Ratiba ya tendo la ndoa kwa wanandoa na wachumba hudhoofisha upendo wa ndani ya ndoa na kuimarisha upendo nje ya ndoa

Ratiba ya tendo la ndoa kwa wanandoa na wachumba hudhoofisha upendo wa ndani ya ndoa na kuimarisha upendo nje ya ndoa

Tendo la ndoa baina ya wanandoa na wachumba ni chachu na kiungo kimojawapo muhimu sana cha kuimarisha upendo, uaminifu, furaha na muunganiko wa wanandoa au wachumba.

Ni tendo muhimu sana linaloweza kuimarisha na kuchochea zaidi uimara wa ndoa au uchumba likitumiwa vizuri, kwa hiyari, ubunifu, ustadi, maarifa, umahihiri, unyenyekevu, utayari na kwa utoshelevu.

Lakini pia likitumiwa vibaya kana kwamba ni adhabu, karaha, usumbufu, uchafu au uonevu basi, upendo ndani ya ndoa au uchumba huo unaweza kuchomoka na kutafuta makazi mahala pengine kwa faraja ya muda ya kificho.

Kupanga ratiba ya kufanya tendo la ndoa kwa wana ndoa au wachumba ni mwanya au uchepushaji wa upendo wa ndani ya ndoa kwenda nje ya ndoa. Tendo la ndoa lifanyike wakati wowote bila ratiba, wanandoa au wachumba wanapopata joto la kuhisi kufanya tendo, iwe sebuleni nyakati za usiku mkalai, jikoni watoto wakiwa shule, chumbani na mahali popote tulivu pa faragha panapo weza kuwapa uhuru na kuwasitiri haja stahiki.

Kila la kheri sana...
😅😅 Ukiona kuna ratiba ya tendo la ndoa ndani ya ndoa jua mambo hayako sawa, na shida inakuaga moja tu sanasana:
Mke ndo mwenye nguvu na sauti ndani, afu mwamba anamuogopa kichizi mkewe, anajifichia kwenye mwamvuli wa kujali.

Tujitathmini sana, kuna mwamba anateseka sana dom huko, ndani ya miaka miwili kapewa unyumba mara mbili.
 
Dah! Pole sana mwamba!! Nna mwanangu anamwaka wa pili.
Kunashida hapo.
 
ungesoma taratibu kwa utulivu bila papara ungenielewa vizuri zaidi, japo kwa kiasi pia umenielewa haidhuru.

nimesema tendo la ndoa ni miongoni au ni moja kati ya vichocheo au viungo vya kuimarisha upendo, furaha, uaminifu n.k kwa wanandoa na wachumba...

na kwa taarifa yako jambo hili halikwepeki kwa tajiri au Maskini, na kwahivyo haliwezi kuwa wazo la kitajiri au kimaskini. Linahusu wanadamu wenye hisia, vichocheo na mahitaji ya kimwili.

Lakini tendo lile sio tu kwaajili ya kupata watoto. Ni starehe pia. Vipi kwa ambao hawana haja ya kupata watoto au tayari wamefunga kupata watoto. Bado wanafanya tendo ili wapate watoto? Anyway hii haikua hoja kwenye bandiko langu, nashukuru kwa mtazamo wako huu na mengine uliyoyadadavua vizuri sio maoni mabaya ni mazuri sana tu.

Katika jamii tunamoishi jambo hili la kupanga siku za kufanya tendo linaleta shida miongoni mwa wanandoa ndio maana nikona ni vema kulisanua na kushirikisha waungwa ili kupata maoni ikiwa lina afya ama laa.

Kwa maoni yangu naona si sawa kama nilivyoeleza kwenye bandiko..
Ukiruhusu ratiba ya tendo la ndoa ndani basi we ni lazima mnyenyekevu sana kwa huyo mwanamke.

Mwanamume akinyenyekezwa na mwanamke, matokeo yake mara nyingi sio mazuri.
 
Duh! Kumbe kwenye mambo ya malavidavi nako upo? Mi nilidhani we ni wa siasa tu!
 
Nipangiwe ratiba si ntapiga mtu? Hivi kama kuna demu wa nje na ndani nimepangiwa ratiba si naenda kwa wa nje kutoa hamu! Uzuri single mama wamekuwa wengi unajitwalia tani yako utakavyo. Mke wa nyumbani atajua mwenyewe na ratiba zake za kutoa penzi
 
Back
Top Bottom