[emoji599]KWA KHERI SAIDO NTIBAZONKIZA ANTIBIOTIC.
Mashabiki na wanachama wote wa Yanga watakukumbuka sana kwa mchango mkubwa ulioutoa kwenye klabu ya Yanga kwa muda wa mwaka mmoja na nusu.
[emoji599]CHANZO CHA YANGA SC KUACHAN NA SAIDO NTIBAZONKIZA
Awali kabisa Yanga walitakaga kiachana na Saido Ntibazonkiza toka msimu uliopita baada ya kuonesha kitendo cha utovu wa nidhamu mbele ya mashabiki wa Yanga na Viongozi wao kwenye mchezo dhdi ya Gwambina Fc kwenye dimba la Benjamin William mkapa stadium.Saido alipishana kauli na Kocha Juma mwambusi na mchezaji akaonesha kitendo cha kutaka kufanyiwa mabadiliko na kushinikiza aondoke uwanjani kabisa licha ya Yanga walikuwa wameshamaliza mabadiliko ya wachezaji watano.
Baada ya mchezo kuisha kocha mpya Nabi alikutana na mchezaji na kumsihi San kuacha kufanya vitendo Kama vile mbele ya Viongozi wake na mashabiki wa Yanga.
[emoji95]Msimu ulipomalizika Yanga kupitia kamati ya usajili walitka kiachana na Saido Ntibazonkiza lakini kocha Nabi ndio aliwahomea viongozi kumwacha.
UTOVU WA NIDHAMU WA MARA KWA MARA
Saido Ntibazonkiza alishaonywa sana na Viongozi wake wa Yanga wakiwemo na Kocha msaidizi Cedric kaze kuacha tabia za kuwashikiniza wachezaji wenzie kambini Kutoka nje ya kambi Avic town na kwenda kwenye kumbi za starehe.Ndani ya msimu huu Saido Ntibazonkiza alishaonywa mara Nne kwenye kamati ya maadili ndani ya Yanga lakini mchezaji alionesha kutojari kwa chochote.
Yanga waliposafiri kwenda mkoani Tanga kucheza mchezo dhidi ya Coastal union Saido Ntibazonkiza alitotoka kambini baada ya mchezo lakini Kocha Nabi alimsisitiza sana kiachana na hiyo tabia bado Saido aligoma kubadirika.
[emoji599]GSM
Wafadhili wa Yanga Gsm walimwitwa mchezaji Saido Ntibazonkiza kufanya nae mazungumzo ya mkataba mpya licha ya vituko vyake vyote Kwani tayari Kocha Nabi alishawaomba mabosi zake wampatie mkataba mpya wa kusalia Yanga msimu ujao.
Mazungumzo baina ya Uongozi wa Yanga na Saido Ntibazonkiza yalikwenda vizuri Yanga walitaka kumpa Saido Ntibazonkiza mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha nyongeza wa mwaka mmoja mbele Kama atacheza kwa kiwango ambacho Kocha Nabi ataridhika nacho msimu ujao.
Baada ya kumalizana kwenye upande wa mslahi Kati ya Yanga na Saido Ntibazonkiza.Sadio Ntibazonkiza aliwaomba Viongozi wake kwenda nchini kwako Burundi Katika shughuli yake(KUFUNGA NDOA). Yanga walimpa baraka zote Saido Ntibazonkiza kwenda kwako Burundi.Yanga walimpa likizo fupi ya wiki mbili kukamilisha shughuli yake lakini Sadio Ntibazonkiza alikaa kwao zaidi ya wiki mbili kitu ambacho uongozi ulimtafuta kujua nini kwa nini amechelewa kurudi kambini lakini Sadio Ntibazonkiza alizima simu zake zote bila kutoa taarifa kwa Uongozi wa Yanga.
Baada ya kutofurahishwa na kitendo hicho Yanga waliamua kuachana nae kutompa mkataba tena.Saido Ntibazonkiza aliporudi kambini Avic town alipewa adhabu ya kukatwa mshahara wake kwa utovu wa nidhamu kitendo ambacho Sadio hakutaka kitokee.
Sadio Ntibazonkiza alipoanza kuomba mkataba mpya ndani ya Yanga Viongozi nao hawakuwa na muda nae.
[emoji599]MWANZA.
Yanga iliposafiri kwenda mkoani Mwanza kucheza na Biashara United mchezaji Saido Ntibazonkiza na ambundo walitoroka kambini Mara baada ya mchezo kuisha kitu ambacho Kocha Nabi kilimuuzi sana na kuwambia mabosi wake Hataki kuwaona kwenye maandalizi yake kuelekea mchezo dhidi ya Simba wa nusu fainali Kombe la Fa.
Nabi alimwambia Mwenyekiti Dkt Mshindo Msolla Ambundo na Sadio watangulie Dar es salaam.Hatimaye jana kamati ya ufundi Yanga ikakutana na kufanya maamuzi ya kuachana nae Sadio Ntibazonkiza.
Katika hatua nyingine Ambundo aliitwa Jana kwenye kamati ya maadili Jana na kuomba msamaha.Ambundo amekubaliwa na atajiunga na timu siku Alhamisi kambini Avic town.
NB;Yanga hakuna mchezaji & kiongozi mkubwa kuliko timu.🟢🟡[emoji123]