Ray C amtembelea Rais Kikwete Ikulu jijini Dar, amshukuru kwa msaada wa matibabu!

Watu wa kwanza kutoa taarifa hii ni Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu. Ilitolewa katika official capacity na sio mtu binafsi. Kuna watu watajisikia wanyonge sana kuona misaada inaenda kwa wale wenye nyenzo nyingi za kujikwamua.

Thanks.
 
Reactions: FJM
Hata kama tungeona picha za Ursino Estate, si bado angeweza kumfadhili huko kama Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania?

Kwani suala ni sehemu au capacity aliyoitumia kumpa huo msaada?

Suala ni jinsi aliyoitumia kwa sababu rais hata awe wapi bado ni rais tu.

Mimi sioni sababu ya kutangaza kama walivyofanya. Wangeweza kuifanya katika faragha yao tu. Lakini mbele ya waandishi? Why?
 
Reactions: EMT
Hata kama tungeona picha za Ursino Estate, si bado angeweza kumfadhili huko kama Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania?

Kwani suala ni sehemu au capacity aliyoitumia kumpa huo msaada?

Angekuwa Ursino Estate au Msoga angalau angeweza kujitetea kwamba kamsaidia kama Rehema Chalamila kwa sababu ana mahusiano binafsi na Elizabeth Chalamila-Mkwasa kwa siku nyingi ambayo yanajulikana wazi na wafuatiliaji wa mambo.

Kikwete hajakuwa rais tangu azaliwe, ana mahusiano na watu, na akitaka kusaidia wapwa zake kama Jakaya hatuna tatizo na hilo.

Akiwa Ikulu hata akitoa hela zake binafsi, kuna wengine tutasema kampa hadhi ya kumpatia msaada katika nyumba ya taifa kwa suala la binafsi.
 
Suala ni jinsi aliyoitumia kwa sababu rais hata awe wapi bado ni rais tu.

Mimi sioni sababu ya kutangaza kama walivyofanya. Wangeweza kuifanya katika faragha yao tu. Lakini mbele ya waandishi? Why?

Lakini kama aliifanya kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa nini ingeifanya faragha?

Kwa maana nyingine, wananchi hawana haki ya kujua anachofanya Rais wao ikiwa ni pamoja na kutoa misaada?

Hapa nina maana kama alimfadhili kama Rais na siyo kama Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
 
hELA ZAKE MFUKONI? NI KWELI NI MILIONI 80 AU MANENO YA WASWAHILI?
 
Lakini kama aliifanya kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa nini ingeifanya faragha?

Na kwa nini afanye hivyo kama rais? Sasa unachohoji ni kweli. Rais akifanya kazi katika hiyo capacity haitakiwi iwe jambo la faragha. Lakini kwa nini afanye hivyo kama rais? That is the question.
 
Reactions: EMT
jamani. Kweli kila mtu na bahati yake. Yule mama alooza mguu hadi sam mahela kampigia debe kwa watz hakusaidiwa. Yule dada mwathirika wa mabomu tena kwa uzembe wa serikali. Hatujasikia serikali kusema lolote

hakumwendea kikwete, kama anataka naye aende kuomba
 
msaada wa kikwete kwa ray c ni pesa zake binafsi au katoa kwenye kodi zetu?
 
At this point kutenganisha hela binafsi za JK na hela za walipa kodi ni kama kuchanganya maji kutoka katika makopo mawili kwenye ndoo, halafu kujaribu kujua maji yepi yametoka katika kopo lipi.

JK hata mshahara wake unatoka kwa walipa kodi.

Kaandika kitabu gani anachopata royalties? Au ana biashara gani ya kuruhusu hizi frequent extravagances?
 
Labda, kwa sababu siku hizi mpaka vikao vya CCM huwa vinafanyika Ikulu, Rais na wasaidizi wake hawakuona shida yoyote ya hilo tukio kufanyika Ikulu?

Kwamba this practice of using the State House for private functions seems to be acceptable by its owners?
 
nasema ni jambo jema kwasababu kamsaidia ili apone.
shida kwangu ni kwann asingeifanya quietly bila kuhitaj iyo media coverage kwani hii inaacha tashwishwi maskion mwetu kwamba je ni vijana wangapi ambao ni wabuya unga na hajawasaidia ama hajajishughulisha nao?? je mateja walioko pale muhimbili stand nao wakidai hayo ataweza kuwasaidia kifedha?? istoshe angekuwa keen enough he would have think of improving rehab centers so as to deal with many addicts rather than dealing with an individual. and kwa wadhifa wake as president angetumia muda wake kuelimisha tabia kuachwa na nafikiri hakuhitaj hata kutoa mchango huo.
 
Acceptance does not absolve one from culpability.

Wrong is wrong, whether widely accepted or not.

Your statement is admission of guilt, rather than defense, Mr. Defense Attorney.

The crucial matter here is whether this was wrong or right, not whether it is accepted or not.

After all, if you are trying to be ironic with a rhetoric question, I noticed a critique of holding CCM meetings at Ikulu, by none other nevertheless.
 
Reactions: EMT
Na kwa nini afanye hivyo kama rais? Sasa unachohoji ni kweli. Rais akifanya kazi katika hiyo capacity haitakiwi iwe jambo la faragha. Lakini kwa nini afanye hivyo kama rais? That is the question.
mm hata kaufanya hivyo kama raisi sina shaka nako ila shaka yangu ni je atamudu kuwafanyia wengine hivyo?? manake yawezekana alitoa pesa zake mfukon weel and good but je kwa wadhifa wake atamudu kuwafanyia wote the same??

think of mgonjwa aloko pale MOI ambapo bei ya upasuaji imepanda by 30% je mtu huyu akimwendea raisi kutaka msaada kwa kutumia guts kama hizi atamsaidia?? manake yawezekana raisi wetu ni mkarimu sana ila sisi tuna hofu nae tu. ngoja nikaombe msaada wa aunt yangu aliye pooza anayehitaj more than 6 mi kwaajili ya upasuaji.

naungana na wewe kwamba ingebaki kati yao tu ingemuongezea heshima sana kuliko kuwa hivi ilivyo.
 
Na kwa nini afanye hivyo kama rais? Sasa unachohoji ni kweli. Rais akifanya kazi katika hiyo capacity haitakiwi iwe jambo la faragha. Lakini kwa nini afanye hivyo kama rais? That is the question.

Agreed. That's the thrust of the issue.
 
I understand that, but if you don't question a person passing through your land without your explicit permission, it could, in the long run, end up being an easement.
 
naomba kuuliza hivi ukitaka kwenda ikulu kumwona raisi unatakiwa kufanya nini??ama kuchukua hatua gani??
 
I understand that, but if you don't question a person passing through your land without your explicit permission, it could, in the long run, end up being an easement.

The exact rationale of this thread. I hope the relevant handlers are reading.
 
Reactions: EMT
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…