Ray C amtembelea Rais Kikwete Ikulu jijini Dar, amshukuru kwa msaada wa matibabu!

Ray C amtembelea Rais Kikwete Ikulu jijini Dar, amshukuru kwa msaada wa matibabu!

Mpwa wangu anaitwa Macho, ni teja kanisumbua mno,keshavunjwa miguu na magari maratatu akiwa anachota mafuta kwenye tankers zikiwa kwenye foleni.ntafanya mpango niende kwa mkulu aisee,

Au umtumie PM Salva Rweyemamu. nadhani ni member humu JF
 
Atakapokoma kujipendekeza na kiherehere ni pale taje lake hilo litakaporudia kubwia miunga. Kama angetaka kuwasaidia waathirika angepambana na biashara ya madawa badala ya kujifanya anawajali mateja. Si alisema ana orodha ya wafanya biashara wa bwimbwi. Mbona hawakamati kama hana faida nao?
Yaani aibu tuliona sisi watazamaji,nadhani gbta yeye alijilaumu baadaye..
 
Atakapokoma kujipendekeza na kiherehere ni pale taje lake hilo litakaporudia kubwia miunga. Kama angetaka kuwasaidia waathirika angepambana na biashara ya madawa badala ya kujifanya anawajali mateja. Si alisema ana orodha ya wafanya biashara wa bwimbwi. Mbona hawakamati kama hana faida nao?

utajuaje mkuu, si ajabu NA MIMI NIMO.
 
Rais wetu ni mtu wa watu. Ndivyo alivyo, tuendelee kumvumilia kwa wale ambao hatufurahishwi na baadhi ya mambo anayofanya.

Mi nadhani ni zaidi ya hapo. Ni mtu wa sifa.. Kumbuka mara 50cent,mara Usain Bolt, Christiano Ronaldo... kumbuka.
 
Atakapokoma kujipendekeza na kiherehere ni pale taje lake hilo litakaporudia kubwia miunga. Kama angetaka kuwasaidia waathirika angepambana na biashara ya madawa badala ya kujifanya anawajali mateja. Si alisema ana orodha ya wafanya biashara wa bwimbwi. Mbona hawakamati kama hana faida nao?

Kuna wakati Watanzania tutakuja jua kuwa Rais huyu hakuja kwa bahati mbaya. Tumepewa ili tujifunze kitu na ni bonge la lesson.
 

RAY C akimshukuru Rais Kikwete kwa matibabu Ikulu jijini Dar es Salaam leo.Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C watu kushoto,Mama yake mzazi RayC Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na kulia ni Sarah Mtweve Dada yake Ray C. (picha na Freddy Maro).


Msanii wa Kizazi Kipya hapa nchini ,maarufu kama Bongo Flavour, Bi Rehema Chalamila anaejulikana zaidi kama Ray C, leo mchana amefika Ikulu ya Dar-Es-Salaam kumshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa msaada mkubwa wa matibabu yake ambayo yanafanyika jijini Dar-Es-Salaam chini ya uangalizi maalum
Ray C amefika Ikulu akiongozana na mama yake mzazi Bibi Margareth Mtweve ambaye pia amemshukuru Rais Kikwete kwa msaada huo mkubwa ambao umesaidia kurudisha hali ya kawaida ya Ray C.
Rais amempongeza Ray C kwa kukubali hali yake ya kiafya na hatimaye kukubali kupata matibabu ambayo bado anaendelea nayo chini ya uangalizi maalum.
Rais amemtaka mwanamuziki huyo kufuata masharti ya madaktari ili aweze kupona kabisa na hatimaye kurudia hali yake ya mwanzo na kurejea katika shughuli zake za kujitafutia kipato na maisha.
Kwa vile Ray C bado yuko katika matibabu, hatutaweka wazi sehemu anayotibiwa hadi atakapokuwa tayari kabisa kurudi katika shughuli zake rasmi hivyo tunaomba jamii impe ushirikiano huo na kuheshimu taratibu zake za matibabu ili hatimaye aweze kupona kikamilifu.
"MWISHO"
Imetolewa na :
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu-DSM
10 Desemba, 2012
 
Get well soon RAY C tunakumic mno A friend in need is a friend indeed, hongera mno Rais
 
I do not buy this cheap popularity kwa RAIS! Who is Ray C? Rais si kwa mambo madogo kama hayo, huyu nasikia alikuwa anakula madawa ya kulevya, wangapi wanayatumia na amewasaidiaje. Mimi sioni kama ni habari hii ya maslahi ya taifa mapaka ipeewe uzito huu. Achana na wahuni Rais, we ni mtu mkubwa kwa mambo makubwa
 
Hivi hapa tatizo ni kumsaidia Ray C, kumsaidia Teja au Kuirusha kwenye Tv?

Tatizo ni kutumia wadhifa alionao,ofisi tukuka ya umma,chombo cha walipa kodi kimetumika pia kama anafanya publicity vile,au anajaribu kugain sympathy ya kundi fulani la watu.
Vitu vile wangefanya wanaotarajia kugombea Urais sawa.
 
Wana haki ya kushukuru,Ray C kuacha kutumia madawa ya kulevya ni raisi lakini pia ikumbukwe kurudia kutumia madawa ya kulevya ni raisi !kuwa makini!
 
Jamani jamaa kamsaidia msanii mwenzie halafu kuna kitu inaitwa sijui ni payback yaani baada ya kufanya biashara unarejesha kiasi fulani kwa customers wako kama kifuta jasho
Tanzania zaidi uijuavyo.........?????!!!!!!
 
ahahahahahahha jana mi nilitoka povu usiku hapa!
mke mwenza cacico hivi iliwapasa mpka kutafat colour code enh!hebu cheki hyo picha!JK bana kachekaaaje!
 
Last edited by a moderator:
NI JAMBO JENA ALILOFANYA MH.RAIS LKINI SWALI NI JE VP NA WALE WENGINE AMBAO KWANZA KUKUONA TU WANAISHIA PALE KWENYE GETI KAMA UMEGUSWA NA HALI YA MAZARA YA MADAWA YA KULEVYA KWA NINI USIFUNGUE TAASISI ITAKAYO SHUGULIKIA MATATIZO HAYO NA KUWASAIDIA WATU WENGI KULIKO HV MMOJAMMOJA TENA HAO NI WALE WENYE FULSA YA KUTANGANZWA NA MAGAZETI KWA VILE NI WATU MAARUFU MHESHIMIWA RAIS EBU ONE DAY PITA MAENEO YA KINONDONI MANYANYA UJIONEE VIJANA GUVU KAZI YA TAIFA WALIVYOASILIKA KAMA ALIVYOKUWA Ray c nao wanaitaji matibabu.
 
Back
Top Bottom