Kila la heri huko aendako! Hakika ameifanyia mambo makubwa klabu yetu, ingawa kuna wakati majeruhi yalimuandama.
Kuondoka kwake, ndiyo kuingia kwa jembe lingine. Safisha safisha iendelee kwa wachezaji wote walioshindwa kuonesha maajabu msimu huu. Mashabiki tunataka usajili wa kishindo wa kujazia nafasi zilizoachwa wazi. Yaani ikiwezekana mchezaji anasajiliwa na kuingia moja kwa moja kwenye First 11 ya timu.
Halitakuwa jambo la busara hata kidogo na msimu huu kuishia hatua ya awali kwenye mashindano ya Kimataifa, kama ilivyotokea msimu huu unao elekea ukingoni.