Rasmi nimeligundua hili, Mungu na Shetani hawapo: Dini ni utapeli

Kama Mungu hayupo Kwa nini usijinyonge? Kuna haja gani ya kuishi miaka 80 wakati mwisho ni kufa tu kama ulvyo Sema? Kwa nini usife sasa hivi?
 
Kama Mungu hayupo Kwa nini usijinyonge? Kuna haja gani ya kuishi miaka 80 wakati mwisho ni kufa tu kama ulvyo Sema? Kwa nini usife sasa hivi?
Nivyema ungejinyonga wewe Ili ukaonane na. Huyo mungu unaemuimba Kila siku Cha ajabu unaishi hutaki kumuona🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hapana,ila inasikitisha sana,hivi hata alama hazioni!!?,ajiulizi yeye katokeaje na viumbe wengine wametokea wapi??nani kamuumba yeye,aridhi,mbingu nk.
Kwa nini unalazimisha awepo aliyeumba viumbe, ardhi na binadamu?

Mbona hujiulizi na huyo aliyeumba ardhi, viumbe na binadamu, Na yeye aliumbwa na nani?

Au unataka kutetea imani zako uchwara ulizo pumbazwa na kuaminishwa?
 
Fanya vyote lakini usimdhihaki Mungu, ni swala la muda atakuthibitishia uwepo wake
Ndivyo ulivyo pumbazwa na kuaminishwa hofu zako uchwara na dini yako.

Huyo Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.

Huyo Mungu kama yupo ajitokeze hadharani mwenyewe ajidhihirishe kama ana huo uwezo.
 
NIMEIKUTA HII MAHALA

Ninajua kila mtu anajua kinachoendelea kule Los Angeles ila sijui ni wangapi wanajua chanzo cha ule moto unaouangamiza mji wa uzuri wa Dunia,

Ilikuwa hivi:

Kulikuwa na event ya super stars🌟 ktk mji wa Los Angeles,
Wakiwa katikati ya sherehe wakaanzisha mchezo wa kupiga kura kwa watu wenye thamani ktk jamii yao,

Majina yaliyoorodheshwa ni 1.Cast&Crew(wacheza filamu wa Hollywood na washiriki)
2.thamani ya mama ,
3.Lopez
4.MUNGU.

Ktk matokeo ya uchaguzi wao matokeo yalikuwa hivi:
Cast&Crew= kura 11
Thamani ya mama=Kura 3
Lopez =Kura 1
MUNGU=walimpa kura 0,

Msimamizi wa uchaguzi akasema matokeo hayo hayashangazi kwani mji wao ni Godless town,
Walipotoka nje wakatengeneza bango kubwa lenye maandishi "God get out in this city"
kesho yake ndo mji ukaanza kulipuka,
Ukumbuke msitu wa Amazon ulioko Brazil ambao ndio msitu mkubwa zaidi duniani ulipoungua miaka 4 iliyopita ni Marekani ndiyo iliyosaidia kuuzima lkn huu wa kwao umewashinda, Marekani ndiye baba wa technology ulimwenguni,ukizungumza Helocopter,ndege,kemikali na kila sayansi unaizungumzia Marekani,
Sasa hivi wanafyeka mahecta ya misitu kwa kuyang'oa na kuchimba kimo kirefu kwenda chini ili moto ukifika usivuke mbele lkn kinachotokea ni kwamba kila wakichimba moto ukifika kwenye mtaro waliouwekea mpaka inatokea cheche moja inapaa angani inavuka mpaka inashukia ghorofa linaambukiza miti na ghorofa nyingine mji unaangamia,
mamia ya ndege na helcopter za zimamoto ziko angani Calfornia zikimwaga kemikali za kuzima moto lkn moto umegoma kuzimika, hakuna matumaini, majumba ya wasanii mabilionea wa Holly Wood yanaangamia,
Holly Wood ndiko kuna makazi ya thamani kuliko miji yote ulimwenguni, kidunia Hollywood inatambuliwa kama makao makuu ya uzur wa dunia lkn saa hii panaelekea kuwa jangwa gumu, wafuatiliaji wa sinema za Hollywood mlioko humu jiji lenu/mazingira yenu pendwa ya Hollywood linaangamia,

Ule moto hautozimwa na technology,
Utazimwa na Toba ya makuhani,

Nimeyasema haya ili kutoa tahadhari tujiweke mbali na vikundi vyenye mizaha juu ya MUNGU MKUU, ukiona kiashiria chochote cha mzaha kwa BWANA kemea kwa nguvu, wasipokuelewa kata connection na hicho kikundi hata kama kina maslahi makubwa kiasi gani,

BWANA MUNGU hadhihakiwi!
 
God is good
Huyo God ambaye unasema is good, ndio anashindwa kuwasaidia maelfu ya watoto wadogo na wanawake wanaokufa kwa njaa, vita, magonjwa na majanga mbalimbali ya asili duniani.

Halafu unakuja hapa kumsifia na kumpa sifa uchwara huyo God mdhaifu ambaye hawezi hata kuwasaidia watu kama hawa👇👇

Huyo Mungu kama yupo ni muovu sana na anastahili kufurushwa huko alipo. Hana wema wowote ule.
 
Gazeti refu limejaza utumbo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…