Wadanganye ( Wapuuzi ) wenzako Yanga SC kuhusu hili na najua wengi wao walivyo ' Oya Oya ' hapa watakuamini kweli kweli tu.
Simba SC ni Klabu inayoendeshwa Kitaalam ( Kisomi ) na pia ina Idara yake nzuri sana ya ' Kijasusi ' ambayo huwa inafanya Tathmini ya Kina kwa Mchezaji imtakaye.
Ni kweli Mchezaji huyu alikuwa katika ' Rada ' za Simba SC na Pesa kubwa tu ya Kumsajili ilishatengwa ila baada ya ' Ujasusi ' kwa Kitaalamu ( hasa wa Kidaktari ) Simba SC iliyoufanya kwa Kushirikiana na ' Waandamizi ' wa Klabu yake huyu Mchezaji imegundulika kuwa ni hayuko 100% vyema Kiafya ( Proin Injury ) na kwamba atakuja Kuigharimu Timu ( Simba SC ) kwa Kumtibu zaidi na Kuingia Hasara vile vile.
Najua kuwa Kiungo wenu Tonombe Mukoko ndiyo amefanikisha hasa kwa Kumshawishi huyu Mchezaji atue Yanga SC ila Yanga SC mnadhani kuwa mmelamba Dume kwa Kuwazidi Simba SC huku mkisahau kuwa huyo Mchezaji hayuko ' that Fit ' kwa Kucheza Mpira mara kwa mara.
Kuhusu Pesa uliyoitaja hapa ni Uwongo mtupu ( tena wa 100% ) kwani Ukweli ni kwamba Yanga SC mmetanguliza Tsh Milioni 350 tu na zingine Tsh Milioni 150 zake mtakuja Kummalizia huku Tanzania baada ya Kuuza uza Magodoro yenu yanayoumiza Migongo.
Namalizia kwa Kuwaambia Yanga SC kuwa Simba SC haisajili bali ' inajazilia ' na kuna ' Bunduki ' Tatu tu za Kigeni zinakuja nafasi ya Beki wa Kati ili acheze Pacha na Onyango huku Wawa akiwa sasa anasaidiana na Kapombe Shavu la Kulia na ' Duchu ' akiendelea Kuchota Uzoefu Kwao.
Pia kuna ' attacking Midfielder ' mmoja kutoka Misri au Congo DR anakuja na tunamalizia na Mshambuliaji ' Talisman ' kabisa kutoka Morocco au Tunisia au Uganda au Afrika Kusini.
Anachokifanya sasa Injinia Hersi Said na GSM yake Watoto wa Mjini akina GENTAMYCINE tunakiita ' anawapiga Ganzi ' kwani anajua kuwa Mmeshaukosa Ubingwa ambao aliwaahidi huku akiapia kuwa msipouchukua Mumuulize Yeye hivyo sasa ' anawazuga ' kwa Kusajili Wachezaji wanaosifika ili msahau ' Kumuhoji ' na ' Kumshambulia ' katika Mkutano wenu Mkuu ujao na aendelee kuwepo sana tu Yanga SC huku Yeye na GSM yake ' Wakijitajirisha ' na Timu yenu ikizidi tu ' Kutaabika ' Kimapato ( Kiuchumi )
Ndiyo maana Yanga SC mnaambiwa hamna Akili kwani ni Watu tu wa Kudanganywa kama Watoto Wadogo halafu ni wepesi mno Kuridhika na Kusahau. Najivunia sana kuwa Shabiki wa Simba SC kwani ni Timu ya Watu Werevu, Wasomi, Makini na Wastaarabu tupu.