Kishimbe wa Kishimbe
JF-Expert Member
- Jul 18, 2013
- 5,566
- 5,477
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na kwa nini RC Makalla asihoji hili,yeye eti anakimbilia kupatanisha!! Hiyo tunaita funika kombe mwanaharamu apite!!Huyu Meya ni mjanja. Yeye na madiwani wake wameiba hela za uzoaji takataka, na Mkurugenzi aliliweka wazi na hawajibu hiyo hoja zaidi ya kumshambulia kibinafsi. Hapa amepiga picha kwa pozi hilo, hakufanya hivyo kwa bahati mbaya. Alijua udhaifu wa watanzania wengi. Alijua kukitokea hoja na mapenzi kwa pamoja, Watanzania watajadili mapenzi waiache hoja. Hapa amefaulu. Watanzania waliomo humu (wanaojiita Great Thinkers) wanajadili pozi la kukumbatia. Hawajadili tena tofauti iliyopo kati ya fedha zilizokusanywa kwa wananchi na kilichoandikwa katika risiti walizopewa. Hawa ni GT wa JF, sasa je waswahili wenzangu huko mtaani, nani atahoji tena? Meya mjanja mjanja hivi, wananchi wajinga wajinga hivi
ugomvi umesha kuwa wa muda mrefu?Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es salaam Amosi Makalla ameanza kazi kwa kishindo
Mheshimiwa Makalla mapema leo amemaliza ugomvi uliodumu kwa muda mrefu kati ya Mstahiki Meya wa Manispaa Kinondoni Mheshimiwa Songoro Mnyonge na Mkurugenzi Bi Spora Liana
Viongozi hao wawili baada ya usuluhishi huo walishikana mkono na kuahidi kuchapa kazi kwa bidii na ushirikiano mkubwa ili kufanikisha utekelezaji wa Ilani ya CCM
Hongera sana RC Makalla
Kazi iendelee
Mi nilifikiria hilo ndiyo litakua swali la kwanza kwa Katibu Mkuu kutoka kwa Waandishi wa habari!!Waliandaa na wapiga picha kabisa hii bongo movie baso inaendelea.
Halafu takataka jana walikutana.na katibu mkuu wa ccm wakashindwa kumwuliza hata swali
🤣🤣Hawa walinyimana mwisho wakaminyana
Huyu Meya muhuni....Hug gani hilo?Meya aache ukanjanja.
Kwahiyo baada ya kumaliza tofauti zao watuambie ukweli sasa, nani alikuwa sahihi kati ya Meya na Mkurugenzi, afu hela zetu zirudishwe.
Afu naona Meya kambamba mke wa watu kwa mahaba yote.
Acha ujinga basi tupo na mama yetu inatosha sanaMakalla for presidency 2030!
Wajinga ndiyo waliwao. Uongozi unajishughulisha na vitu ambavyo siyo majukumu yake. Mkuu wa mkoa anapata wapi muda wa kupoteza eti kuwapatanisha watu na taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari utadhani ametengeneza roketi. Bado tuko nyuma sana sana na viongozi wa aina hii ni mzigo tu.#Mwandishi wetu
21/05/2021
Ni siku Moja imepita tangu katibu Mkuu wa ccm Ndg Daniel Chongolo atowe maelekezo ya Nidhamu kwa watumishi wa serikali na chama alipokuwa akiongea na vyombo vya habari kwa mara ya kwanza jijini Dodoma jana 20/05/2021.
Mkuu wa Mkoa wa Dar ess allam Mh Amos makala leo 21/ 05/2021 ametumia maagizo hayo ya katibu Mkuu kwa kuwaita watendaji Wakuu wa wilaya ya kinondoni Ndg Songoro Mnyonge ambae ni mstahiki meya na Mkurugenzi Wa Manispa bi Spora liana ambao walikuwa katika sintofahamu kubwa Katika utendaji wa Kazi zao.
Aliwaita ofisini Kwake kisha kuongea nao kwa kina na busara kubwa na kuziweka Sawa sintofahamu zao na wote kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano,busara na hekima Kati yao.
Pongezi za dhati zimuende Katibu Mkuu wa CCM Ndg Daniel Chongolo kwa kuliona hili kwa watumishi wote wa chama na serikali na kisha kulitolea maelekezo yenye msisitizo.
Lakini Mh Amos Makala pia awe mfano wa kuigwa popote na kwa yeyote hasa Katika kusimamia maagizo na pia kutumia busara zaidi Katika kutatua na kusawazisha matatizo na sintofahamu Kati ya watumishi.
*SEKTETARIATE MPYA*j
#Kazi Iendelee[emoji1241]View attachment 1792822View attachment 1792824
Je huyo mama amefichua kile alichosema akiendelea kuonewa atasema? Inaelekea kuna uovu huyo Meya aliufanya, huyo mama ana siri kubwa#Mwandishi wetu
21/05/2021
Ni siku Moja imepita tangu katibu Mkuu wa ccm Ndg Daniel Chongolo atowe maelekezo ya Nidhamu kwa watumishi wa serikali na chama alipokuwa akiongea na vyombo vya habari kwa mara ya kwanza jijini Dodoma jana 20/05/2021.
Mkuu wa Mkoa wa Dar ess allam Mh Amos makala leo 21/ 05/2021 ametumia maagizo hayo ya katibu Mkuu kwa kuwaita watendaji Wakuu wa wilaya ya kinondoni Ndg Songoro Mnyonge ambae ni mstahiki meya na Mkurugenzi Wa Manispa bi Spora liana ambao walikuwa katika sintofahamu kubwa Katika utendaji wa Kazi zao.
Aliwaita ofisini Kwake kisha kuongea nao kwa kina na busara kubwa na kuziweka Sawa sintofahamu zao na wote kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano,busara na hekima Kati yao.
Pongezi za dhati zimuende Katibu Mkuu wa CCM Ndg Daniel Chongolo kwa kuliona hili kwa watumishi wote wa chama na serikali na kisha kulitolea maelekezo yenye msisitizo.
Lakini Mh Amos Makala pia awe mfano wa kuigwa popote na kwa yeyote hasa Katika kusimamia maagizo na pia kutumia busara zaidi Katika kutatua na kusawazisha matatizo na sintofahamu Kati ya watumishi.
*SEKTETARIATE MPYA*j
#Kazi Iendelee[emoji1241]View attachment 1792822View attachment 1792824
Acha dhana potofu!!! Si kila mtu moyo mchafu! Ili maadamu lisiwe kama lile busu la Yuda IskariyoteWanakumbatianaje hivyo?
RC Amos Makalla amewakutanisha Meya wa manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wake Sipora Liana. Vyombo vya habari vikaripoti kuwa mgogoro umeisha 🤣.
Je nini kiini cha mgogoro huo unaodaiwa kumalizwa na Makalla?
1. Kulitokea udanganyifu kwenye malipo ya ukusanyaji wa taka. Wenyeviti wa mitaa wakishirikiana na watendaji walikusanya fedha lakini wakatoa risiti zenye figures pungufu. Mkurugenzi akaagiza wakamatwe. Lakini katika hali ya kushangaza watendaji wakachiwa, wakabaki wenyeviti na wajumbe peke yao. Ikaonekana ni double standards. Kwanini kosa wafanye wote lakini wengine waachiwe na wengine washikiliwe?
Wenyeviti wakiwa rumande wakawalilia madiwani wao. Madiwani wakamhoji Mkurugenzi. Akajibu kuwa watendaji walipewa dhanana. Lakini jambo la kustaajabisha Wenyeviti walipoomba dhamana walinyimwa. Mkurugenzi anadaiwa kutoa maelekezo wasitoke hadi sikukuu ya Eid ipite.
Meya akaingilia kati. Akamwambia Mkurugenzi ni kosa kuweka watu ndani siku 5 bila kuwapeleka mahakani. Kama wanatuhumiwa kula pesa za taka wafunguliwe mashtaka na wapelekwe mahakamani. Otherwise wapigiwe hesabu walipe waachiwe. Kukatokea mabishano. Mgogoro ukatiwa ndimu.
2. Mwaka jana Halamshauri hiyo ilitenga Bilioni 1.5 kujenga vyumba vya madarasa ktk shule mbalimbali. Lakini Baraza la madiwani walipokagua walikuta shule nyingi ujenzi haujakamilika. Shule moja walikuta ujenzi upo kwenye hatua ya msingi. Wakatahamaki kwa sababu ujenzi huo unatakiwa kukamilika kabla mwaka mpya wa fedha yani July 1.
Wakamuuliza Mwalimu mkuu akajibu kuwa hajaletewa fedha kutoka Halmashauri. Mkurugenzi aliposikia hivyo akampigia simu mwalimu huyo na kumpa vitisho. Mwalimu akamrekodi na kumtumia Meya. Meya akamuuliza Mkurugenzi kwanini unatisha walimu? Je mwalimu huyo alifanya kosa gani kusema hajapelekewa pesa?
Mkurugenzi akaeleza kuwa Mwalimu huyo alimletea dokezo juzi, hivyo kulaumiwa kwa kutopeleka hela ni kumuonea. Lakini nyaraka zinaonesha kuwa dokezo lipo ofisi ya Mkurugenzi tangu mwezi April. Kama alipewa dokezo April lakini anasema ni "juzi" je alitaka apewe lini ili aone hajaonewa? Mgogoro ukaendelea.
3. Mkurugenzi ametoa tuhuma kuwa Halmashauri ina genge la wezi. Tuhuma hizo ni za mara kwa mara. Meya akamwambia si jambo la busara kila wakati Mkurugenzi kulalamika. Ni vizuri ataje hilo genge la wezi na tuhuma zao ili wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria. Lakini kulalamika kwamba kuna genge la wezi halafu huchukui hatua yoyote si sahihi. Mgogoro ukazidi.
4. Mkurugenzi kujihisi yupo juu ya Meya alisema "mimi natekeleza maagizo kutoka juu, kwenye mamlaka iliyoniteua". Meya akamwambia sheria ya serikali za mitaa no.8 ya mwaka 1982 inamtaka Mkurugenzi kutekeleza maagizo ya baraza la madiwani, sio mamlaka ya uteuzi. Mkurugenzi kusikia hivyo akapanic na kusema "nina sms ya maelekezo kutoka juu nitaisoma mwisho wa kikao" Meya akamuuliza unamtisha nani? Mgogoro ukazidi kukolezwa moto.
#MyTake:
Ni bahati mbaya sana kwamba Wakurugenzi wengi hawajui mipaka ya utendaji wao. Kuna wakurugenzi wana-behave kama maDC, wengine kama mameya, wengine kama maDAS, wengine kama wenyeviti wa CCM wilaya. Yani kila mmoja na akili zake zinavyomtuma. Wakurugenzi wachache sana wanaowaheshimu wenyeviti wao wa halmashauri/Mameya na kujua kwamba hao ndio maboss zao. Kuna wakurugenzi hudhani wanaweza kutoa amri hata kwa vyombo vya dola [emoji1]. Futuhi.!
Sipora alipokua Mkurugenzi wa jiji alimsumbua sana Meya Isaya Mwita. Na kwa kuwa Isaya alitokana na Chadema basi Sipora hakumpa nidhamu anayostahili. Alimburuza na wakati mwingine walibishana hadi kwenye vikao. Kuna siku Sipora alimwambia Isaya "mimi ndiye boss wa jiji la Dar" Nikacheka sana. Nikasema kumbe huyu mama hajui Meya ni boss wake 🤣.
Kuna haja ya kufanya marekebisho ya sheria ili Wakurugenzi waajiriwe katika level za halmashauri. Tumpunguzie Rais mzigo wa kufanya teuzi. Nafasi za Ukurugenzi zitangazwe na Halmashauri husika, watu wenye sifa waombe. Baada ya usaili atakayeajiriwa anaripoti kwa baraza la madiwani kama mamlaka yake ya kazi na nidhamu. Awajibike kwa maslahi ya halmashauri husika. Kwa kufanya hivyo itapunguza migogoro na itasaidia halmashauri nyingi kupiga hatua za kimaendeleo.
By GJ Malissa