RC Chalamila: Wanaume wengi wa Mkoani Mbeya wanapenda kulelewa

RC Chalamila: Wanaume wengi wa Mkoani Mbeya wanapenda kulelewa

Wanaume wamechakarika miaka mingi sana ili kuweka miundombinu na mazingira rafiki, kwa sasa muda mwingi wanapose kuhifadhi nguvu zao, haya wanawake pambaneni..
 
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, amesema kuwa asilimia kubwa ya wanawake wa mkoa wa Mbeya, wameachiwa jukumu la kuendesha familia zao huku wanaume wakiongoza kufanya vitendo vya dhuluma dhidi ya mali zinazotafutwa na wake zao.

Chalamila ameyasema hayo wakati akifunga kongamano la sita la jinsia ngazi ya wilaya, ambalo limefanyika katika Halmashauri ya wilaya ya Mbeya.

RC Chalamila amesema kuwa wanawake wengi mkoani humo, ndiyo wanaobeba majukumu ya kutunza na kulea familia, ambapo hufanya shughuli mbalimbali za ujasiriamali ikiwemo kuuza mboga na matunda, wakati wanaume wakitumia mwanya huo kuwafanyia vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kunyang'anya fedha wanazopata kwenye biashara na kwenda kuhonga michepuko.

"Idadi kubwa ya wanaume mkoani Mbeya, wanapenda kulelewa hawapendi kujishughulisha, wanawategemea wanawake kulisha familia na kufanya kila kitu, mbaya zaidi huwashinikiza wake zao kuomba mkopo kwa kutumia account zao ili wadhulumu hizo hela, nawaambia wanawake msikubali kutumika kama ndoa yako ina shida ondoka kaanzishe maisha mengine", amesema RC Chalamila.

EATV
Pale unapopewa speech uongee afu huna cha kuongea
 
Bashiru alisema Chalamila na Makonda waendebwakasome maasili.

JAMAA NI MZIGO, KUTWA KULOPOKA LOPOKA.

ANAWACHEZEA WATU WA MBEYA????
Huyu atakuja kuwa Kama Makonda part 2. Anapenda sana misifa ya kijinga na kuropoka ovyo ovyo!

Let wait and see! Just a matter of time!
 
yeye mbona analelewa na mwanaume mwenzake, Magufuri anamlea sana huyo kijana, huyo kijana aache kujidhalilisha akumbuke ni kheri mume anayelelewa na mkewe kuliko yeye anayelelewa na Dr Magu (mwanaume mwenzake). Mbeya wote watafutaji..ukiona mzee hajishuhulishi wamepokezana majukumu kwa muda..aache kiherehere atuachie mbeya yetu arudi iringa kwao. Wanawake wa Mbeya pigeni kazi acheni kusikiliza maneno ya kwenye kanga na maneno ya kitaarabu taraabu
 
Mjibu kwa hoja si kumlalamikia RC ,anapata hizo kesi ndiyo maana anasema hivyo, wanaume wengi wa Mbeya twambie mnatunza familia zenu? Si kumpandishia RC, wamama wengi wa huko hujitegemea mahitaji yao!
 
Nafasi za uongozi za kuteuliwa (na sasa za ubunge,udiwani na urais) ni kulelewa kama kulelewa kwingine.
Yeye kwa kuwa ni "me" aliyepo Mbeya,basi naye ni wa kulelewa.
Huyu dogo asitake tutoe mambo yake ya kulelewa kule Moro enzi hizo,tena na mama muuza ndizi.
[emoji23][emoji23][emoji23] kumbe mnajuana eee, yeye alisha acha kulelewa sasa anawambia wenzie waache kulelewa
 
Hili jambo ni taboo kusemwa, ingawa halina shaka ndani yake. Tembelea shughuli nyingi za uzalishaji mali muda wa kazi ujionee ni wakina nani wapo busy na shughuli.

Halafu nenda kwenye vilabu na vikao vya mitaani ujione wazee wakazi wakifanya yao. Halafu time ya mlo, wao ndio wa kwanza mezani. Na wanadai ugali nyama, na sio mchicha wala mnafu.
Halafu watu wanamsema RC wakati ni kweli, halafu ni walevi hao?
 
wanaume wa Mbeya mbona mnacheka cheka na huyu . Wakina Mwasakafyuka, Mwambipile, Mwasomola kweli mnalelewa nyie?😂😂😂😂😂
 
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, amesema kuwa asilimia kubwa ya wanawake wa mkoa wa Mbeya, wameachiwa jukumu la kuendesha familia zao huku wanaume wakiongoza kufanya vitendo vya dhuluma dhidi ya mali zinazotafutwa na wake zao.

Chalamila ameyasema hayo wakati akifunga kongamano la sita la jinsia ngazi ya wilaya, ambalo limefanyika katika Halmashauri ya wilaya ya Mbeya.

RC Chalamila amesema kuwa wanawake wengi mkoani humo, ndiyo wanaobeba majukumu ya kutunza na kulea familia, ambapo hufanya shughuli mbalimbali za ujasiriamali ikiwemo kuuza mboga na matunda, wakati wanaume wakitumia mwanya huo kuwafanyia vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kunyang'anya fedha wanazopata kwenye biashara na kwenda kuhonga michepuko.

"Idadi kubwa ya wanaume mkoani Mbeya, wanapenda kulelewa hawapendi kujishughulisha, wanawategemea wanawake kulisha familia na kufanya kila kitu, mbaya zaidi huwashinikiza wake zao kuomba mkopo kwa kutumia account zao ili wadhulumu hizo hela, nawaambia wanawake msikubali kutumika kama ndoa yako ina shida ondoka kaanzishe maisha mengine", amesema RC Chalamila.

EATV
Si kweli
 
Ndio maana wamemchagua mwanamke kuwa mbunge kwasababu wanapenda kulelewa mmetuaibisha watu wa Mbeya
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwa hiyo huko vibenten nikama kawaida?
 
Back
Top Bottom