Mkuu
Palantir,
Ahsante kwa kunikaribisha vinginevyo huenda nisingeuona huu mjadala manake nimetingwa kidogo! Baadae nita-force kupata muda nije kupitia maoni ya wadau hapo juu!
Back to the topic.
Binafsi, huyu Indian Hero nilikuwa sijawahi kumsikia na kwahiyo thanks to
Dumbuya.
Pamoja na yote hayo, ngoja nichangie jambo moja kwamba kwanini nadhani RAW walimpotezea Black Tiger!!
Hapa sina shaka, RAW wenyewe ndo wanajibu sahihi.
Hata hivyo, kwa maoni yangu naona Black Tiger alikuwa 100% ASSET kwa RAW huku akiwa na percentage ndogo sana ya kuwa LIABILITY kwao!
Ni kama naji-contradict but am not!
Kwa mtazamo wangu, naona kuna sababu kubwa 2 za kufanya Spy swap au kufanya jaribio lolote la kumuokoa Jasusi aliyedakwa!
1. Sababu ya kwanza ni kujenga confidence... kuwafanya Deep Cover Operatives wa-feel so secured kwamba, cku likiwakuta basi agency itafanya kila iwezalo kuwaokoa.
Yale mambo ya "if you're caught, you're on your own" they don't work pretty good... yana-demoralize!
2. Sababu nyingine ni hofu kwamba, Agent aliyedakwa anaweza kumwaga siri zaidi akiona agency yake imemtosa.
Kwamba, Jasusi limedakwa lakini pamoja na mateso yote bado anakaza kuongea chochote USEFUL kwa sababu anaamini anaweza kuokolewa either through Spy swap or through any Spy trade!
Lakini akiona agency yake imemtosa, wengine option inayobaki ni kutoa siri in exchange for something!
Sasa turudi kwa Black Tiger.
Ukifuatilia historia yake, anaonekana wazi hakuifahamu vizuri RAW cuz', baada tu ya kuwa recruited na kupewa mafunzo ya kikachero; akavuka border na kuingia Pakistan.
Aidha, kuna uwezekano mkubwa kwamba kabla hajavuka border, Security Clearance yake ilikuwa ya kawaida ambayo isingemwezesha kuwa na access to top secret.
Hii maana yake ni kwamba Black Tiger aliondoka India wakati akiifahamu RAW kijuu juu tu na kwahiyo, kudakwa kwake hakuwa threat (LIABILITY) to RAW kv RAW yenyewe hakuifahamu vizuri!
Na kwavile hakuwa threat, nadhani ndo maana RAW waliamua kumchinjia baharini. Waliamini hata kama angesagwa namna gani, asingekuwa na siri ya kuitoa kiasi cha kuwa threat kwa RAW au any Indian intelligence agency.
Kinyume chake, kama angekuwa amekaa RAW kwa muda mrefu kiasi cha kufahamu mengi (top secrets + secrets) kuhusu RAW, I think ingekuwa ni story tofauti!
I believe RAW wangekuwa tayari kufanya spy trade kwa hofu asije kutoa siri zaidi!
Aidha, suala la Pakistan kutaka maongezi baada ya kuwa wamemdaka Black Tiger; ni dalili tosha kwamba hawakupata chochote cha maana toka kwake!! Hawakupata kwa sababu hakuwa nacho!
kwahiyo; kuliko kukosa yote, inaonekana Pakistan walishakuwa tayari for any tangible Spy trade!
Kwa bahati mbaya, Wahindi wakakaza kv walijua wamedaka "Joka la Kibisa!"
That brings us to Hoja #2... kwanini basi hawakumwokoa ili kuwapa nguvu maajenti wengine kwamba, in case of anything, wapo pamoja nao?!
Binafsi sioni sababu ya ku-justify kitendo walichomfanyia unless kama ndo policy yao!! Kwamba, ile policy ya "if you are caught, you're on your own", kwao haina mjadala!
Na kwa kuangalia uadui uliopo kati ya India & Pakistan, naweza kuwaelewa... kwamba, kuliko kukiri hadharani kwamba una deep cover operatives ndani ya military and/or intelligence community ya adui yako; ni kheri kukana jumla!