RC Amos Makalla amaliza mgogoro wa Meya na Mkurugenzi Kinondoni

RC Amos Makalla amaliza mgogoro wa Meya na Mkurugenzi Kinondoni

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amemaliza sintofahamu ya uongozi wa manispaa ilijitokeza Kati ya meya manispaa ya kinondoni Ndg Songoro Mnyonge na mkurugenzi wa manispaa Spora Liana.

Utatuzi wa mgogoro huo umefanyika leo katika kikao Cha pamoja kilichoitishwa leo na mkuu wa mkoa na kuwakutanisha meya na mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni.

Mkuu wa mkoa amewataka viongozi hao kurejea ofisini na kufanya kazi kwa pamoja, kutekeleza miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi.

Kwa upande wa Meya na mkurugenzi wamemaliza tofauti zao na wamehaidi kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi mapana ya wananchi.

photo_2021-05-20_10-16-31.jpg
photo_2021-05-20_10-13-57.jpg
photo_2021-05-20_10-14-01.jpg

photo_2021-05-20_10-14-00.jpg

Zaidi tazama: Video: Malumbano kati ya Meya Isaya Mwita na Mkurugenzi wa Kinondoni Sipora Liana
 
Meya aache ukanjanja.

Kwahiyo baada ya kumaliza tofauti zao watuambie ukweli sasa, nani alikuwa sahihi kati ya Meya na Mkurugenzi, afu hela zetu zirudishwe.

Afu naona Meya kambamba mke wa watu kwa mahaba yote.
 
Kazi nzuri na Mwanzo mwema kwa Mkuu wa Mkoa mwana Simba SC ' Kindakindaki ' Mwenzangu na Mdau Mwenzangu wa Miziki ya Congo ( Misebene ) hasa Bendi yetu pendwa ya Wenge Musica BCBG Ndugu Amos Makalla.

Sina wasiwasi nae Kiuongozi kutokana na Historia yake na najua huu Mkoa atauweza na atapata Ushirikiano wetu wote wana Dar es Salaam tofauti na ilivyokuwa kwa Mpuuzi Mmoja aliyekosa Kura za Maoni za kutosha ndani ya CCM ili agombee Ubunge Jimbo la Kigamboni.

Ila nimeshtushwa kidogo katika hizi Picha namuona Bwana Songoro ' amemuhagi ' Bi. Spora katika hali ya ' Kimahaba ' kabisa tena huku kama vile ' akijibebisha ' Mabegani Kwake na akiwa na Furaha ya 100% na ya Mwenzake Kisaikolojia ikionekana ni ya 50% tu.

Huenda 'Ugomvi' wao ni wa Kibaiolojia.
 
Kazi nzuri na Mwanzo mwema kwa Mkuu wa Mkoa mwana Simba SC ' Kindakindaki ' Mwenzangu na Mdau Mwenzangu wa Miziki ya Congo hasa Bendi yetu pendwa ya Wenge Musica BCBG Ndugu Amos Makalla.

Sina wasiwasi nae Kiuongozi kutokana na Historia yake na najua huu Mkoa atauweza na atapata Ushirikiano wetu wote wana Dar es Salaam tofauti na ilivyokuwa kwa Mpuuzi Mmoja aliyekosa Kura za Maoni za kutosha ndani ya CCM ili agombee Ubunge Jimbo la Kigamboni.

Ila nimeshtushwa kidogo katika hizi Picha namuona Bwana Songoro ' amemuhagi ' Bi. Spora katika hali ya ' Kimahaba ' kabisa tena huku kama vile ' akijibebisha ' Mabegani Kwake na akiwa na Furaha ya 100% na ya Mwenzake Kisaikolojia ikionekana ni ya 50% tu.

Huenda 'Ugomvi' wao ni wa Kibaiolojia.
Mke wa PM mstaafu
 
Back
Top Bottom