Ravinder Kaushik ''Black Tiger'' : Jasusi mbobezi aliyefia jela ya ugenini

✔✔✔
Mkuu Malcom... this is best piece of work na ni ukweli mtupu!! Yaani umemaliza yote na hujaacha kitu.
 
✔✔✔
Mkuu Malcom... this is best piece of work na ni ukweli mtupu!! Yaani umemaliza yote na hujaacha kitu.

Mkuu haya makampuni binafsi yanakoenda yatatuhatarishia usalama wa Nchi na Bara zima kwa Ujumla: Tusipoangalia na kuchukua hatua stahiki yatatushinda mchana kweupe kwasababu yana nguvu sana kuliko hata Colonial Chartered Companies and worse enough they are out of control. Leo hii George Soros na NGO zake ameivuruga Ulaya hakuna mfano, sasa mtu moja kama huyu na nguvu alizonazo atashindwa kusababisha hata vita ya dunia kweli ???
 

Asante kwa kwa angalizo hili.Ilikuwa isomeke miaka ya mwanzoni ya 1970 (early 1970's)..Marekebisho yamefanyika.
 
Hawa makampuni bora yasije uku Tz,

Maana Mkulu akikurupuka KICHWA KICHWA akakamata makinikia yao

REVENGE YAKE ITAKUA BALAA KWETU

Aisee,
Hii vita ya uchumi inahitaj akili sana, hasa hasa unapopambana na mtu alokuzd kwa kila kitu tena Kwa gap kubwa.

Kuna kitabu kimoja nimesahau mwandishi wake ila kina title ya ''From the Battlefield to the Boardroom'' kimeelezea jinsi mikakati mingi ilivyobadilika kutoka kwenye enzi za vita na kuingia katika dunia ya uchumi.Tunaishi katika ulimwengu wa vita zinazopiganiwa kwenye vyumba vya wakurugenzi watendaji badala ya makamanda na majenerali.Karibia kila idara ya haya makampuni makubwa duniani kuna mfumo kama wa jeshi ukiangalia kwa jicho la muandishi.

Kwa kujua au kutokujua makampuni mengi yametumia falsafa za kivita katika kuteka soko jipya,kutengeneza bidhaa mpya nakuitambulisha,kulinda mauzo ya bidhaa zilizopo,kupanua shughuli za biashara na kujipambanua kwa washindani.

Kuna kampuni ilikuwa inaitwa Sears miaka ya 1960 ambayo ilikuwa kubwa na yenye mtandao mkubwa wa matawi lakini bwana mdogo (kwa wakati huo) Sam Walton akiwa anaanza biashara alitumia mbinu ya kumshambulia adui pale alipokuwa hapalindi,kwa kufungua matawi nje ya miji ambako Sears walikuwa hawajafungua.Leo tunayo Walmart na Sam Walton ni kati ya mabilionea wakubwa duniani pamoja na familia yake nzima

''To be certain to take what you attack is to attack a place the enemy does not protect'' - Sun Tzu.

Vita ya uchumi inahitaji akili,mbinu na mikakati ya hali ya juu.Udukuzi na intelijensia ni sehemu kubwa sana ya kukuwezesha kushinda vita hivi la sivyo utapotezwa mapema asubuhi.
 
hakika nimeiona na nimejifunza kitu
 
Mkuu mi naomba unieleweshe kitu hapo!
Huyo jamaa pamoja na kubadikisha utambulisho na kuanza chuo akiwa na utambulisho mpya! Hilo jeshi la Pakistani linauzembe kiasi gani kumuajiri mtu bila kujua history yake?

Huo utambulisho aliobadilisha bila shaka ulikua kujifanya ni raia wa Pakistani. Kwahiyo hilo jeshi halikuweza kufuatilia taarifa za huyo jamaa kujiridhisha kuhusu familia yake, maeneo aliyokulia, shule alizosoma mpaka kufika hapo chuo.
 
Mkuu Malcom Lumumba kama ungepewa nafasi ya kutoa maoni nini kifanyike ktk nchi zetu zinazoendelea ili kupambana na hao manguli, ungeshauri nini?
 
Kazi ya ujasusi ni tamu chungu hasa utakapokuwa umegundulika daah he was pay the price
 

Historia haijaacha mengi ya kuongeleka lakini kwa muktadha wa kipande hiki ni kuwa Rajasthan,mji ulioko mpakani mwa India na Pakistan kwa wingi watu wake wanalafudhi,matamshi na muundo wa mwili wa aina moja tofauti yao kubwa ikiwa ni dini.Upande wa Pakistan ni waislamu (na wanatahiriwa) upande wa India ni wahindu ambao kitamaduni hawafanyi tohara.Na katika vitu vya msingi ambavyo pande hizi mbili zinatofautiana cha kwanza ni dini/imani na ni ngumu kwa mmoja kuvuka kiimani kwenda kwingine hasa kwa wakati uliokuwa na utaifa na udini kama ule (1970's).
Kumbuka hata Mahatma Gandhi aliuliwa na mhindu (India) kwa sababu alionekana anasera za upole kwa wapakistan (waislamu) kitu ambacho wahindu hawakupendezwa nacho kwa kiasi kikubwa.

Ukiacha hicho kipengele kimoja nadhani kwenda na utambulisho mpya nina uhakika ni ule uliokuwa umepandikizwa.Amini ya kuwa kuna majina mengi walikuwa nayo na wangeweza kuchagua ila wakachagua utambulisho wa Nabi A. Shakir kwa sababu ulikuwa na historia inayowezwa kuunganika.Kwenda chuo na kufaulu ni njia moja wapo ya kujenga msingi mzuri wa historia hiyo.Na pia kujenga kwake maisha nje ya jeshi kama kuoa na kuzaa tena hukohuko pakistan ilikuwa ni kielelezo kikubwa.

Lakini kwa ufupi ni makosa kama haya ndiyo yanayotengeneza miundombinu bora ya usimamizi wa taasisi hizi za usalama.Kuwa na uhakika kuwa baada ya tukio hili jeshi la Pakistan lilifumua na kurekebisha mambo mengi kwenye mfumo wake wa usaili wa maofisa wa ngazi zote jeshini humo.
 
sifa kuu ya ujasusi ni uzalendo uliotukuka...unafanya kazi kulinda taifa lako...but ujue utapotea na kumbukumbu zako zote zinafutwa....sijajua baada ya hapo mkewe na mwanawe walipelekwa wapi.......sababu hata kizazi chako kinapotezwa kabisa ili asitokee wa kuja kulipiza kwa kujipenyeza penyeza..... mbya zaidi hakuna application......unakuwa pin pointed....off u go....
 
walipeleka boya likawahi kushikwa duh! lkn si huwa wanafundishwa namna ya kudanganya (poteza maboya na vile mnavyodhani na uthibitisho wa uongo huo ili aaminike)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…