RC Chalamila: Dar ni washamba tu hapa Mbeya tunafanya kazi na kupiga bia kila siku hatusubiri kufunguliwa Jumapili

RC Chalamila: Dar ni washamba tu hapa Mbeya tunafanya kazi na kupiga bia kila siku hatusubiri kufunguliwa Jumapili

Hawa wakuu wa mikoa wa Mbeya na Dar es Salaam si ndio Bashiru alisemaa anaanza nao warudi shule
Na huyo jamaa wa Mbeya alivyoambiwa hivyo na Bashiru akaenda pale NDC(National Defence College) kuongeza maujuzi,lkn naona bado hakijaeleweka.
 
Hahaha nimwcheka sana asisee huyu RC alinichekesha pale alipoanza kuwanyuka madogo bakora shule na left yake na ninachokiona hapa ndio kinazidi kunichekesha
 
Kila siku naota ndoto mbaya, leo nimeota kuwa Mobutu Sese Seko Kuku wa pili anakuja kuitawala nchi fulani ya Afrika mashariki!
 
Duh huyu Mhehe naye bwana Sijui maneno haya amefundishwa na Nani!?
 
Hayati baba wa Taifa Mwalimu Nyerere wakati wa uongozi wake, hakuna kiongozi wa Kisiasa ambaye alikuwa anapewa madaraka bila kupitia chuo cha Kivukoni.
Huko walifundishwa jinsi ya kuongea na wanainchi na namna ya kutoa taarifa kwa umma.
Sasa hivi kila kiongozi ana mbinu zake za kuongoza kulingana na alivyozaliwa.
Kuna mambo ambayo kiitifika wakuu wa mikoa na wilaya hawaruhusiwi kuyaongelea lakini utakuta wanapwapwaja kwa ukali na amri.
Kwa mfano tofauti zinapojitokeza na Inchi jirani kutokana na ugonjwa wa corona, mkuu wa wilaya au mkoa haruhusiwi kulisemea hili. Wanaohusika hapa ni Mabalozi, Waziri wa Mambo ya nje na Rais wa INCHI baada ya kushauriana.
Tumeona wakuu wa mikoa wakitoa matamshi yanayohusiana na Inchi jirani ambayo ni hatari kitaifa kwa sababu wanatoa tuhuma na kuzilaumu Inchi jirani wakati wao si wasemaji wa mambo ya Inchi za nje.
 
Back
Top Bottom