Rasmi: Yanga SC yaishinda Mabavu ya Kifedha Simba SC kwenye usajili wa Masoud Djuma

Rasmi: Yanga SC yaishinda Mabavu ya Kifedha Simba SC kwenye usajili wa Masoud Djuma

Wadanganye ( Wapuuzi ) wenzako Yanga SC kuhusu hili na najua wengi wao walivyo ' Oya Oya ' hapa watakuamini kweli kweli tu.

Simba SC ni Klabu inayoendeshwa Kitaalam ( Kisomi ) na pia ina Idara yake nzuri sana ya ' Kijasusi ' ambayo huwa inafanya Tathmini ya Kina kwa Mchezaji imtakaye.

Ni kweli Mchezaji huyu alikuwa katika ' Rada ' za Simba SC na Pesa kubwa tu ya Kumsajili ilishatengwa ila baada ya ' Ujasusi ' kwa Kitaalamu ( hasa wa Kidaktari ) Simba SC iliyoufanya kwa Kushirikiana na ' Waandamizi ' wa Klabu yake huyu Mchezaji imegundulika kuwa ni hayuko 100% vyema Kiafya ( Proin Injury ) na kwamba atakuja Kuigharimu Timu ( Simba SC ) kwa Kumtibu zaidi na Kuingia Hasara vile vile.

Najua kuwa Kiungo wenu Tonombe Mukoko ndiyo amefanikisha hasa kwa Kumshawishi huyu Mchezaji atue Yanga SC ila Yanga SC mnadhani kuwa mmelamba Dume kwa Kuwazidi Simba SC huku mkisahau kuwa huyo Mchezaji hayuko ' that Fit ' kwa Kucheza Mpira mara kwa mara.

Kuhusu Pesa uliyoitaja hapa ni Uwongo mtupu ( tena wa 100% ) kwani Ukweli ni kwamba Yanga SC mmetanguliza Tsh Milioni 350 tu na zingine Tsh Milioni 150 zake mtakuja Kummalizia huku Tanzania baada ya Kuuza uza Magodoro yenu yanayoumiza Migongo.

Namalizia kwa Kuwaambia Yanga SC kuwa Simba SC haisajili bali ' inajazilia ' na kuna ' Bunduki ' Tatu tu za Kigeni zinakuja nafasi ya Beki wa Kati ili acheze Pacha na Onyango huku Wawa akiwa sasa anasaidiana na Kapombe Shavu la Kulia na ' Duchu ' akiendelea Kuchota Uzoefu Kwao.

Pia kuna ' attacking Midfielder ' mmoja kutoka Misri au Congo DR anakuja na tunamalizia na Mshambuliaji ' Talisman ' kabisa kutoka Morocco au Tunisia au Uganda au Afrika Kusini.

Anachokifanya sasa Injinia Hersi Said na GSM yake Watoto wa Mjini akina GENTAMYCINE tunakiita ' anawapiga Ganzi ' kwani anajua kuwa Mmeshaukosa Ubingwa ambao aliwaahidi huku akiapia kuwa msipouchukua Mumuulize Yeye hivyo sasa ' anawazuga ' kwa Kusajili Wachezaji wanaosifika ili msahau ' Kumuhoji ' na ' Kumshambulia ' katika Mkutano wenu Mkuu ujao na aendelee kuwepo sana tu Yanga SC huku Yeye na GSM yake ' Wakijitajirisha ' na Timu yenu ikizidi tu ' Kutaabika ' Kimapato ( Kiuchumi )

Ndiyo maana Yanga SC mnaambiwa hamna Akili kwani ni Watu tu wa Kudanganywa kama Watoto Wadogo halafu ni wepesi mno Kuridhika na Kusahau. Najivunia sana kuwa Shabiki wa Simba SC kwani ni Timu ya Watu Werevu, Wasomi, Makini na Wastaarabu tupu.
sasa popoma nimefurahi kusikia tunaongeza wageni watatu nani anaondoka? maana hata baada ya kuondoka kahata bado wageni wako kumi
 
Simba ni wazuri kwa scouting ya wachezaji hivi karibuni walitunia mamilioni ya shilingi kwa Chikwende, Peter Maduhlwa, Mugalu(matizo ya goti) Junior Lukosa. Hii ni tafsiri halisi ya timu yenye Scouting Bora kwa apa kwetu kwa mwaka mmoja.
 
sasa popoma nimefurahi kusikia tunaongeza wageni watatu nani anaondoka? maana hata baada ya kuondoka kahata bado wageni wako kumi

Hakuna mpango wa kuwaondoa wachezaji 3 a kigeni kutoka simba (Asikudanganye). ili waondoe achezaji wa3 ni lazima wa-offload some!

Na kama ni ku-offload some basi ni Kagere & Wawa!

sioni uwezekano wa mchezaji yeyote aliyebaki tofauti na hao kuondoshwa.

In fact msimu huu hawatosajili zaidi ya wachezaji 3 overall (local & international players)
 
Simba ni wazuri kwa scouting ya wachezaji hivi karibuni walitunia mamilioni ya shilingi kwa Chikwende, Peter Maduhlwa, Mugalu(matizo ya goti) Junior Lukosa. Hii ni tafsiri halisi ya timu yenye Scouting Bora kwa apa kwetu kwa mwaka mmoja.

Kuna mdau hapo juu anaitwa GENTAMYCINE

Amesema kuwa klabu yake ina scout bora kuliko AL ahly, Tp Mazembe na mamelodi.
 
Masoud Djuma (umri 28) akamilisha usajili wake ndani ya Yanga SC kwa dau la USD500,000 (Bilioni 1 & Milioni 150) Yanga imefanikiwa kuwashinda wapinzani wao Simba SC Tanzania baada ya offer yao ya USD 399,000 (Milioni 850) kutupiwa kapuni.

Simba SC Tanzania ilimuhitaji Djuma kama mchezaji pacha wa Shomari Kapombe (Umri 29) ambaye umri wake unaelekea ukingoni.

Sasa Yanga imekamilisha usajili wa klanza kabla hata dirisha la usajili halijafunguliwa. Djuma atasafiri kuelekea Dar pale msimu wa LigiKUuu nchini ongo yaani Linafoot itakapofikia tamati.

Je mabavu ya kifedha yaliyo onyeshwa na Yanga SC kwenye mbio za kumsajili Masoud Djuma dhidi ya mahasimu wao ni kiashirio tosha kuwa Yusuph Manji ameanza kutunisha misuli yake?

View attachment 1813956
Wacha aje afe njaa
 
Tuache ushabiki usio na maana. Kama kweli Yanga wamemsajili Djuma wapewe hongera zao kwani siioni timu isiyopenda kuwa na mchezaji wa aina yake. Ni beki wa pembeni lakini dakika zote tisini yupo kwenye "box" la timu pinzani. Krosi nzuri, chenga zenye faida na kasi sasa ukiwa naye unahitaji nini cha zaidi. Tunaoufahamu mpira tulijuwa tu Simba inapeleka amsha amsha kama kawaida ili tu Yanga ilipe pesa nyingi kwani kwa Simba ya sasa mahitaji ya beki wa pembeni sio kipaumbele chao kwani yupo Kapombe anawatosha. Kwa Simba kumsajili Djuma ingekuwa ni uharibifu wa nafasi za wachezaji kumi wa kigeni na isitoshe hakuna timu duniani inayoweza kusajili wachezaji wote bora peke yake kwani hata Real Madrid ilishindwa hilo zoezi enzi za "Galaticos".
 
Mleteni na huyo kichapo kipo pale pale hiyo tarehe 3. Kwanza pale Simba angecheza nafasi ya nani?
 
Shomari Kapombe - anuary 28, 1992 (age 29 years)

Djuma Shabani - March 16, 1993 (age 28 years)
kapombe yupogo Simba shida ni kwa uzee wake hadi aje kuzoea style yenu ya butuabutua mtashangaa
 
so kamati ya wabebaji kutoka yanga isha jiandaa kumpokea au round hii wanakuja kwa staili nyingine ya kumbuluza baada ya kuona wale walio wabeba jujuu mwanzo hawajaleta impact?
 
Hawa waliopo wanashindia mihogo halafu mtoe bilioni moja na ushee kusajili mchezaji mmoja? hii ni akili, matope au mataputapu.
 
Back
Top Bottom