Tetesi: Ray C akimbizwa Muhimbili

Tetesi: Ray C akimbizwa Muhimbili

Nakumbuka kuna vibinti vingi vilikuwa vinatamani kuwa kama Ray C, sijui kama bado wanatamani? Umaarufu ni stress juu ya stress. Watu wanafanya mambo hata ya kijinga ili wawe masupasta, I wish wangechukua muda mchache watafakari nini wanachotaka. Wengi hutumia madawa ya kulevya kama njia ya kukabiliana stress za kubaki kuwa relevant as ukirelax kidogo wengine wanauchukua huo ustar. Maisha simple na content ambayo huleta positive impact kwa jamii ni mazuri sana. Ni muda sasa watu wakarudia misingi ya imani. Maana mengine yote ni ubatili.
 
Hivi Unga unakuaje hadi mtu anashindwa kuacha. Nimetumia vilevi vyote ila hii kitu hii ndo kabisa wala sikujaribu.
wala usitake kuujua asee nikimkumbuka kipenz whitney naskitika pamoja na mwanae wauza unga wote walaanike kwa mauwaji
 
Mwanadada Ray C amekimbizwa hospitali ya rufaa ya Muhimbili asubuhii hii akiwa mahututi. Ugonjwa unaomsumbua haujajulikana, amewahishwa hospitalini hapo asubuhi hii na kaka yake Tony pamoja na mama yake baada ya kupigiwa simu wamfuate huko Kinondoni.

Tuendelee kumuombea kheri dada yetu.
Mimi nitakuwa tofauti na wengi hapa,kama anauguwa kwa ajiri ya unga sitompa pole kamwe na niseme aumwe zaidi asipate nafuu kabisa!lakini kama anaugua kwa ajiri ya Mungu niko tayari kufunga kwa maombi kwake hata mwezi mmoja!
 
Pole Ray C Mungu akuponye poleni familia Mungu awape uvumilivu
 
Princess. Ukiponyoka kwenye Unga Ukimwi Unaanza, Maana Unga na Ukimwi ni Mtu na Mdogo Wake, maana wakisha Maliza Kubwia wanaanza Kushugulikiana. Sasa hapo Kuna kau salama Princess Nifaa?

Unga ni Pepo Baya Sana, ndiyo maana Mtu Akisha Anza Kubwia Ubadilika Hata Sura, yaani unapoteza ualisia wako kabisa, Embu Fikiria Princess, Rayc Alivyo Mzuri Amekosa Nini Maskini ya Mungu, Shetani Anamtumikisha namna hiijamani!

Kazi ya Shetani ni kuku Aibisha uaibike Machonipa watu, watu wamrudie Mungu Jamani Wawa sikilize viongozi wao wa Dini ili wabadilike na Mungu awashindie Jamani.
Prince,sisi ambao hatujaanza kutumia Mungu atusaidie hata tusijaribu kuukaribia.
Na wale wenzetu waliokwisha kutumbukia katika janga hilo Mungu awaopoe huko.
Amen!
 
Nani kakuambia mateja wana muda wa kujisavia shingo ya kizazi wakati starehe yao ni hiyo sukari laini tu dada yangu.
Na nguvu ya kufanya shughuli hiyo anaitoa wapi kama ulimuona Chid ndio utaelewa vizuri
Huyu aliwahi kusaidiwa na Kikwete akiwa madarakani na njia pekee kwake ilikuwa kuacha kubwia sasa kama alirudia haipo njia ya kumsaidia tena ni kusubiri matokeo yoyote yanayoweza kumtokea huyu mrembo.
 
Mungu atamsaidia kwa kumpa nafasi nyingine tena. Get well soon Ray c.
 
Naungana na Nifah hapo kwamba huyu Mdada hakuonesha mabadiliko ana alichagua lifestyle fulani.
Baadae alikuwa hataki tena ushauri,kupiga picha akikaa auchi ikawa zake,yaani ilikuwa inaboa kweli aisee.
Sasa tumuombee nini tena,maana hata sijui nimuombee vipi.
Ngoja nifikirie namna ya kumuombea,maana hapa yale maombi ya mwanzo yalipokelewa kisha mtu karudia tena.
Nitarudi tena
 
Siwezi Kumuonea Huruma Ray C amezaliwa mwaka 1982 ni Mtu mzima Kuingia katika madawa alijua kabisa madhara yake na hayo ndiyo maisha aliyoyachagua kwani hakua mdogo kwa kuona mifano tuu ya watu mbalimbali ya watu Ambao wanatumia mimi naungana na Mkewangu/ Mama enu mdogo Nifah we don't feel sorry for her.
 
Huyu dada anahitaji kusaidiwa; kumlaumu kuwa alijichagulia haya maisha sio sahihi (unless tuna ushahidi wa tunayoyasema). watu wengi hapoa tanzania na kwignineko wanaingia kwenye madawa ya kulevya kwa kudanganywa kama vile kuchanganyiwa katika sigara, vinywaji nk. Ifahamike kuwa mtu akitumia madawa ya kulevya kwa siku tano hadi wiki tu! inatosha kumfanya huyu mtu awe addicted (mteja). Madawa ya kulevya (Cocaine, Heroine) yana physiological dependency, yaani mtu anapoacha kuyatumia anapata mabadiliko ya kimwili (ki-fiziolojia) kama vile, kuharisha, kusikia baridi, kutokwa makamasi, kuona maluweluwe na kuota ndoto za kutisha-hali hii wenyewe ndio huiita ''arosto''. Tusiwanyanyapae hawa watu sio wote waliamua kwa hiari yao, wakiwa wanafahamu possible consequence za haya ''makitu''.
 
Back
Top Bottom