RC Chalamila: Tunaweza kuwa na ‘Magufuli Ruling Party’ na mambo yakaenda vizuri kabisa

RC Chalamila: Tunaweza kuwa na ‘Magufuli Ruling Party’ na mambo yakaenda vizuri kabisa

Lisemwalo lipo na kama halipo basi laja. Nadhani huu ni mkakati uliopangwa vyema tu kwamba; Hebu ropokeni kila mahali; Bungeni yupo Kibajaji &Co, nje yupo Ng'wanri na Chalamila & Co. Huku mtu akikataa kataa kumbe anaimezea mate hiyo siku ije mtakapokosea muandike katiba mpya kuwa; Tuwe na chama kipya kimoja tu MRP ambacho kitaua vyama vingine vyote hadi ccm ili kuonesha kuwa; Hatuna upendeleo. Nawasilisha
 
Wee, kwanza alimwambia aache vitamaatamaa va hovyo, pili akamwambia hakubaliani na mawazo potofu ya kuunda chama cha kiukoo cha makufuli ruling party, tatu atamtumbua, au atatengua uteuzi wake kwasababu kamvunjia heshima sana.

Ile ni zuga tu ili isiwe wazi sana. Hayo Magufuli anayogomea jukwaani anayafanya kwa vitendo. Box la kura haliheshimiwi kabisa kwenye hii awamu yake.
 
Mzee mkapa aliwai kukataza huu umimi hawakusikia?
 
Kwa sugu amegonga mwamba. Kwenye malumbano ya hoja alikuwa anajib juu juu tu. Huyu anajiona bado ni kada wkt ameshateuliwa kuwa mkuu wa mkoa. Awaze kama RC. Hawaon ma RC wenzie walivyo.. yeye kutwa akili mpeperuko
Mkuu kongole kwa neno "akili mpeperuko".
 
Rais John Magufuli amesema anatamani kuendelea kuwepo kwa vyama vingi vya upinzani ili kuongeza ushindani, huku CCM ikiendelee kupata ushindi

Kauli hiyo ya Rais Magufuli ilitofautiana na Mkuu wake wa Mbeya, Albert Chalamila aliyetaka kibaki chama kimoja tu.

"Tunaweza kuwa na ‘Magufuli Ruling Party’ na mambo yakaenda vizuri kabisa," alisema RC Chalamila.

Leo katika ziara yake mkoani Mbeya Rais Magufuli ataweka jiwe la Msingi la ujenzi wa nyumba za walimu, mabwenu na maabara katika Chuo cha Ualimu Mpuguso na kuzungumza na wananchi wa Tukuyu.
 
RC kama huyu utawala ukishapita unaweza kukutana nae ukadondosha chozi wanatiaga huruma sana
 
Aliysemewa na RC alikuwepo pale pale juzi jukwaani wakati yanasemwa,hakuona haja ya kukanusha na alifurahia na vigelegele vikapigwa!!!

List ikawa imeongezeka ya wapiga zumari,ndani ya bunge ni Juma Nkamia na Lusinde Kibajaji,mwenye ziara za raisi RC Charamila,nafikiri mwenyewe kajitokeza kuchezesha kekundu ili ionekane sio lengo lake kupusa atakavyo!!!

Awamu ya V-WONDERS!!!
 
Nadhani Msajili wa Vyama vya Siasa atafanya haraka kutueleza chama hiki kitapata usajili wa kudumu lini maana inaonekana kina usajili wa muda kapok use tayari kinaongoza serikali tangu 2015.
Chakamila ametusaidia kujua kwa nini hakukua na nembo ya Ccm yenye jembe na nyundo, kwenye mabango ya kampeni ya chama hicho bali nembo ya "MAGUFULI" yenye "MWENGE" uliochanua. Katika kampeni hizo hakukuwa na maneno yaliyozoeleka ya chagua Ccm, bali Chagua MAGUFULI(Na hapa ndo Chalamila ametufumbua macho kumbe walimaanisha Magufuli Rulling Party). Hata baada ya uchaguzi tulisikia Rais akijinasibu "Serikali ya Magufuli" (Ruling Party) hadi alipofanya kikao na viongozi waandamizi wastaafu na Mkapa akakosoa slogan hiyo. Hata hivyo hilo limeshimdikana kwa Mwenyekiti wa chama kipya, kwani siku hizi akibadilisha anasema "Serikali ninayoiongoza mimi"(Magufuli Government).
Hatuwezi kulaumu kwa kila kitu maana hata vitabu vya dini vinasema shukruni kwa kila jambo. HATA KWA HILI ASANTE RC CHALAMILA KWA KUTUFUMBUA MACHO.
 
Ni kama kuna mkataba na anayetukirimia uhai huku ni kupofuka na kukosa chembe cha hofu ya Mungu
 
Utakaporuhusu kuwepo kwa Magufuli Ruling Party yawezekana kabisa hata ndani ya CCM vikazaliwa vyama vidogo vidogo vingi kwa mfano Nape......party na Bashe......party.

Lakini pia hata kule upinzani tutakuwa na Mbatia Opposition Party, Mrema Opposition Party, mzee Rungwe Opposition Party nk.

Jamani wana CCM wenzangu huwa tunafikiria kweli kabla ya kuongea yaani tunataka kurudi kule Nyerere alikotutoa?!

Ngachoka kabisa
Maendeleo hayana vyama!
 
Salaam waungwana [emoji1538]

Sijaupeleka huu uzi jukwaa la siasa sababu sidhani kama kule ni mahala pa uzi huu.

Uzi wangu unabebwa na swali kama linavyosomeka kwenye heading

Hivi aliposema Magufuli Ruling Part alimaanisha!?
 
Jamaa anakosa hata heshima kwa wananchi kwa Lugha yake mbovu
 
Back
Top Bottom