RC Chalamila: Kujifanya wanasheria pamoja na kupenda kiingereza kunakwamisha maendeleo ya mkoa wa Kagera

Nakumbuka yule mkuu wa wilaya somebody kinawiro yule aliyetoka.alizuia kabisa manispaa ya bukoba isihamishe stendi pale ilipo ( yaan iendelee ile ya matope) kupeleka kule kyakairabwa ambako walishaanza hata kujikusanya kuweka tiles..
Kisa ikiamishiwa kyakairabwa chadema watapata credit ya kuchaguliwa tena 2020...

Sasa 2020 ccm walishinda kwa nguvu lakin hadi leo 2022 hakuna ujenzi wowote...

It seems ccm wanapenda watu wa kagera wasipate maendeleo..
 
Hivi ukijengwa stand ndio maedeleo tayari??, ungezungumzia viwanda, vyuo vikuu hapo ningekuelewa.
Kinachotakiwa ni kuitisha development forum
na kualika wataalm wakafanya mawasilisho ya changzmoto na fursa zilizopo,na kuibua mjadala wenye lengo la kuweka mipango ya maendekeo endelevu kwa maslahi mapana ya mko wa Kagera.
 
Kagera iko mpakani mwa Uganda, Rwanda, Burundi lakini watu wa kagera kwaufupi wamelala sana wavivu
Kilichokuwa kinaleta maendeleo Kagera ni "nyarubanja", tangu nyarubanja ife na maendeleo yaliondoka. Hao walangira walipenda saana kuwatumikisha Wahangaza, Warundi, Wanyambo, na Wanyarwanda. Ni kama vile Wanyakyusa walivyokuwa wakifanikiwa kwenye kilimo kwa kuwatumikisha Wasafa na Wakinga. Baada ya huduma za hayo makabila kuondoka ukawa ndiyo mwisho wa kukua kwa maendeleo kwa kasi kwa Wanyakusa. Wahaya nao "fate" yao ni hiyohiyo, Kingereza kinngi huku majanga kwenye kazi.
 
Siyo kweli kazi za manamba wamezipita. Asili mia 90 ya watanzania wa makabila yote kazi za manamba hawajazipita, na hii ni pamoja na Wahaya. Kisomo na kusoma kunakoongelewa mpaka leo ambapo tunadai Wahaya/Wachagga wamesoma hizo ni takwimu wakati tunapata uhuru. Sasa hivi mikoa inakaribia kuwa sawa, na hata huko BK siyo kila mtu amesoma. Zaidi ya asili mia 80 ya Wahaya hawajasoma kama ilivyo kwenye makabila mengine. Wahaya walidekezwa na huduma za sawa na bure za Warundi, Wahangaza, Wanyambo. Huduma hizi zilipopotea, maendeleo yalisimama. Labda warudishiwe "nyarubanja".
 
Alianza Nyerere kupeleka washenzi mkoa wa Kagera ili kukwamisha maendeleo ya mkoa, hiyo tabia haijawahi kuisha leo tunatafuta mchawi kwa maneno ya shombo.

Eti mara hii Wahaya leo wamekuwa laughing stock ya nchi!!
Jamani mbona mnamuonea Nyerere, wakati technocrats wengi wakati wa Nyerere walikuwa Wahaya?. Mchawi wa maendeleo ni ninyi wenyewe (Wahaya). Mnaukumbuka mvutano wa viongozi wenu kuhusu ujenzi wa soko? Kagasheki, et al, waligombana vikali kuhusu ujenzi wa soko na sjui iliishia wapi.
 
Hizo takwimi za 80% ya wahaya kutosoma umezitoa wap?
 
Kagera iko mpakani mwa Uganda, Rwanda, Burundi lakini watu wa kagera kwaufupi wamelala sana wavivu

Sijawahi kuona mpakani watu wanalala maajabu haya

Kufungua biashara na kufanya kazi 24/7 ndio duniani wanashindana hivyo ingawa miaka ya nyuma sana hata wazungu walikuwa wanafungua maduka siku 4 tu kwa wiki ila Wahindi wakawafundisha namna ya kufanya kazi walipoona muda mchache tu wameisha nunua nyumba na wanatembelea Benz

Sasa ndugu zetu hapo masifa kibao ila maendeleo zero

Acha wapewe ukweli
 
Ushirika hasa wa zao la kahawa umewainua saana Wahaya. Kumbuka ushirika na makanisa ndiyo ulihangia saana kusomesha Wahaya. Shule binafsi pamoja na kugharimia karo kuliwafanya Wahaya wengi kupata elmu. Kama ni ushirika kufa mjilaumu wenyewe Wahaya. Ushirika uliendeswa loally kila sehemu. Kama mliuua ushirika mjilaumu wenyewe.
 
Hizo takwimi za 80% ya wahaya kutosoma umezitoa wap?
Labda ningeongeza kwa kusema ninamaanishha kuhitimu chuo. Maana elimu yenye manufaa TZ inaanzia kuhitimu chuo, kumbuka hayo ni makadirio ya nchi nzima, tena huenda yako juu.
 
Inyi nshomile fomu foo na ngambo tukakwenda .......
Ndiyo hayo sasa Chalamila hayataki
 
Binafsi nimemwelewa..kamaanisha mbwembwe nyingi na hawatak kuamka kiakili wanajikuta wako mbele by far ..wala sio kejeli ni kweli
 
Ndo haya anayosemea Rc ...umeanza kupinga na huku bk panajulikana ...acha kufananisha hiyo mikoa na bk mkuu
 
Una uandishi murua
 
Kwa hiyo kujua kingereza kunazui Bukoba kujengwa stendi ya kisasa...

Stendi za dom, dar, nk zimejengwa kwa sababu watu wake hawajui kingereza...


CCM haipendi wasomi na watu wa kureason Ndo maana inapata shida sana kagera
Dah kweli kabisa hapo.....yaani Kagera kwa sababu wanaongea sana viingereza ndo maana stendi kuu ya mabasi ni mbovu Ila ya Dodoma ni nzuri kwa kuwa wanaongea kiswahili.

Sasa sijui lugha ina mahusiano gani na maendeleo ya mkoa husika. Yaani kweli tunaongozwa na vilaza wasiofikiria vya kuongea wao kwuta kuropoka.
 
Acha ubishi wee Nshomile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…