Hayati baba wa Taifa Mwalimu Nyerere wakati wa uongozi wake, hakuna kiongozi wa Kisiasa ambaye alikuwa anapewa madaraka bila kupitia chuo cha Kivukoni.
Huko walifundishwa jinsi ya kuongea na wanainchi na namna ya kutoa taarifa kwa umma.
Sasa hivi kila kiongozi ana mbinu zake za kuongoza kulingana na alivyozaliwa.
Kuna mambo ambayo kiitifika wakuu wa mikoa na wilaya hawaruhusiwi kuyaongelea lakini utakuta wanapwapwaja kwa ukali na amri.
Kwa mfano tofauti zinapojitokeza na Inchi jirani kutokana na ugonjwa wa corona, mkuu wa wilaya au mkoa haruhusiwi kulisemea hili. Wanaohusika hapa ni Mabalozi, Waziri wa Mambo ya nje na Rais wa INCHI baada ya kushauriana.
Tumeona wakuu wa mikoa wakitoa matamshi yanayohusiana na Inchi jirani ambayo ni hatari kitaifa kwa sababu wanatoa tuhuma na kuzilaumu Inchi jirani wakati wao si wasemaji wa mambo ya Inchi za nje.