Wick
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 8,313
- 12,170
Matokeo yake syria imekuwa uwanja wa kujaribu silaha mpya!..Kweli wamepigwa sana huko Syria, yaani hakufai kabisa. Kila mtu anamvizia mwenzake halafu wanajeshi wao hawagusani kwa moja kwa moja.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Matokeo yake syria imekuwa uwanja wa kujaribu silaha mpya!..Kweli wamepigwa sana huko Syria, yaani hakufai kabisa. Kila mtu anamvizia mwenzake halafu wanajeshi wao hawagusani kwa moja kwa moja.
✔✔✔Moja ya Changamoto kubwa sana kwenye mambo ya vita katika Karne hii ya 21 ni haya Majeshi binafsi, kwa lugha ya kitaalamu wanasema PRIVATIZATION OF THE MILITARY. Imefikia kipindi Serikali hazitumi tena wanajeshi wake na majasusi wake bali zinaajiri makampuni binafsi kufanya hizo kazi za kijeshi: Sasa kama makampuni binafsi yanaenda kufanya shughuli kubwa unategemea hawatakuwa na silaha nzito kweli ??? Kibaya zaidi ni kwamba Sheria za vita zilitengenezwa kwa kuwalenga wanajeshi wa nchi, makundi ya wadai uhuru na makundi ya waasi lakini hazikuyalenga haya makampuni binafsi ya ulinzi. Mfano kuna mikataba ya kimataifa inayohusu Vita inaitwa The GENEVA CONVENTION ya mwaka 1949, hii imewagusa tu wanajeshi wa nchi husika. Mpaka sasa hakuna Sheria au Mkataba wa kimataifa ambao umetengenezwa ili kuyabana haya makampuni binafsi ya Ulinzi ambayo yanaweza kumiliki silaha nzito.
Hapa kuna hatari kubwa kwasababu hizi silaha na teknolojia zinaweza kuangukia kwenye mikono ya magaidi na wakafanya mambo ya ajabu msiamini. Hivi kama wale BLACK WATERS wanapigana na wanajeshi wa Iraq na kuwaua unadhani hao watu wana silaha ndogo kweli ??? Tatizo hili la watu binafsi kumiliki silaha au jeshi madhara yake tumeyaona sana katika historia. Nchini Uchina miaka mia kadha iliyopita kulikuwa na wafanyabiashara "Merchants" ambao walikuja kupata pesa nyingi sana na wakaanza kumiliki vikosi vikubwa vya wanajeshi wao, hili lilipelekea ufalme wa Uchina kuwa katika vita zisizoisha hadi wakajikuta wamechelewa sana kwenye maendeleo.
Ushahidi mwingine ni K.G.B na Interpol,
Baada ya Urusi kuanguka majasusi wengi waliajiriwa na makundi ya kimafia ambayo mengi yao yalikuwa yanahusika na biashara haramu ya silaha nzito. Kuna jasusi wa K.G.B alikuwa anaitwa Victor Anatoliyevich Bout a.k.a Africa's Merchant of Death. Yeye alikuwa anachukua silaha nzito za kivita kutoka nchi zilizokuwa zinaunda Jumuiya ya kisovieti na kule sehemu kama Congo DRC, Sierra Leone, Angola, Rwanda, Burundi na kwingineko. Kibaya zaidi ni kwamba silaha nyingi zilikuwa zinapitia Bandari ya Dar es Salaam na Mombasa na baadhi ya wakubwa walikuwa wanajua na kushiriki kabisa. Nchi kama Uchina, Iran, India na Korea Kaskazini zilitumia huu mwanya kununua teknolojia nzito kutoka Urusi kupitia watu binafsi.
Sasa hii michezo yote michafu inafanywa kupitia BLACK MARKET kwasababu kukamatwa ni ngumu, hakuna kodi yoyote ile na mataifa mengi yanajihakikishia usiri mkubwa juu ya taarifa zao za manunuzi ya silaha. Yaani ni hatari sana haya makundi ya watu binafsi yanapoanza kufanya biashara za Vita na Ulinzi bila kuwepo na Mikataba maalumu ya kuwabana.
Hebu usiangalie tu kwenye vita ya hizi silaha la Kimakenika bali angali kwenye ulimwengu wa kimtandao sasa "THE WORLD OF CYBER SPACE" ambayo ni sehemu mbaya sana na hatari kuliko zote kwasasa. Watu wanasema INTERNET KNOWS NO BOUNDARIES. Hakuna sheria madhubuti ambayo imejaribu kuzungumzia hatari za mtandao kwenye mambo ya Usalama, NATO peke yao ndiyo walijitahidi kuaandaa THE TALLINN MANUAL inayozungumzia haya mambo. Lakini kuna makampuni makubwa sana ya kimtandao siku hizi, yanaajiri wasomi na wataalamu mbali mbali duniani kote. Yanaweza yakafanya vita ya kimtandao na kusababisha madhara makubwa sana kwa dunia. Hebu angalia makampuni kama GOOGLE, MICROSOFT, FACEBOOK, KASPERSKY na mengineyo jinsi ambavyo yana teknolojia kubwa sana kuliko hata nchi ya Tanzania na vyombo vyake vya Usalama (Haya ni makampuni binafsi). Ushahidi wa hili ni kipindi kile GOOGLE MAPS zimeingia, tulikuwa tunaweza hata kuangalia ramani nzima ya kambi ya jeshi ya LUGALO bure kabisaa.
Binafsi naona shirika kama hili kwa dunia yetu ya sasa ni hatari kuliko wale wanaomiliki RAPTORS au SUKHOI. Tumeona juzi Mark Zuckerberg kapata kashfa ya kuuza taarifa za wateja wake kwa wanasiasa. Nasikia GOOGLE nao wanauza kwa siri taarifa za watumiaji wao (Mimi na wewe) kwa makampuni mengine ya Urembo, Magari, Ngono na muziki ili yaweze kujua mwelekeo wa soko umekaaje. Sasa jiulize kama Tanzania inaingia kwenye Vita na baadhi ya mataifa au makundi ya Kigaidi halafu wakaamua kwenda Google kununua taarifa zao kuhusu Tanzania unadhani nini kitawazuia kuuza ??? Maana katika ubepari haya Makampuni yanachoangalia ni kupata faida kwa gharama yoyote ile.
NB: Mkuu pia usisahahu kwamba mpaka sasa Marekani imeshindwa kuyadhibiti hata makampuni makubwa ya Ulinzi, Silaha na Mafuta. Tumeona jinsi ambavyo makampuni makubwa ya mafuta kama Halliburton na Exxon Mobil yanawachezea wanasiasa wa Marekani ili kufanya migogoro nao wapate faida kubwa. Mfano hai kabisa Vita vya Iraq viliumiza sana Uchumi wa Marekani lakini kampuni la Mafuta la Halliburton lilipata faida mara tano na soko lake la hisa lilipanda balaa. Ukisoma vitabu kama MIDNIGHT IN THE AMERICAN EMPIRE na THE MERCHANTS OF DEATH haya yote kuhusiana na hizi hatari za makampuni binafsi kumiliki nguvu kubwa ya kijeshi. Leo hii kampuni la Exxon Mobil alikokuwepo Rex Tillerson kuna kitengi cha Intellijensia kinafanya kazi kama ambavyo TISS inafanya kwa Tanzania au CIA kwa Marekani. Sasa na jinsi walivyokuwa na pesa sidhani kama leo wakiamua kupigana na nchi kama Tanzania, Kenya, Uganda au Congo DRC tunaweza kushindana nao kwa Urahisi.
Hapa kuna hatari kubwa sana huko mbeleni,
Hapo bado hujagusa makampuni makubwa binafsi ya madawa kama Pfizer, Monsanto, Syngenta, NYSE na mengineyo ambayo mbali tu na kututengenezea madawa yanafanya tafiti hatari sana za silaha za kibaolojia na kuziuzia Serikali zao.
Miaka nyuma kadhaa niliwahi kushirikishwa kwenye tafiti moja inayohusiana na BIO-PIRACY barani Africa nikapewa niwaandikie wale walimu wangu baadhi ya vitu. Ndipo nikapata bahati ya kusoma nyaraka zinazohusu umafia ambao Africa tunafanyiwa na haya makampuni nikabaki nasikitika tu.....
CC: Red Giant , Consigliere, Nalendwa , SirChief , Prof, chige , Maalim Shewedy ,neo1
✔✔✔
Mkuu Malcom... this is best piece of work na ni ukweli mtupu!! Yaani umemaliza yote na hujaacha kitu.
Huyu tapeli Na msaliti wa nchi unamwita mzalendoNamuona Lissu.
Ametapeli nini,mtu akitoa ushauri au mawazo mbadala ndo anakua tapeli?.Huyu tapeli Na msaliti wa nchi unamwita mzalendo
Sijaelewa hapa " Ravinder alikuwa mpenzi wa sanaa za sinema na maonesho na hivyo ilivyofika siku ya mahafali yake mwaka 1975 alikuwemo kwenye kikundi cha maonesho siku hiyo."
"Hatua ya kwanza kwa kijana Nabi aliyekuwa na umri wa miaka 23 kwa sasa ilikuwa ni kujiunga na Chuo Kikuu cha Kashmir akichukua masomo ya sheria (LLB) na mwaka 1975 alimaliza masomo hayo yote"
Mwaka 1975 graduation mbili ya home and away...?
Hawa makampuni bora yasije uku Tz,
Maana Mkulu akikurupuka KICHWA KICHWA akakamata makinikia yao
REVENGE YAKE ITAKUA BALAA KWETU
Aisee,
Hii vita ya uchumi inahitaj akili sana, hasa hasa unapopambana na mtu alokuzd kwa kila kitu tena Kwa gap kubwa.
hakika nimeiona na nimejifunza kituNiseme ukweli nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa mada mbalimbali katika jukwaa hili na
nikatamani nami kuleta bandiko moja ila kutokana na ratiba kuingiliana muda ukawa
hautoshi.
Kuna maneno nimekosa kiswahili chake fasaha na hivyo kutohoa au kutumia neno la kiingereza naomba tuchukuliane katika hilo.
Pia nimeona kabla ya kanuni za Mtandaoni hazijaanza kutugawa ni nafasi ya mwisho kupost ''Anonymously''.Hivyo baada ya kuisoma post ya ''Agent Provocateur'' nikahamasika kuimaliza makala hii. Karibu !!
Source ya taarifa :Ravindra Kaushik - Wikipedia na mitandao mbalimbali.
RAVINDER KAUSHIK
View attachment 756387
Ni kijana aliyezaliwa kutoka familia ya kiPunjabi katika mji wa Sri Ganganagar uliopo karibu kabisa na mpaka wa India na Pakistan,jimbo la Rajasthan tarehe 11 April 1952.Ravinder alikuwa ni mtoto wa J.M Kaushik ambaye alikuwa mwanajeshi mstaafu wa kikosi cha anga (Indian Airforce).J.M Kaushik alikuwa akifanya kazi katika kiwanda cha nguo (Textile Mill) baada ya kustaafu.
Ravinder aliweza kusoma katika shule ya serikali na kufaulu vizuri na kuendelea na masomo ya juu katika chuo cha binafsi jimbo la Uttar Pradesh.Alikuwa ni kijana mtanashati,mwenye akili nyingi na kipaji kikubwa katika sanaa japo akiwa chuoni Lucknow alisomea shahada ya Biashara (B.com).Ravinder pia alikuwa kijana maarufu sana shuleni kutokana na kipaji chake cha kuigiza.
Ravinder alikuwa mpenzi wa sanaa za sinema na maonesho na hivyo ilivyofika siku ya mahafali yake mwanzoni mwa miaka ya 70 (1970's) alikuwemo kwenye kikundi cha maonesho siku hiyo.Ravinder alikuwa maarufu kwa kuwaigiza wapigania uhuru wa India na siku hiyoilikuwa ni nafasi yake ya kuigiza katika ngazi ya kitaifa kwani maonesho hayo yalikusanya watazamaji kutokea vyuo vya jirani na wengine mbalimbali.
Akiwa na umri mdogo wa miaka 21 aliweza kuteka mioyo ya watazamaji katika maonesho ya Sanaa pale Lucknow ambapo kwenye igizo hilo alikuwa ni shushushu wa India aliyekuwa akirubuniwa kutoa taarifa kwa vikosi vya China.Ukakamavu wake wa kuonesha uhimilivu wa hali ya juu pamoja na ustadi katika kuonesha uzalendo uliwafurahisha wote waliokuwepo na kumuweka katika orodha ya waigizaji waliokuwa bora mwaka huo.
Jambo ambalo Ravinder alikuwa halijui ni kuwa katika watazamaji walikuwepo maofisa wa Usalama wa India kutoka kitengo cha Utafiti na Uchambuzi (RAW yaani Reasearch and Analysis Wing) na maisha yake yalikuwa yanaenda kubadilika baada ya maonesho hayo.Zimebakia taarifa chache mno za kijana Ravinder Kaushik baada ya maonesho yale ila rekodi mbalimbali zinasema alifuatwa na maofisa wale wakiwa wamekunwa na kiwango cha ueledi,ushupavu na ujuzi alichoonesha akiigiza kama mwanajeshi wa India na kumshawishi kujiunga na kitengo hicho.
Ravinder hakuwa na pingamizi na inasemekana alikwenda nyumbani na kuaga kuwa anaenda New Delhi kwa ajili ya kufanya kazi ya kutumikia taifa pasi na ufahamu wa yanayo mngojea huko mbeleni.
MAISHA NDANI YA RAW
RAW ni kitengo cha usalama cha India kinachojishughulisha na utafiti na uchunguzi wa mambo ya nje,kilianzishwa mwaka 1968 baada ya kushindwa kwa India katika vita ya mpaka wa Himalaya ambayo inapakana na nchi ya uChina.Kutokana na kushindwa vita hii na nyingine za mara kwa mara katika mipaka yake,India ilianzisha kitengo hiki katika jitihada za kutengeneza ubobezi katika kukusanya taarifa na kujenga uwezo wa kiintelijensia kuweza kutumia taarifa hizo kulinda usalama wa nchi.
RAW iliweza kufanikiwa kuwa kitengo maridadi kabisa kikanda (Asia) na kidunia katika ukusanyaji taarifa na kuweza kushiriki katika matukio mengi kama Uhuru wa Bangladesh na urudishaji wa Jimbo la Sikkim katika mipaka ya India.RAW imejikita katika kukusanya taarifa za nchi za nje,kupambana na ugaidi na kuishauri serikali ya India katika mambo yahusuyo sera za nchi za nje pamoja na usalama wa programu za nyuklia.Wadadisi wengi wanakichukulia kama chombo makini na wanakitambua kama moja ya taasisi nyeti na muhimu katika mhimili wa utawala wa India.
Baada ya kurudi New Delhi (yalipokuwa makao makuu ya RAW),Ravinder alianzishiwa mafunzo mara moja ili kumfundisha maarifa ya ujasusi ya kistadi na ya kitaaluma hasa katika udukuzi wa taarifa na uchunguzi wa maadui bila kusahau mafunzo ya ukakamavu wa mwili.Pia akiwa kama shushushu wa awali (Junior Spy) aliweza kufundishwa lugha ya Urdu na mafundisho ya dini ya kiislamu.Hii ilikuwa ni muhimu sana ukizingatia mission aliyokuwa ameandaliwa mbele yake.Na kutokana na jinsi India iliovyokuwa imejigawanya kidini ilikuwa ni lazima afisa usalama apitie mafunzo yote ya dini ili kumuwezeha kuishi katika jamii ya imani yoyote.
Kijana Ravinder pia aliweza kupewa mafunzo ya hali ya juu yahusuyo hali ya kijiografia ya India na maadaui wote wa nje (hasa Pakistan) ambayo kwa wakati huo ilikuwa ni tishio kwa India kutokana na mafarakano yaliyokuwa yakitokea mara kwa mara katika mipaka ya nchi hizo mbili.Akiwa katika mafunzo hayo ya ukachero Ravinder alitahiriwa pia.
Baada ya miaka miwili ya mafunzo ya hali ya juu Ravinder alikuwa tayari ameiva kwa mission yake na akiwa miongoni mwa vijana bora waliosajiliwa kwa ajili ya mafunzo katika kitengo cha RAW hasa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kitaaluma na kuvaa uhusika pasipo kutambulika.
NABI AHMED SHAKIR – PAKISTAN
India ilikuwa imeshapigana na nchi majirani kadhaa,China na Pakistan zikiwa za karibu zaidi.Kwa muda sasa kitengo cha RAW waliweza kunasa taarifa za kiintelijensia kuhusu vita iliyokuwa inaandaliwa na Pakistan,hivyo kuhitajika hatua za haraka kuweza kuidhibiti ikiwezekana kuizuia kabisa.
Moja kati ya hatua mbalimbali ambazo India ilichukua ni kupeleka mashushushu kupeleleza na kudukua taarifa za kijeshi za Pakistan wakiwa kama maofisa wakazi (Resident agents).Kati ya maafisa waliochaguliwa katika mission hii,Ravinder Kaushik alikuwa mmojawapo ingawa yeye alikuwa na maagizo maalum ya kimkakati kwenda kuishi na kujipenyeza kwenye jeshi la Pakistan ili kukusanya na kutoa taarifa za kiintelijensia kwa RAW hatimae kuwawezesha kujipanga na kuzuia mashambulizi ya kutoka Pakistan.
Kabla ya kufika Kashmir (Pakistan) na kuanza mission yake,Rajinder Kaushik ilibidi kwanza abadilishwe utambulisho na identity yake pamoja na rekodi zake zote za nyuma kufutwa.Na katika zoezi hili akapewa jina jipya la Nabi Ahmed Shakir na kutengenezewa nyaraka zote za utambulisho zenye jina lake jipya la kiislamu ambalo lingemuwezesha kujichanganya kwenye jamii za Pakistan ambazo ni waislamu pasipo kuwa na shida ukizingatia kipaji na ujuzi wa kijasusi alionao kwa sasa.
Nabi Ahmed Shakir alishuka Pakistan akiwa na mission moja tu ; kudukua taarifa za kiintelijensia na kuzipeleka nchini kwake.Haikua kazi rahisi na kutokana na maelezo ya mission yake alikuwa na jukumu la kuingia katika jeshi na kujipenyeza ili kupata fursa ya kudukua taarifa za kiintelijensia.
Hatua ya kwanza kwa kijana Nabi aliyekuwa na umri wa miaka 23 kwa sasa ilikuwa ni kujiunga na Chuo Kikuu cha Kashmir akichukua masomo ya sheria (LLB) na mwaka 1975 alimaliza masomo hayo yote ikiwa ni katika kutengeneza historia nzuri pamoja na kupata nafasi ya kujiunga na jeshi la nchini humo.Kutokana na uwezo wake wa juu kitaaluma alifaulu vizuri na kufuatia utaratibu wa usajili wa jeshi katika vyuo kila mwaka alifanikiwa kujiunga na jeshi kwa ufaulu mzuri aliokuwa nao.
Akiwa afisa mwenye ukakamavu wa hali ya juu,Nabi Ahmed Shakir aliweza kupita mafunzo yote ya jeshi la Pakistan akiwa katika ngazi za awali (ukarani) na baada ya miaka michache aliweza kupanda vyeo mbalimbali ndani ya muda mfupi.
Nabi Ahmed Shakir pia aliendeleza maisha nje ya jeshi kwa kuoa mwanamke wa kipalestina Amanat ambaye alikuwa mtoto wa mmoja wa washonaji wa jeshi na kufanikiwa kupata mtoto mmoja.
Kutoka mwaka 1979,Nabi Ahmed Shakir alikuwa akipitisha taarifa mbali mbali za kimkakati na kijeshi toka Pakistan na kuzipeleka India na kuzidi kujitengenezea umaarufu mkubwa ndani ya RAW na vitengo vingine vya usalama kutokana na uhakika na ubora wa taarifa za kiintelijensia alizokuwa akitoa.Taarifa hizi ziliiwezesha India kuwa mbele kimipango na kimkakati katika kupambana na wapakistan na inasemekana aliweza kuokoa maelfu ya wanajeshi wa kihindi kwa taarifa zake muhimu na za kiintelijensia.Haikuchukua muda mrefu sana akapandishwa cheo na kufika ngazi ya Umeja katika jeshi la Pakistan na kupelekea kuzidi kwa umuhimu wake kwa RAW hata kutunukiwa jina la “Black Tiger'' (Chui Mweusi) na aliyekuwa waziri mkuu wa wakati huo Indira Gandhi ingawa kuna rekodi zinazosema ni waziri wa mambo ya ndani S.B.Chavan ndiye aliyempatia jina hilo.Mambo yalikuwa yanaenda vizuri kwa RAW na Ravinder Kaushik (Nabi Ahmed) lakini bahati yao ilikuwa inakaribia kufika tamati.
INYAT MASIHA NA MWISHO WA NABI AHMED SHAKIR
Mwishoni mwa Septemba mwaka 1983, raia mmoja wa India kwa jina la Inyat Masiha alikamatwa akivuka mpaka kuingia Pakistan.
Kufuatia usaili wa awali,raia huyu alitia mashaka katika maelezo yake na hivyo kupelekwa katika kitengo cha Intelijensia cha Pakistan kuweza kubaini ukweli yakinifu.Kushukiwa kuwa ni shushushu wa India kulimweka Inyat kwenye usimamizi wa hali ya juu pamoja na shinikizo kubwa kutoka katika vikosi hivi vya Pakistan vikimtaka akiri na kusema ukweli juu ya utambulisho wake na dhima ya safari yake (misssion).Ni katika maongezi haya ndipo jina la Nabi Ahmed Shakir ''Black Tiger'' lilivyoweza kuibuka na kupelekea udadisi mkubwa zaidi hata kufikia mateso kwa Inyat na mwishowe kukiri kuwa ni ofisa usalama wa India na alitumwa kumpatia taarifa (maagizo) kadhaa mmoja wa maafisa wao aliyepo nchini humo.
Kutubu huku kwa Inyat ambaye alikuwa ni ofisa wa ngazi za chini kulipelekea uchunguzi mpana zaidi wa kuwepo kwa mashushushu wa kihindi katika ardhi ya Pakistan.Mateso zaidi yalimfata Inyat na kupelekea kutoa maelezo ya afis aliyekuwa anapelekewa maagizo hayo na kupelekea kumtaja Nabi Ahmed Shakir,ambaye kwa wakati huo alikuwa ni meja mwenye heshima katika jeshi la Pakistan.
Hii ilikuwa ni taarifa ya kushtukiza na yenye kuwaacha midomo wazi maofisa usalama wa Pakistan waliokuwepo.Ujumbe huu ulipitishwa kwa wakuu wa idara ya mambo ya ndani na jeshi la ulinzi na ikaagizwa kufanyika kwa uchunguzi mara moja kupata uhakika pasi na shaka yakuwa ni kweli Meja Nabi Ahmed Shakir ni shushushu wa India.
Mkakati ukapangwa wa kumtafuta Nabi na kuweza kumkamata kwenye tukio ''red handed''.Mkakati wenyewe ulikuwa ni Inyat Masiha kutumia lugha ya kijasusi kumpata Nabi kwa mawasiliano ya siri na kisha kupanga nae kukutana kwenye park ambapo maafisa wa Paskistan wangekuwepo kumkamata Nabi Ahmed Shakir.
Tukio hilo linapangwa na kuratibiwa katika umakini na uangalizi wa hali ya juu na baada ya kupokea ujumbe uliokuwa umeandikwa kwa kutumia lugha ya kiintelijensia (codes) ambazo ni wao tu wangeweza kuuelewa, Meja Nabi Ahmed Shabir alijikuta akiamuamini Inyat na kukubali kwenda kukutana nae katika eneo la mapumziko (park).Wakiwa tayari wamefika eneo la tukio,Meja Nabi Ahmed Shakir anakamatwa na kutiwa nguvuni mwa wanausalama wa Pakistan na kuanza safari yake mpya iliyojaa mateso,manyanyaso na ukatili wa hali ya juu.
Baada ya kukamatwa Nabi Ahmed Shakir sasa akiitwa kwa jina lake Ravinder,alipitia shuruba ya mateso makali na makachero wa pakistan kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo katika kambi ya mahojiano Sialkot.Nabi Ahmed (Ravinder Kaushik) alifikishwa mahakamani na kuhukumiwa kunyongwa mnamo mwaka 1985.Hukumu ambayo baada ya rufaa aliweza kupunguziwa na kupata kifungo cha maisha jela.Hii ilikuwa mwaka 1990.
Kipindi chote cha kukamatwa,kuhojiwa na kustakiwa kwa Ravinder Kaushik ''Black Tiger'' ,kitengo cha RAW hakikusema wala kufanya lolote na idara ya
ulinzi na usalama ya India ilikuwa kimya na haikuchukua hatua zozote kumuokoa mwana intelijensia wao aliyekuwa mikononi mwa adui katika ardhi ya maadui.Hata pale makachero wa Pakistan hali wakiwa na ushahidi juu ya Ravinder na Inyat walipojaribu kuanzisha majadiliano ya kimataifa bado walipinga kuwa siyo watu wao na kuwatelekeza bila msaada wowote.
Ravinder alipitia jela mbalimbali zikiwemo Sialkot,Kot Lakhpat na Mianwali ambapo aliishi kwa tumaini la kuwa ipo siku taifa alilolipigania na kulitumikia muda wote litakuja kumuokoa.Kutokana na uduni wa mazingira katika jela za Pakistan pamoja na kuhamishwa mara kwa mara ili kuondoa uwezekano wa mkakati wowote kupangwa kumtorosha,Ravinder alipata maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu na baadae asthma katika jela yenye ulinzi wa hali ya juu ya Mianwali (New Central Jail Mianwali).
Mwaka 2001 takribani miaka 16 toka akamatwe,jasusi makini na hodari katika kazi yake,mwenye weledi na umakini wa hali ya juu alikuwa akipumua pumzi yake ya mwisho ndani ya kuta za jela ya Mianwali.Hakika kifo chake kilikuwa cha kusikitisha na chenye maumivu ya kutisha.Alifariki akiwa mpweke na mwenye kuelemewa na magonjwa.Kutokana na kukataliwa na taasisi za usalama za India,Kaburi lake likajengwa palepale Mianwali nyuma ya jela aliyofia.
Akiwa katika kitanda chake cha mauti,Ravinder alipata kuandika barua kadhaa na kuzituma kwa siri kwa baba yake ambayo moja wapo kuna nukuu ya maneno "Kya Bharat jaise bade desh ke liye kurbani dene waalon ko yahi milta hai?" akimaanisha ''Je haya ndiyo malipo ya mtu kutoa maisha yake kwa kulitumikia taifa la India?''.
Barua hizi za siri zilimfikia baba yake Ravinder,kaka yake na mama yake wa miaka 72.Baba yake alifariki kwa mshtuko wa moyo,na barua mbalimbali za kuomba serikali iingilie suala hili tokea mwaka 1987 ziliishia katika masikio yaliyozibwa.Hazikuzaa matunda zaidi ya majibu kadhaa ya wizara ya mambo ya nje kuwa suala hilo linashughulikiwa nchini Pakistan.
Kipande cha barua mojawapo kutoka kwa mama yake Ravinder kwenda kwa waziri mkuu A.B. Vajpayee kilisomeka , “Had he not been exposed, Kaushik would have been a senior army officer of the Pakistan government by now and (continued in) the coming years (serving India secretly).” yaani ''Kama mwanangu asingebainishwa,angelikuwa katika ngazi za juu kabisa katika jeshi la Pakistan na kuendelea kulitumikia taifa lake la India.''
Familia hii haikupata stahiki zozote kutoka serikalini,ila baada ya kifo cha Ravinder ilianza kupokea fedha za kujikimu kiasi cha Rupees 500 za kihindi na baadae kuongezwa hadi Rupees 2000 na kisha kusitishwa kabisa baada ya kifo cha mama yake Ravinder.
Maswali mengi yaliulizwa kwa Vyombo vya usalama vya India ambavyo vilikuwa kimya katika suala hili,kwa nini hawakuweza kumuokoa jasusi wao namba moja nchini Pakistan ???
1.Je,ni kwa sababu ya kulinda usalama wa makachero/mashushushu wake waliokuwepo nchini Pakistan ???
2.Je,ni kulinda heshima na uadilifu wa taifa (National Intergrity) ??
Moral of the story :
''There is a price to pay for being a patriot '' - '' Kuna gharama za uzalendo''
Dumbuya.
2018.
Utupe mfano kama yupi kiongozi...?Mi nasemaga jasusi wa kweli ni yule ambaye hakamatwi wala kujulikana,naam huyu ndiye jasusi aliyebobea.
Mkuu mi naomba unieleweshe kitu hapo!Niseme ukweli nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa mada mbalimbali katika jukwaa hili na

Mkuu Malcom Lumumba kama ungepewa nafasi ya kutoa maoni nini kifanyike ktk nchi zetu zinazoendelea ili kupambana na hao manguli, ungeshauri nini?Moja ya Changamoto kubwa sana kwenye mambo ya vita katika Karne hii ya 21 ni haya Majeshi binafsi, kwa lugha ya kitaalamu wanasema PRIVATIZATION OF THE MILITARY. Imefikia kipindi Serikali hazitumi tena wanajeshi wake na majasusi wake bali zinaajiri makampuni binafsi kufanya hizo kazi za kijeshi: Sasa kama makampuni binafsi yanaenda kufanya shughuli kubwa unategemea hawatakuwa na silaha nzito kweli ??? Kibaya zaidi ni kwamba Sheria za vita zilitengenezwa kwa kuwalenga wanajeshi wa nchi, makundi ya wadai uhuru na makundi ya waasi lakini hazikuyalenga haya makampuni binafsi ya ulinzi. Mfano kuna mikataba ya kimataifa inayohusu Vita inaitwa The GENEVA CONVENTION ya mwaka 1949, hii imewagusa tu wanajeshi wa nchi husika. Mpaka sasa hakuna Sheria au Mkataba wa kimataifa ambao umetengenezwa ili kuyabana haya makampuni binafsi ya Ulinzi ambayo yanaweza kumiliki silaha nzito.
Hapa kuna hatari kubwa kwasababu hizi silaha na teknolojia zinaweza kuangukia kwenye mikono ya magaidi na wakafanya mambo ya ajabu msiamini. Hivi kama wale BLACK WATERS wanapigana na wanajeshi wa Iraq na kuwaua unadhani hao watu wana silaha ndogo kweli ??? Tatizo hili la watu binafsi kumiliki silaha au jeshi madhara yake tumeyaona sana katika historia. Nchini Uchina miaka mia kadha iliyopita kulikuwa na wafanyabiashara "Merchants" ambao walikuja kupata pesa nyingi sana na wakaanza kumiliki vikosi vikubwa vya wanajeshi wao, hili lilipelekea ufalme wa Uchina kuwa katika vita zisizoisha hadi wakajikuta wamechelewa sana kwenye maendeleo.
Ushahidi mwingine ni K.G.B na Interpol,
Baada ya Urusi kuanguka majasusi wengi waliajiriwa na makundi ya kimafia ambayo mengi yao yalikuwa yanahusika na biashara haramu ya silaha nzito. Kuna jasusi wa K.G.B alikuwa anaitwa Victor Anatoliyevich Bout a.k.a Africa's Merchant of Death. Yeye alikuwa anachukua silaha nzito za kivita kutoka nchi zilizokuwa zinaunda Jumuiya ya kisovieti na kule sehemu kama Congo DRC, Sierra Leone, Angola, Rwanda, Burundi na kwingineko. Kibaya zaidi ni kwamba silaha nyingi zilikuwa zinapitia Bandari ya Dar es Salaam na Mombasa na baadhi ya wakubwa walikuwa wanajua na kushiriki kabisa. Nchi kama Uchina, Iran, India na Korea Kaskazini zilitumia huu mwanya kununua teknolojia nzito kutoka Urusi kupitia watu binafsi.
Sasa hii michezo yote michafu inafanywa kupitia BLACK MARKET kwasababu kukamatwa ni ngumu, hakuna kodi yoyote ile na mataifa mengi yanajihakikishia usiri mkubwa juu ya taarifa zao za manunuzi ya silaha. Yaani ni hatari sana haya makundi ya watu binafsi yanapoanza kufanya biashara za Vita na Ulinzi bila kuwepo na Mikataba maalumu ya kuwabana.
Hebu usiangalie tu kwenye vita ya hizi silaha la Kimakenika bali angali kwenye ulimwengu wa kimtandao sasa "THE WORLD OF CYBER SPACE" ambayo ni sehemu mbaya sana na hatari kuliko zote kwasasa. Watu wanasema INTERNET KNOWS NO BOUNDARIES. Hakuna sheria madhubuti ambayo imejaribu kuzungumzia hatari za mtandao kwenye mambo ya Usalama, NATO peke yao ndiyo walijitahidi kuaandaa THE TALLINN MANUAL inayozungumzia haya mambo. Lakini kuna makampuni makubwa sana ya kimtandao siku hizi, yanaajiri wasomi na wataalamu mbali mbali duniani kote. Yanaweza yakafanya vita ya kimtandao na kusababisha madhara makubwa sana kwa dunia. Hebu angalia makampuni kama GOOGLE, MICROSOFT, FACEBOOK, KASPERSKY na mengineyo jinsi ambavyo yana teknolojia kubwa sana kuliko hata nchi ya Tanzania na vyombo vyake vya Usalama (Haya ni makampuni binafsi). Ushahidi wa hili ni kipindi kile GOOGLE MAPS zimeingia, tulikuwa tunaweza hata kuangalia ramani nzima ya kambi ya jeshi ya LUGALO bure kabisaa.
Binafsi naona shirika kama hili kwa dunia yetu ya sasa ni hatari kuliko wale wanaomiliki RAPTORS au SUKHOI. Tumeona juzi Mark Zuckerberg kapata kashfa ya kuuza taarifa za wateja wake kwa wanasiasa. Nasikia GOOGLE nao wanauza kwa siri taarifa za watumiaji wao (Mimi na wewe) kwa makampuni mengine ya Urembo, Magari, Ngono na muziki ili yaweze kujua mwelekeo wa soko umekaaje. Sasa jiulize kama Tanzania inaingia kwenye Vita na baadhi ya mataifa au makundi ya Kigaidi halafu wakaamua kwenda Google kununua taarifa zao kuhusu Tanzania unadhani nini kitawazuia kuuza ??? Maana katika ubepari haya Makampuni yanachoangalia ni kupata faida kwa gharama yoyote ile.
NB: Mkuu pia usisahahu kwamba mpaka sasa Marekani imeshindwa kuyadhibiti hata makampuni makubwa ya Ulinzi, Silaha na Mafuta. Tumeona jinsi ambavyo makampuni makubwa ya mafuta kama Halliburton na Exxon Mobil yanawachezea wanasiasa wa Marekani ili kufanya migogoro nao wapate faida kubwa. Mfano hai kabisa Vita vya Iraq viliumiza sana Uchumi wa Marekani lakini kampuni la Mafuta la Halliburton lilipata faida mara tano na soko lake la hisa lilipanda balaa. Ukisoma vitabu kama MIDNIGHT IN THE AMERICAN EMPIRE na THE MERCHANTS OF DEATH haya yote kuhusiana na hizi hatari za makampuni binafsi kumiliki nguvu kubwa ya kijeshi. Leo hii kampuni la Exxon Mobil alikokuwepo Rex Tillerson kuna kitengi cha Intellijensia kinafanya kazi kama ambavyo TISS inafanya kwa Tanzania au CIA kwa Marekani. Sasa na jinsi walivyokuwa na pesa sidhani kama leo wakiamua kupigana na nchi kama Tanzania, Kenya, Uganda au Congo DRC tunaweza kushindana nao kwa Urahisi.
Hapa kuna hatari kubwa sana huko mbeleni,
Hapo bado hujagusa makampuni makubwa binafsi ya madawa kama Pfizer, Monsanto, Syngenta, NYSE na mengineyo ambayo mbali tu na kututengenezea madawa yanafanya tafiti hatari sana za silaha za kibaolojia na kuziuzia Serikali zao.
Miaka nyuma kadhaa niliwahi kushirikishwa kwenye tafiti moja inayohusiana na BIO-PIRACY barani Africa nikapewa niwaandikie wale walimu wangu baadhi ya vitu. Ndipo nikapata bahati ya kusoma nyaraka zinazohusu umafia ambao Africa tunafanyiwa na haya makampuni nikabaki nasikitika tu.....
CC: Red Giant , Consigliere, Nalendwa , SirChief , Prof, chige , Maalim Shewedy ,neo1
Mkuu mi naomba unieleweshe kitu hapo!
Huyo jamaa pamoja na kubadikisha utambulisho na kuanza chuo akiwa na utambulisho mpya! Hilo jeshi la Pakistani linauzembe kiasi gani kumuajiri mtu bila kujua history yake?
Huo utambulisho aliobadilisha bila shaka ulikua kujifanya ni raia wa Pakistani. Kwahiyo hilo jeshi halikuweza kufuatilia taarifa za huyo jamaa kujiridhisha kuhusu familia yake, maeneo aliyokulia, shule alizosoma mpaka kufika hapo chuo.