Rasmi naenda kuacha ajira, Wasomi tumegeuka kituko kwa uoga wa kutegemea matone ya mshahara huku wageni na std 7 wakitajirika kwa rasilimali zilizojaa

Rasmi naenda kuacha ajira, Wasomi tumegeuka kituko kwa uoga wa kutegemea matone ya mshahara huku wageni na std 7 wakitajirika kwa rasilimali zilizojaa

Bora na hongera sana kwa kuukimbia utumwa
Ila wengi wanasoma na kutafuta ajira ili wakale rushwa na sio kulitumikia Taifa
Asilimia kuɓwa wanawaza wizi tu katika taasisi za umma
. Nimesikiliza documentary ya BBC4 radio
Wakurugenzi South Africa wanauwawa sana pindi wanapoingia kazini
Wanaingia kwa kujuana ili wale hela za tenda na miradi ya serikali
Wanasiasa pia wameuwawa wengi sana huko

Afadhali ukaendeleze biashara zako mwenyewe
Kuhusu wakuja hao wanadunduliza na kufika mbali wengi nawajua hawachukui mkopo bali malengo ya miaka mingi ya kuficha hela na kuja kufanya kitu cha maana

Ukiona kaibuka na kiwanda basi kakusanya zaidi ya miaka 10
 
Kibongo bongo, kuna idadi ndogo sana ya wafanyakazi wanaofurahia ajira zao. Wengi wanafanya tu kwa sababu hawana option nyingine.

Na kwenye kujiajiri, kama alivyosema mtoa mada! Pasipo kufanya maandalizi ya muda mrefu, unaweza ukajikuta umeumbuka mtaani.
 
Kimekukuta nini mkuu tupe hints
Mshahara ni 765k, wanakata mpaka inabaki 540k. Hiyo hela ukitoa gharama za maisha unabaki na laki mbili au tatu. Sasa kwa hiyo saving ya laki mbili tatu utafanya maendeleo gani?
Maafisa utumishi wanadhani labda tulikua hatuna kazi huko mitaani so mikwara kibao,ujinga ujinga tu. Ukimcheck mtu mwenyewe umemzidi kipato cha jumla na mengineyo,ila kila siku mikwara tu. Ukiuliza huyu vipi utaambiwa huyo anataka ajira mpya ujue nguvu ya cheo chake tu si vingine,ni UPUUZI!!

Njaa zimetanda huku Halmashauri,nyuso za wafanyakazi wakongwe zimekunjamana,hawana furaha kabisa ya maisha. Ni kama watu ambao wanasukuma tu siku zisogee wazeeke wapate kiinua mgongo au wafe tu.

Watumishi wamepauka,sio kwa kupenda ila ni kipato kiduchu ambacho hakilingani na mahitaji. Wengi wao ni futureless,waoga wa maisha,wao kazi ndio mkombozi wao,kazi ambayo haiwapi furaha wala uhuru wa kipato.

Kila nikiwatizama naona kama na mimi nitakuja kufanana na wao,nikose tumaini la maisha,niishie kuandaa madokezo,nikopwe na halmashauri kwa ziara za hapa na pale. Niishie kuishi maisha ya madeni,salary advance,songesha au Mgodi..?? Aaah nakata tamaa,hii kazi naiacha.
 
Nimesoma uzi pamoja na comments za wachangiaji wengi

My take

1.Ukiwa umeajiriwa na ukafanikiwa kupata mtaji na ukaweza kuanzisha biashara ambayo ni sustainable , ni sahihi kabisa kuacha kazi na kwenda kupambania biashara zako ili ziweze kukua zaidi

2. Uthubutu ni muhimu - Lakini uthubutu wa kuacha kazi na kwenda kuanzisha biashara ambayo huielewi kwa mara ya kwanza ni risk kubwa sana maana asimilia za kufeli huwa ni kubwa kuliko za kufanikiwa

3.Kuajiriwa sio jambo baya sana kama ambavyo linakua portrayed au kua associated na umaskini , wako watu wameajiriwa na wanafanya vizuri na wana maendeleo makubwa sana lakini pia ieleweke katika mnyororo wa maisha kila mtu ana role to play - hata waajiriwa wanahitajika ! Kila mtu akijiajiri nani atafanya kazi za kuajiriwa ?

4.Hakuna watu wanaopoteza pesa nyingi sana katika kujaribu biashara kama waajiriwa - wengi wao wanajaribu kilimo, kufungua vioffice vya hapa na pale lakini kwasaabu ya muda finyu wa kuangalia hizo biashara nyingi huwa zinakufa au wasimamizi ambao wanakua wameaminiwa wanaziua kwasababu hawana vision sawa na wewe uliyezianzisha.

5.Shida ni moja , hata wewe ambaye umeweza kuwa muajiriwa na ukaanzisha biashara na zikafanikiwa hata tukikuuliza au kukuomba muongoza wa biashara unayoifanya au kutuambia misingi unayoitumia najua utatuambia tu "za kuambiwa changanya na zako" au "kapambane kama nilivyopambana"

6.There is more than the eye can see ! Some are lucky some are just not - biashara unaweza ukaianzisha kwako ikakataa akaja mtu mwingine, eneo lile lile ulikokuwepo biashara yake ikakubali wakati yako ilibuma ikikuacha na mzigo mkubwa wa hasara au madeni.

7. Mwisho kabisa pamoja na maangalizo hapo juu ni kweli nchi hii ina fursa nyingi sana, na pesa nyingi ipo kwenye kazi ngumu ambazo waajiriwa au tunaojiazania ni wasomi tunazikwepa au kuziogopa au kua na wasiwasi na jamii kwamba tutaonekaje ! Lakini pia kuna dhuluma kubwa sana na utapeli mwingi maana wabongo hawaaaminiki na wengi wanapenda wenzetu wanaothubutu washindwe na kufeli kabisa
 
And the time is now.

Sisi watanzania nimekuja kushangaa sana inakuwaje tumejaaliwa rasilimali tunawaachia wahindi, waarabu, wapalestina, wairan, wanapiga mihela halafu sisi tunauza mpaka mashamba ili upate ajira, kuanza maisha kwenye ajira sio tatizo ila shida ni kulala usingizi wa pono kuridhika mazima na matone ya mshahara mpaka uzeeni.

Itoshe kusema ajira imeweza kunipa pesa za kujitegemea, gari, mikopo ya fasta, n.k ila sasa ni muda wangu ku venture other oppurtunities.

Nimeamua niingie kwenye biashara za rasili mali zetu tulizojaalowa kwa upendeleo mkubwa sana hapa Tanzania, mwaka jana pekee niliingiza zaidi ya mara 4 ya mshahara wangu + posho za mwaka mzima net profit faida baada ya kuondoa gharama zote and i am barely 35 and very energetic, why nimalizie prime yangu kwenye kusubiri mshahara na posho ? Hell No !! hapana kwakweli !!, i am set to go, My plan ni kuacha ajira hata sasa ila kwa sababu kadhaa ambazo ni external factors ntaacha mwakani .

Nashukuru kiingereza cha kumingle kwenye soko kinapanda, nimepata exposure kwenda nje ya nchi kitu kilichofanya nijue kwamba watanzania tunachezea fursa za rasili mali zetu, nina idle connections sababu ya uoga wangu but ni muda wa kuzifanya ziwe active.

MUHIMU: Kazi naacha kwenda kuendeleza na kuzipa muda na umakini biashara ambazo tayari nina uzoefu nazo, siachi kazi kwenda kuanza biashara from scratch.

Sawa kila la kheri.
 
Back
Top Bottom