Rasmi nimemaliza chuo, bila mshahara wa milioni moja sifanyi kazi. Tumshauri au tumuache!

Eli Cohen min -me ushauri wenu unahitajika
First of all, huyu bado ana hangover ya graduation.

Nakumbuka hata mimi kipindi namaliza chuo kuna stanadard fulani unakuta unajiwekea ila mostly zinaenda na hewa kwa maana hazina uhalisia katika soko hili la ajira ambalo hata ukipata kazi mtu anataka ukae kwake kama intern miaka hadi mitatu huku anakulipa mshahara wa 300k, tena kupata internshipi hii bado ni kama neema na bahati.

Kama unakuta una misiingi kama ya muandika x post hio, unapaswa kuwa versatile, lakini unasema hivyo alafu unaenda kukaa kwa shemeji unasubiria ajira ya mshahara wa ndoto zako utasugua makochi sana

Versatile namaanisha, inapswa uingie ufanye mambo mengine ya kukusogezea maisha huku ukiwa unasubiri mshahara wa ndoto.

Tofauti na hapo unafanya vichekesho vya tom and jerry
 
Umeeleza vizuri vijana wakiwa chuo wanadhani maisha ni simple kihivyo, kumbe uhalisia ni kuwa mambo ni magumu sana, tena sana.
 
Yuko sahihi.Nampongeza Kwa shauku yake.mshahara chini ya milioni bila marupurupu ni kupoteza nguvu Yako Bure na kujichelewesha kuondokana na umasikini.Ni Bora ujiajili mwenyewe kama ufugaji kilimo,uvuvi,n.k lakini siyo kulipwa vijisenti vya kununua pipi ambavyo ni chini ya milioni au milioni kamili bila marupurupu
 
SAWA, lakini je uhalisia uko hivyo mtaani. Kazi zinataka uwe a experience ya miaka mitatu kwenda juu, ndio umegraduate experience huna, sana sana utajitolea kwa viposho vya 150k
 
After 6 month, atafutwe mtashangaa namna watu wanavyo badilika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…