RC Amos Makalla amaliza mgogoro wa Meya na Mkurugenzi Kinondoni

RC Amos Makalla amaliza mgogoro wa Meya na Mkurugenzi Kinondoni

Jamaniii wakati huu mgogoro wa Meyya na Mkurugenzi unarushwa hewani, mimi sikuwa na luku so simu ilizima, ninaomba mtanange urudiwe (In Mc Mboneka's Challenge)......... hahahaha dah Hongera sana Mh. Makala.
 
Meya aache ukanjanja.

Kwahiyo baada ya kumaliza tofauti zao watuambie ukweli sasa, nani alikuwa sahihi kati ya Meya na Mkurugenzi, afu hela zetu zirudishwe.

Afu naona Meya kambamba mke wa watu kwa mahaba yote.
Naona watamnyanyasa mpaka aseme poh! Mama Mkurugenzi kaingilia maslahi ya watu na vocha(risiti) zao za shs 1,000! Mradi unamfahidisha hata Mayor!
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amemaliza sintofahamu ya uongozi wa manispaa ilijitokeza Kati ya meya manispaa ya kinondoni Ndg Songoro Mnyonge na mkurugenzi wa manispaa Spora Liana.

Utatuzi wa mgogoro huo umefanyika leo katika kikao Cha pamoja kilichoitishwa leo na mkuu wa mkoa na kuwakutanisha meya na mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni.

Mkuu wa mkoa amewataka viongozi hao kurejea ofisini na kufanya kazi kwa pamoja, kutekeleza miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi.

Kwa upande wa Meya na mkurugenzi wamemaliza tofauti zao na wamehaidi kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi mapana ya wananchi.

View attachment 1792517View attachment 1792518View attachment 1792519
View attachment 1792521


Zaidi tazama: Video: Malumbano kati ya Meya Isaya Mwita na Mkurugenzi wa Kinondoni Sipora Liana
sina chama,!Huu i uungwana nimeukubali.!!
 
Huwezi kunioneaaaaa haki nilicheka mpaka wanasiasa lazima uwe mnafiki hapo ukute wako na kinyongo kama kawa kama Dawa. Mimi siwezi uanasiasa mambo ya unafiki I can't do it..
 
Huu mtanange bado mbichi mno na huenda ndio kwanza unaanza! Sababu no hizi hapa:-
1. Mifumo ya upigaji kwenye usafi, ujenzi na usambazaji wa stationaries uliokuwa unafanywa na vijikampuni vya madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa ilipigwa pini na huyu mama.
2. Zile posho za hovyo na rejareja walizokuwa wanalipana madiwani nazo zimefutiliwa mbali na huyu mama.
3. Zile staili za ajira za rejareja kwa kazi za muda mfupi kujazwa na ndugu na watoto wa madiwani kazipiga panga!
4. Wizi na ubadhirifu wa vifaa vya ujenzi na ujenzi usiozingatia value for money kausiriba vibaya kwani anazama Hadi site kuhesabu tofali, nondo, mbao na tofali!
5. Hataki ujazaji holela wa mafuta na car services zilizo nje ya budget.
Yaani siyo madiwani tu tu hawana furaha na Raha ya kazi Bali hata wafanyakazi wa kawaida hawahemi wakisikia sauti yake kwani anafanya account ya kila iitwayo Senti ya serikali lazima ipitie kwenye mkono wake na aihoji.
Mama kaja na mchumi wake kutoka anakokujua!
Hapa njaa lazima ihamie kwao maana ni kweli manispaa ya kinondoni ilioza kwa kuliwa na mchwa wa kila rangi ambao walifikia kiwango Cha kuwa untouchable na mamalaka zao za uteuzi!
Na Mimi nasema, akamatie hapohapo kwani kuwa mjumbe wa siasa wa ccm mkoa na diwani au meya siyo tiketi ya kufisidi Mali za halmashauri na serikali kwani walio wengi wanazibunya fedha za serikali na hata za force account zinazotokana na makusanyo ya halmashauri! Mama piga wezi hao!
 
Hivi huyu Spora si ndio kipindi kile aliwachoma akina Kangi Lugola et al walivyomuomba rushwa...

Alikwisha mtwisha fedha za TAKUKURU mbunge wa Bahi!!! Songoro asifanye mchezo na huyo mama ni chuma cha moto hata Mwendazake alimtambua!! Sio siri kuwa Kinondoni inajulikana kuwa ni chafu nchi nzima hivyo huyo Meya hawezi kuwa msafi!
 
Barabara ya Kinondoni Makumbusho kupitia Mwananyamala inakaribia mwaka sasa.
 
Back
Top Bottom