Rasmi: Yanga SC yaishinda Mabavu ya Kifedha Simba SC kwenye usajili wa Masoud Djuma

Rasmi: Yanga SC yaishinda Mabavu ya Kifedha Simba SC kwenye usajili wa Masoud Djuma

Pesa nyingi sana hiyo kwa mchezaji mmoja tu kwa timu zetu hizi, ingeweza kutumika hata kuboresha miundombinu ya klabu...
Hiyo si pesa nyingi kwa sasa. Pengine mchezaji kama yeye hapo baadaye atakua kununuliwa kwa takribani pesa zaidi ya hiyo.

2002 Ronaldo De Lima alikuwa na thamani ya $46.3 million, Mwaka 2019 Nicolaus Pepe (Arsenal) alikuwa na thamani ya €79 million.

Kila zama na zama zake!
 
Huku Jangwani atutaki mambo za kuchoteana Uzoefu, Huku inabidi uje na uzoefu wako hata kama una majeruhi mwili mzima.
Ni kweli kabisa, maana Saido, Sarpong na Fiston Abdou Razak ni wazoefu kweli kweli
 
Kakimbia njaa kama hujui.
Sasa binadamu akiwa na njaa si anakufa?

Binadamu akikaa siku 3 pasi na kula chochote ni lazima afe. Sasa mbona Carlos Guimares Calinho na ukizingatia amekaa pale ka muda wa miezi 6.

Au unapanga kutuambia kuwa binadamu ana uwezo wa kukaa miezi 6 bila kula? 😂
 
Hiyo si pesa nyingi kwa sasa. Pengine mchezaji kama yeye hapo baadaye atakua kununuliwa kwa takribani pesa zaidi ya hiyo.

2002 Ronaldo De Lima alikuwa na thamani ya $46.3 million, Mwaka 2019 Nicolaus Pepe (Arsenal) alikuwa na thamani ya €79 million.

Kila zama na zama zake!

Mchezaji wa miaka 28 huwezi mpigia hizo hesabu, huo si umri wa kusajili ukitarajia kufanya biashara...

Ukiacha hilo, timu za Tanzania hazijawekeza sana kwenye biashara ya wachezaji (kuuza/kununua/kuuza), ukitazama mchezaji wa mwisho Yanga kuuza nje ni Msuva na kabla ya hapo sijui alikuwa nani usishangae akawa Papii Nonda Shaban
 
Ni kweli kabisa, maana Saido, Sarpong na Fiston Abdou Razak ni wazoefu kweli kweli

Hao sasa haana tatizo la uzoefu (Kimombo: Experience).

Hao wote ni Legends kwenye soka!

Nikimaanisha hao unaodhani hawana experience wameshapitia mikiki mikiki huko uarabuni na ulaya?
 
Masoud Djuma (umri 28) akamilisha usajili wake ndani ya Yanga SC kwa dau la USD500,000 (Bilioni 1 & Milioni 150) Yanga imefanikiwa kuwashinda wapinzani wao Simba SC Tanzania baada ya offer yao ya USD 399,000 (Milioni 850) kutupiwa kapuni.

Simba SC Tanzania ilimuhitaji Djuma kama mchezaji pacha wa Shomari Kapombe (Umri 29) ambaye umri wake unaelekea ukingoni.

Sasa Yanga imekamilisha usajili wa klanza kabla hata dirisha la usajili halijafunguliwa. Djuma atasafiri kuelekea Dar pale msimu wa LigiKUuu nchini ongo yaani Linafoot itakapofikia tamati.

Je mabavu ya kifedha yaliyo onyeshwa na Yanga SC kwenye mbio za kumsajili Masoud Djuma dhidi ya mahasimu wao ni kiashirio tosha kuwa Yusuph Manji ameanza kutunisha misuli yake?

View attachment 1813956
Kwani ni nani kakwambia Manji amehusika?
 
Mchezaji wa miaka 28 huwezi mpigia hizo hesabu, huo si umri wa kusajili ukitarajia kufanya biashara...

Hahahaha

Gonzalo Higuani alitoka Napoli kwenda Juventus kwa dau la €90m hapo ilikuwa mwaka 2016. Akiwa na Miaka 28.

Au Yanga SC wamekosea halafu Juventus amepatia?
 
Djuma Shabani ana tatizo sugu la ankle, tuombe awe amelipatia ufumbuzi vinginevyo atakuwa kama Saido Ntibanzokiza
 
Wadanganye ( Wapuuzi ) wenzako Yanga SC kuhusu hili na najua wengi wao walivyo ' Oya Oya ' hapa watakuamini kweli kweli tu.

Simba SC ni Klabu inayoendeshwa Kitaalam ( Kisomi ) na pia ina Idara yake nzuri sana ya ' Kijasusi ' ambayo huwa inafanya Tathmini ya Kina kwa Mchezaji imtakaye.

Ni kweli Mchezaji huyu alikuwa katika ' Rada ' za Simba SC na Pesa kubwa tu ya Kumsajili ilishatengwa ila baada ya ' Ujasusi ' kwa Kitaalamu ( hasa wa Kidaktari ) Simba SC iliyoufanya kwa Kushirikiana na ' Waandamizi ' wa Klabu yake huyu Mchezaji imegundulika kuwa ni hayuko 100% vyema Kiafya ( Proin Injury ) na kwamba atakuja Kuigharimu Timu ( Simba SC ) kwa Kumtibu zaidi na Kuingia Hasara vile vile.

Najua kuwa Kiungo wenu Tonombe Mukoko ndiyo amefanikisha hasa kwa Kumshawishi huyu Mchezaji atue Yanga SC ila Yanga SC mnadhani kuwa mmelamba Dume kwa Kuwazidi Simba SC huku mkisahau kuwa huyo Mchezaji hayuko ' that Fit ' kwa Kucheza Mpira mara kwa mara.

Kuhusu Pesa uliyoitaja hapa ni Uwongo mtupu ( tena wa 100% ) kwani Ukweli ni kwamba Yanga SC mmetanguliza Tsh Milioni 350 tu na zingine Tsh Milioni 150 zake mtakuja Kummalizia huku Tanzania baada ya Kuuza uza Magodoro yenu yanayoumiza Migongo.

Namalizia kwa Kuwaambia Yanga SC kuwa Simba SC haisajili bali ' inajazilia ' na kuna ' Bunduki ' Tatu tu za Kigeni zinakuja nafasi ya Beki wa Kati ili acheze Pacha na Onyango huku Wawa akiwa sasa anasaidiana na Kapombe Shavu la Kulia na ' Duchu ' akiendelea Kuchota Uzoefu Kwao.

Pia kuna ' attacking Midfielder ' mmoja kutoka Misri au Congo DR anakuja na tunamalizia na Mshambuliaji ' Talisman ' kabisa kutoka Morocco au Tunisia au Uganda au Afrika Kusini.

Anachokifanya sasa Injinia Hersi Said na GSM yake Watoto wa Mjini akina GENTAMYCINE tunakiita ' anawapiga Ganzi ' kwani anajua kuwa Mmeshaukosa Ubingwa ambao aliwaahidi huku akiapia kuwa msipouchukua Mumuulize Yeye hivyo sasa ' anawazuga ' kwa Kusajili Wachezaji wanaosifika ili msahau ' Kumuhoji ' na ' Kumshambulia ' katika Mkutano wenu Mkuu ujao na aendelee kuwepo sana tu Yanga SC huku Yeye na GSM yake ' Wakijitajirisha ' na Timu yenu ikizidi tu ' Kutaabika ' Kimapato ( Kiuchumi )

Ndiyo maana Yanga SC mnaambiwa hamna Akili kwani ni Watu tu wa Kudanganywa kama Watoto Wadogo halafu ni wepesi mno Kuridhika na Kusahau. Najivunia sana kuwa Shabiki wa Simba SC kwani ni Timu ya Watu Werevu, Wasomi, Makini na Wastaarabu tupu.
Kwa yote uloyaandika hapa hatuna shida nayo na ikiwezekana Eng ataporudi tutaenda airport kumbeba tena!
 
Djuma Shabani ana tatizo sugu la ankle, tuombe awe amelipatia ufumbuzi vinginevyo atakuwa kama Saido Ntibanzokiza

Mbona atumzungumzii Shomari Kapombe au kwa sababu amesajiliwa Simba SC?

By the way, wala hatutegemei awe mchezaji wa kucheza mechi zote za Yanga SC. Ndio maana Kibwana Shomari yupo. Hata akiwa nje kwa wiki mbili nadhani Kibwana Shomari atazisimamia vyema hizo wiki mbili.
 
Kwa yote uloyaandika hapa hatuna shida nayo na ikiwezekana Eng ataporudi tutaenda airport kumbeba tena!

Kokote duniani unapo fanya kazi nzuri ni lazima Upongezwe.

Sidhani kama kuna kabira lolote hapa Bongo lisilo na utamaduni wa kupongeza jambo jema.

Nadhani akifika pale airport abebwe na mashabiki mpaka kwake Mikocheni. Itapendeza zaidi.
 
Djuma Shabani ana tatizo sugu la ankle, tuombe awe amelipatia ufumbuzi vinginevyo atakuwa kama Saido Ntibanzokiza
Haya Mara nyingi ni maneno yasiyo na msingi.

Kila timu ni lazima iwe na aina hiyo ya mchezaji.

Kama kweli angekuwa na hilo tatizo basi hizo timu nyingine kama alizoziainisha Manara zisingekuwa zinamuhitaji.
 
Hahahaha

Gonzalo Higuani alitoka Napoli kwenda Juventus kwa dau la €90m hapo ilikuwa mwaka 2016. Akiwa na Miaka 28.

Au Yanga SC wamekosea halafu Juventus amepatia?

Halafu akauzwaje baada ya hapo? ( Hiyo ndio mantiki ya nilichoandika juu pale)
 
Kipindi cha usajili ni kipindi ambacho mashabiki mazwazwa wa utopolo ndio wanakuwa na furaha kuliko hata mechi ligi kuu zikichezwa

Nadhani umekosea kutokuzingatia fulaha inayopatikana pale timu inapochukua Ubingwa.

Wana Jangwani wamekuwa na furaha mara 27. Ukilinganisha na Mikia ambao wamekuwa na furaha mara 21 tu. Yaani mara 6 zaidi.

Narudia tena. Mara 6 zaidi.
 
Halafu akauzwaje baada ya hapo? ( Hiyo ndio mantiki ya nilichoandika juu pale)
Sio kila mchezaji anaye sajiliwa kwa gharama kubwa analengwa auze kwa gharama kubwa zaidi. Lengo la awali ni kuwa msaada wake kwenye klabu husika kuendana na thamani yake.

Afrika hatujafikia kwenye mipango ya mpira wa kibiashara.

Baada ya msimu kadhaa ya mafanikio pale Juve, Higuaini alikwenda Inter Miami (Timu ya Beckham) on a free transfer.
 
Mbona atumzungumzii Shomari Kapombe au kwa sababu amesajiliwa Simba SC?

By the way, wala hatutegemei awe mchezaji wa kucheza mechi zote za Yanga SC. Ndio maana Kibwana Shomari yupo. Hata akiwa nje kwa wiki mbili nadhani Kibwana Shomari atazisimamia vyema hizo wiki mbili.
Shomari Kapombe amekuwa akipata tatizo akiwa tayari ndani ya Simba. Huyu Djuma anasajiliwa na tatizo kabla hata hajaanza kucheza
 
Back
Top Bottom