotuba ya Mwenyekiti wao. Mjadala umehusisha wabobezi kweli ambao wanachambua vizuri kweli na kueleweka vizuri.
kusema. Kweli hivi ndo namna Chama cha Siasa Makini knapaswa kufanya siasa zake. Hivi ndo namna Chama kinachopaswa kushika dola kinapaswa kujiendesha.
Hongereni sana Chadema. Sasa mmekuwa na kupevuka na kustahili kupewa nchi na dola.
Naiona Tanzania njema na nzuri sana chini ya Chadema.
Kwa namna hii hotuba ya Mwenyekiti ilivyokuwa well organised leo alafu ukilinganisha na CCM wanavyolundika wasanii wasio la akili na machawa kwenye mikutano yao ndipo una amini tunaongozwa na wajinga Tanzania(CCM)
Mungu akazidi kuwabariki
Lord Denning
Dubai
Bado tunaukumbuka wosia wa Baba wa Taifa aliposema nanukuu, "I can't let my country go to the dogs"! Mwisho wa kunukuu.