Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Baada ya kusimamishwa kuitumikia Yanga kwa muda kutokana na utovu wa nidhamu, rasmi klabu hiyo imetangaza kuachana na kiungo mshambuliaji Saidi Ntibazonkiza 'Saido' kutokana na mkataba wake kufikia tamati.
Yanga imesema kuwa Saido ambaye alisimamishwa wiki iliyopita baada ya kutoka kambini bila ruhusa, amemaliza mkataba wake leo Mei 30, 2022 baada ya miaka miwili ya utumishi wake klabuni hapo.
Yanga imesema kuwa Saido ambaye alisimamishwa wiki iliyopita baada ya kutoka kambini bila ruhusa, amemaliza mkataba wake leo Mei 30, 2022 baada ya miaka miwili ya utumishi wake klabuni hapo.