RC Hapi: Jumamosi ya pili ya kila Mwezi itakuwa ni siku ya kufanya mazoezi watumishi wa umma na Wananchi wote mkoa wa Iringa

RC Hapi: Jumamosi ya pili ya kila Mwezi itakuwa ni siku ya kufanya mazoezi watumishi wa umma na Wananchi wote mkoa wa Iringa

Mkuu wa mkoa wa Iringa Salum Happi amesema jopo la madaktari wa mkoa wa Iringa wamemweleza kuwa mkoa huo unanyemelewa na magonjwa nyemelezi kama kisukari nk.

Kufuatia hali hiyo RC Happi amewaagiza Wakuu wa wilaya mkoani humo kuhakikisha kila Jumamosi ya pili ya kila mwezi inakuwa ni siku ya mazoezi ya Umma ambapo watumishi wote na wananchi kwa ujumla watapaswa kufanya mazoezi.
Watakaopuuza hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Source Channel ten

Maendeleo hayana vyama!
Imeshafeli kabla hata haijaanza
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 kidikteta UCHWARA kingine na hili litafeli tu. Eti hatua za kisheria zitachukuliwa 🤣🤣🤣🤣🤣🤣atawafukuza kazi au kuwaweka rumande? MPUUZI kweli huyu!

Kufanya mazoezi kwa lazima hakuwezi kuwa na manufaa kwa Afya za wahusika!! Wafanyakazi wapewe elimu ya umuhimu wa mazoezi ili kila mmoja afanye mazoezi yanayomfaa yeye kufuatana na umri wake; pia afanye mazoezi kufuatana na wakati unaomfaa!!!
Hivi vidikteta uchwara vinaiga mambo bila kufanya utafiti; sio kila mazoezi ni sahihi kwa kila mtu!! Mazoezi yanategemea umri na pia jinsia ya muhusika; kuna mazoezi mengine hayafai kufanywa na wanawake na wazee!!!
 
Na hapa ndio unaona viongozi wasio na akili. Kwanza jumamosi ni Sabato takatifu kwa tunao amini hivyo.
Pili hivi mtu anashamba, jumamosi saa kumi na mbili asubuhi kawahi shambani kwake kwa kupamis siku za kazi. Hii si zaidi ya zoezi? Wao wanafikiri watumishi wote tumebweteka kama wao. Nina kuku, mahindi, na mbogamboga nikakimbie wanjani kutafuta mini?
Hahahaaaa..........!
 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Salum Happi amesema jopo la madaktari wa mkoa wa Iringa wamemweleza kuwa mkoa huo unanyemelewa na magonjwa nyemelezi kama kisukari nk.

Kufuatia hali hiyo RC Happi amewaagiza Wakuu wa wilaya mkoani humo kuhakikisha kila Jumamosi ya pili ya kila mwezi inakuwa ni siku ya mazoezi ya Umma ambapo watumishi wote na wananchi kwa ujumla watapaswa kufanya mazoezi.
Watakaopuuza hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Source Channel ten

Maendeleo hayana vyama!
Aiseee....hahahaha
 
Dsm chupu chupu watiwe vidole kupimwa tezi dume, washukuriwe mashujaa wa kigamboni
Hilo la jamaa kupigwa huko kigamboni nililidaka mapema Sana sema nilikuwa nasubiri kuconfirm tu.

Ile ndio ilikua safari yake.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] kidikteta UCHWARA kingine na hili litafeli tu. Eti hatua za kisheria zitachukuliwa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]atawafukuza kazi au kuwaweka rumande? MPUUZI kweli huyu!
Hakuna SHERIA wala KANUNI yoyote ndani ya JMT inayoweza kumuwajibisha mtumishi wa umma ambaye hatatekeleza agizo hili.

Ni kweli ukilitazama hili tamko kwa jicho la pili linaweza kum-describe Happi kama dictator, lakini mimi binafsi nawiwa kumuita BENEVOLENT DICTATOR; huyu ni yule dictator anayetoa amri kali lakini kwa MANUFAA ya wanaopewa amri hiyo, kwa mfano Rais akilazimisha kila mwananchi apatiwe chanjo ili kujikinga na ugonjwa flani.

All in all, mazoezi ni jambo jema, ila RC alitakiwa kushauri tu na wala siyo kutoa agizo la namna hii.

Nawasilisha.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom