RC Amos Makalla amaliza mgogoro wa Meya na Mkurugenzi Kinondoni

RC Amos Makalla amaliza mgogoro wa Meya na Mkurugenzi Kinondoni

Haka ka maza na kenyewe ni katata sana. Si ndio huyu alikuwaa hapatani na Meya Boniphace yule wa Chadema?
 
Huyu Meya ni mjanja. Yeye na madiwani wake wameiba hela za uzoaji takataka, na Mkurugenzi aliliweka wazi na hawajibu hiyo hoja zaidi ya kumshambulia kibinafsi. Hapa amepiga picha kwa pozi hilo, hakufanya hivyo kwa bahati mbaya. Alijua udhaifu wa watanzania wengi. Alijua kukitokea hoja na mapenzi kwa pamoja, Watanzania watajadili mapenzi waiache hoja. Hapa amefaulu. Watanzania waliomo humu (wanaojiita Great Thinkers) wanajadili pozi la kukumbatia. Hawajadili tena tofauti iliyopo kati ya fedha zilizokusanywa kwa wananchi na kilichoandikwa katika risiti walizopewa. Hawa ni GT wa JF, sasa je waswahili wenzangu huko mtaani, nani atahoji tena? Meya mjanja mjanja hivi, wananchi wajinga wajinga hivi
 
Meya mpaka amesinzia ha ha haaa
bi spora naona kumbe Neema za Allah zilimtembelea sio haba.
 
Tutafsirie tu hata kwa hilo kumbato, naona mmoja kakumbatia kwa mikono yote mwingine kakumbatiakwa mmoja, au labda aliogopa kushika kiuno cha wenyewe tumuache tu.
[emoji3][emoji3][emoji3]ugomvi wa mahaba
 
Kwa upande wa Meya na mkurugenzi wamemaliza tofauti zao na wamehaidi kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi mapana ya wananchi.
1621587305686.png
1621587347667.png

Macho yao hayaakisi kusameheana toka moyoni
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amemaliza sintofahamu ya uongozi wa manispaa ilijitokeza Kati ya meya manispaa ya kinondoni Ndg Songoro Mnyonge na mkurugenzi wa manispaa Spora Liana.

Utatuzi wa mgogoro huo umefanyika leo katika kikao Cha pamoja kilichoitishwa leo na mkuu wa mkoa na kuwakutanisha meya na mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni.

Mkuu wa mkoa amewataka viongozi hao kurejea ofisini na kufanya kazi kwa pamoja, kutekeleza miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi.

Kwa upande wa Meya na mkurugenzi wamemaliza tofauti zao na wamehaidi kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi mapana ya wananchi.

View attachment 1792517View attachment 1792518View attachment 1792519
View attachment 1792521
Hapo ni njaa zao wote wanaogopa kutumbuliwa hivyo wameamua kufunika kombe mwanaharamu apite lakini ndani ya mioyo yao ngoma bado mbichi wataishi kwa kuviziana tu.
 
Waliandaa na wapiga picha kabisa hii bongo movie baso inaendelea.
Halafu takataka jana walikutana.na katibu mkuu wa ccm wakashindwa kumwuliza hata swali
 
Kazi nzuri na Mwanzo mwema kwa Mkuu wa Mkoa mwana Simba SC ' Kindakindaki ' Mwenzangu na Mdau Mwenzangu wa Miziki ya Congo ( Misebene ) hasa Bendi yetu pendwa ya Wenge Musica BCBG Ndugu Amos Makalla.

Sina wasiwasi nae Kiuongozi kutokana na Historia yake na najua huu Mkoa atauweza na atapata Ushirikiano wetu wote wana Dar es Salaam tofauti na ilivyokuwa kwa Mpuuzi Mmoja aliyekosa Kura za Maoni za kutosha ndani ya CCM ili agombee Ubunge Jimbo la Kigamboni.

Ila nimeshtushwa kidogo katika hizi Picha namuona Bwana Songoro ' amemuhagi ' Bi. Spora katika hali ya ' Kimahaba ' kabisa tena huku kama vile ' akijibebisha ' Mabegani Kwake na akiwa na Furaha ya 100% na ya Mwenzake Kisaikolojia ikionekana ni ya 50% tu.

Huenda 'Ugomvi' wao ni wa Kibaiolojia.
Si unakumbuka kwenye ule ugomvi alimuuliza 'au una sababu nyingine'?
 
nje ya mada tena, nani kaona furniture na deco alizonakshia ofisi bashite wakati anadumu kwenye nafasi. haha full gsm humo ndani.. af leo mtu yupo benchi
 
Back
Top Bottom