RC Chalamila ahoji kama Bandari imeuzwa mbona soko la Ferry bado lipo. Asema waliopotosha wote wako ndani na wataendelea kukamatwa wakiibuka wengine

Huyu jamaa ni muongo wa kutupa! Sasa anaongea hivyo ili kuwatisha watu au?
 
Ila Chalamila ana vituko sana sasa Bandari na soko la feri mbona ni kama mchana na usiku.

Nae hapo akajiona kaongea😁

Ila inasemekana ni kiongozi ambae muda yote anampigia kampeni samia yani anahakikisha katika kila jambo kampromoti iwe msibani,kanisani,michezoni hata barabarani ni moja ya mbinu anatumia kulinda ugali wake
 
Aina ya Viongozi kama hawa wamebakia Tanzania pekee
Hakika kuna huyu na IGP wambura😁

Moja kati ya kauli zao za kushangaza ni hii Chalamila kusema bandari haijauzwa na ndio mana soko la ferry bado lipo😁 na wambura kusema rais atapinduliwa😁

Hizi kauli za viongozi hawa zinadhihirisha ni jinsi gani tulivyo na viongozi wa ajabu katika Taifa hili ambao ni wasaidizi wa Rais

Wazungu wanasema gabbage in gabbage out
 
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama DSM ,anataka kuvuluga maji !!!
 
Mambo ya kitoto myaache hukohuko kwa wenyewe msituletee humu.
 
Kumbe anadharau kiasi hicho. Ningekuwa kwenye kundi hilo ningemjibu" je sisi unatuona wajinga Sana Hadi utwambie mbona soko la ferry Bado lipo?" Kauli yake na yule aliyesema "wanasema bandari imeuzwa mbona haijawekwa mfukoni na kuondoka "? Ina tofauti Gani. Hawa Jamaa kumbe huwa wanaona wavuvi na wananchi wa kawaida ni wajinga. Kwamba hawawezi kuchanganua mambo
 
Hawa jamaa wanawachukulia wabongo kama mbumbumbu mzungu wa reli, kwani bandari,ni Mali inayohamishika?
Ukiuza nyumba ya familia yako, uliyemuuzia anaibeba na kuondoka nayo? Nikiamua kuiacha vile vile, nikaipangisha, wanao wakija wanaiona ipo vile vile, wanaweza, wakasema ni yao, wakati hawafsidiki chochote, hawaishi humo, hawawezi kuingia, kama imepangishwa, hawali rent!
Kuuzwa sio lazima uamishe, kenge sana huyu mbwa
 
AtajielewA baadaye
 
Kina Chalamila wapo wengi sana kwenye hii Nchi., kikubwa mambo yake yanaenda na ugali unakuja mezani kwa wakati. Ni wale waliosemwa na Nyerere enzi zile vijana wa hovyo kabisa kila kitu ndiyo bwana mkubwa.
 
Kashalewa madaraka huyu tayari
 
ushahidi hakuna mkuu ila kuna maneno ya hovyo2
 
Imagine this mindset ya RC 🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…