Moja ya Changamoto kubwa sana kwenye mambo ya vita katika Karne hii ya 21 ni haya Majeshi binafsi, kwa lugha ya kitaalamu wanasema PRIVATIZATION OF THE MILITARY. Imefikia kipindi Serikali hazitumi tena wanajeshi wake na majasusi wake bali zinaajiri makampuni binafsi kufanya hizo kazi za kijeshi: Sasa kama makampuni binafsi yanaenda kufanya shughuli kubwa unategemea hawatakuwa na silaha nzito kweli ??? Kibaya zaidi ni kwamba Sheria za vita zilitengenezwa kwa kuwalenga wanajeshi wa nchi, makundi ya wadai uhuru na makundi ya waasi lakini hazikuyalenga haya makampuni binafsi ya ulinzi. Mfano kuna mikataba ya kimataifa inayohusu Vita inaitwa The GENEVA CONVENTION ya mwaka 1949, hii imewagusa tu wanajeshi wa nchi husika. Mpaka sasa hakuna Sheria au Mkataba wa kimataifa ambao umetengenezwa ili kuyabana haya makampuni binafsi ya Ulinzi ambayo yanaweza kumiliki silaha nzito.
Hapa kuna hatari kubwa kwasababu hizi silaha na teknolojia zinaweza kuangukia kwenye mikono ya magaidi na wakafanya mambo ya ajabu msiamini. Hivi kama wale BLACK WATERS wanapigana na wanajeshi wa Iraq na kuwaua unadhani hao watu wana silaha ndogo kweli ??? Tatizo hili la watu binafsi kumiliki silaha au jeshi madhara yake tumeyaona sana katika historia. Nchini Uchina miaka mia kadha iliyopita kulikuwa na wafanyabiashara "Merchants" ambao walikuja kupata pesa nyingi sana na wakaanza kumiliki vikosi vikubwa vya wanajeshi wao, hili lilipelekea ufalme wa Uchina kuwa katika vita zisizoisha hadi wakajikuta wamechelewa sana kwenye maendeleo.
Ushahidi mwingine ni K.G.B na Interpol,
Baada ya Urusi kuanguka majasusi wengi waliajiriwa na makundi ya kimafia ambayo mengi yao yalikuwa yanahusika na biashara haramu ya silaha nzito. Kuna jasusi wa K.G.B alikuwa anaitwa Victor Anatoliyevich Bout a.k.a Africa's Merchant of Death. Yeye alikuwa anachukua silaha nzito za kivita kutoka nchi zilizokuwa zinaunda Jumuiya ya kisovieti na kule sehemu kama Congo DRC, Sierra Leone, Angola, Rwanda, Burundi na kwingineko. Kibaya zaidi ni kwamba silaha nyingi zilikuwa zinapitia Bandari ya Dar es Salaam na Mombasa na baadhi ya wakubwa walikuwa wanajua na kushiriki kabisa. Nchi kama Uchina, Iran, India na Korea Kaskazini zilitumia huu mwanya kununua teknolojia nzito kutoka Urusi kupitia watu binafsi.
Sasa hii michezo yote michafu inafanywa kupitia BLACK MARKET kwasababu kukamatwa ni ngumu, hakuna kodi yoyote ile na mataifa mengi yanajihakikishia usiri mkubwa juu ya taarifa zao za manunuzi ya silaha. Yaani ni hatari sana haya makundi ya watu binafsi yanapoanza kufanya biashara za Vita na Ulinzi bila kuwepo na Mikataba maalumu ya kuwabana.
Hebu usiangalie tu kwenye vita ya hizi silaha la Kimakenika bali angali kwenye ulimwengu wa kimtandao sasa "THE WORLD OF CYBER SPACE" ambayo ni sehemu mbaya sana na hatari kuliko zote kwasasa. Watu wanasema INTERNET KNOWS NO BOUNDARIES. Hakuna sheria madhubuti ambayo imejaribu kuzungumzia hatari za mtandao kwenye mambo ya Usalama, NATO peke yao ndiyo walijitahidi kuaandaa THE TALLINN MANUAL inayozungumzia haya mambo. Lakini kuna makampuni makubwa sana ya kimtandao siku hizi, yanaajiri wasomi na wataalamu mbali mbali duniani kote. Yanaweza yakafanya vita ya kimtandao na kusababisha madhara makubwa sana kwa dunia. Hebu angalia makampuni kama GOOGLE, MICROSOFT, FACEBOOK, KASPERSKY na mengineyo jinsi ambavyo yana teknolojia kubwa sana kuliko hata nchi ya Tanzania na vyombo vyake vya Usalama (Haya ni makampuni binafsi). Ushahidi wa hili ni kipindi kile GOOGLE MAPS zimeingia, tulikuwa tunaweza hata kuangalia ramani nzima ya kambi ya jeshi ya LUGALO bure kabisaa.
Binafsi naona shirika kama hili kwa dunia yetu ya sasa ni hatari kuliko wale wanaomiliki RAPTORS au SUKHOI. Tumeona juzi Mark Zuckerberg kapata kashfa ya kuuza taarifa za wateja wake kwa wanasiasa. Nasikia GOOGLE nao wanauza kwa siri taarifa za watumiaji wao (Mimi na wewe) kwa makampuni mengine ya Urembo, Magari, Ngono na muziki ili yaweze kujua mwelekeo wa soko umekaaje. Sasa jiulize kama Tanzania inaingia kwenye Vita na baadhi ya mataifa au makundi ya Kigaidi halafu wakaamua kwenda Google kununua taarifa zao kuhusu Tanzania unadhani nini kitawazuia kuuza ??? Maana katika ubepari haya Makampuni yanachoangalia ni kupata faida kwa gharama yoyote ile.
NB: Mkuu pia usisahahu kwamba mpaka sasa Marekani imeshindwa kuyadhibiti hata makampuni makubwa ya Ulinzi, Silaha na Mafuta. Tumeona jinsi ambavyo makampuni makubwa ya mafuta kama Halliburton na Exxon Mobil yanawachezea wanasiasa wa Marekani ili kufanya migogoro nao wapate faida kubwa. Mfano hai kabisa Vita vya Iraq viliumiza sana Uchumi wa Marekani lakini kampuni la Mafuta la Halliburton lilipata faida mara tano na soko lake la hisa lilipanda balaa. Ukisoma vitabu kama MIDNIGHT IN THE AMERICAN EMPIRE na THE MERCHANTS OF DEATH haya yote kuhusiana na hizi hatari za makampuni binafsi kumiliki nguvu kubwa ya kijeshi. Leo hii kampuni la Exxon Mobil alikokuwepo Rex Tillerson kuna kitengi cha Intellijensia kinafanya kazi kama ambavyo TISS inafanya kwa Tanzania au CIA kwa Marekani. Sasa na jinsi walivyokuwa na pesa sidhani kama leo wakiamua kupigana na nchi kama Tanzania, Kenya, Uganda au Congo DRC tunaweza kushindana nao kwa Urahisi.
Hapa kuna hatari kubwa sana huko mbeleni,
Hapo bado hujagusa makampuni makubwa binafsi ya madawa kama Pfizer, Monsanto, Syngenta, NYSE na mengineyo ambayo mbali tu na kututengenezea madawa yanafanya tafiti hatari sana za silaha za kibaolojia na kuziuzia Serikali zao.
Miaka nyuma kadhaa niliwahi kushirikishwa kwenye tafiti moja inayohusiana na BIO-PIRACY barani Africa nikapewa niwaandikie wale walimu wangu baadhi ya vitu. Ndipo nikapata bahati ya kusoma nyaraka zinazohusu umafia ambao Africa tunafanyiwa na haya makampuni nikabaki nasikitika tu.....
CC:
Red Giant ,
Consigliere,
Nalendwa ,
SirChief ,
Prof,
chige ,
Maalim Shewedy ,
neo1