Rasmi: Yanga yafuzu klabu bingwa Afrika kwa mwaka 2025/2026

Rasmi: Yanga yafuzu klabu bingwa Afrika kwa mwaka 2025/2026

Wazee wa hatua za awali dhidi ya vitimu vya ethiopia, sudan kusini, eritrea na djibout.. This club ni takataka kwa kweli
 
Kufuatia ushindi wake wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Azam FC hivi punde, sasa ni rasmi kuwa Yanga omefuzu kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika kwa msimu wa 2025/2026.

Ushindi huo wa Yanga unaifanya kufikisha alama 67 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote, isipokuwa Simba.

Kikomo kinachoweza kufikiwa na Azam ni alama 63 huku Singida Black Stars ikikomea kwenye alama 62 endapo timu hizo zitashinda mechi zao zote 4 zilizosalia.

Tayari Yanga ameshajihakikishia nafasi ya 1 au ya 2 na hivyo kupata tiketi ya kushiriki michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Kongole wananchi!
Tunafurahia kweli, ila huko club bingwa hata makundi hatufiki sisi.
 
IMG-20250412-WA0019.jpg
 
Back
Top Bottom