RC Kafulila awanyoosha wachina wa CHICCO, ni wale waliotaka kutupiga TZS 15BL kwenye ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa kilometa 57 kwa TZS 75BL

RC Kafulila awanyoosha wachina wa CHICCO, ni wale waliotaka kutupiga TZS 15BL kwenye ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa kilometa 57 kwa TZS 75BL

Sheria za China zinaruhusu Rushwa ukiwa nje ya China kama rushwa hio ni kwa manufaa ya nchi yao, yaani kuziibia nchi zingine
 
Wachina wamefunga ndoa za ufisadi na watawala wa kiafrica
Bila kutawanya mamkaka ya dola kwa wengi Africa itabakia kwenye giza nene la Ufisadi. Nchi nzima eti HAZINA ni moja na anayeamua hela zitumikaje ni MTU MMOJA.... kichekesho.... Anayeteua watu wote kwenye dola ni MTU MMOJA...kichekesho
 
CHADEMA mmefurahi Sana kisa aliwatoroka 😂😂
Sema TAIFA..... dawa na vijana Mi-CHAWA huwa ndiyo hii... alifikiri Mafuguli ataishi milele - hela aliyopewa ishaisha sasa hivi ni msoto tu.

Akatafute shule ya Secondary ya kufundishe kule kwao Uvinza vinginevyo maji yatakuwa mma
 
Mkurugenzi wa TANROADS alikuwa wapi

Waziri wa ujenzi naye alikuwa wapi

Team ya ufundi ya TANROADS inafanya nini mpaka RC abaini makosa yote hayo tena ya kitaalamu
Unadhani nn apo Zaid ya rushwa ushasikia mkuuu wa mkoa Mpya na iyo mikataba Yote imesainiwa na mkuuu wa mkoa wa zaman wameshindwa kuelewana kupeana mgao na mkuuu wa mkoa wa zaman kwaiyo kaamua kulipua bovu hii nchi DAh 😪#kaziiendeleee
 
Sema TAIFA..... dawa na vijana Mi-CHAWA huwa ndiyo hii... alifikiri Mafuguli ataishi milele - hela aliyopewa ishaisha sasa hivi ni msoto tu.

Akatafute shule ya Secondary ya kufundishe kule kwao Uvinza vinginevyo maji yatakuwa mma
Daaah,
 
View attachment 2290873


Kampuni ya kichina ya CHICCO yatekeleza agizo la RC Kafulila, tayari imekamilisha marudio ya barabara yenye urefu wa kilometa 10 zenye thamani ya tzs15bl.

==
Kampuni ya Kichina ya CHICCO inayotekeleza ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi - Maswa yenye urefu wa kilomita57, ilianza ujenzi tangu mwaka 2018 kwa thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania billion 75. Wachina hawa walikwaa kisiki baada ya kutakiwa kurudia ujenzi wa vipande vya barabara vinavyofikia kilometa 10 kutokana na kujenga chini ya kiwango kilichowekwa.

Agizo hilo la kutakiwa kurudia ujenzi lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe David Kafulila Juni 5, 2021 ikiwa ni wiki moja tu baada ya kuripoti mkoani Simiyu kama Mkuu wa Mkoa mpya. Leo ikiwa ni mwaka mmoja sasa tangu agizo hilo, RC Kafulila akihojiwa na kituo cha EATV amekiri kuridhishwa na kazi iliyofanywa na kwamba ujenzi upo zaidi ya asilimia 96% kwa viwango vinavyokubalika.

"Nakumbuka ilikuwa ni wiki ya kwanza baada ya kuripoti kama RC, hii barabara niliona wakati nakuja kuripoti Simiyu. Nilifanya ziara na Bodi ya Barabara na kuelekeza marudio ya barabara na kumwelekeza mkandarasi kurudia. Nilimsisitiza barabara yake haitapokewa na Mhe. Rais ikiwa chini ya kiwango" alisema Kafulila na kuongeza kuwa, "mbali ya kurudia barabara, pia mshauri mwelekezi(consultant) alibadilishwa. Sasa watu wote wakipita wanafurahi kuona serikali sasa itapokea barabara imara sawa na thamani ya fedha zao wanazozitoa kupitia kodi na tozo mbalimbali."

"Huu ni ujumbe wangu kwa wakandarasi wote mkoani Simiyu, hakuna mradi utakaopokelewa ukiwa chini ya kiwango. Kwasasa nina amani hata Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan akipita kukagua nina amani kwamba fedha iliyoletwa ndani ya mkoa wetu kwajili ya barabara na hata miradi mingine, thamani ya pesa(value for money) inaonekana. Wakandarasi wababaishaji hawana nafasi, nimeshavunja na nitaendelea kuvunja mikataba na kila mbabaishaji aliyepata mradi kwa bahati mbaya Simiyu," alisisitiza zaidi.

"Serikali inalaza mabilioni ya fedha barabaran ndio maana lazma kuhakikisha tunabanana. Yaani gharama kilomita 1 ya lami ni takribani 1.5 bn., pesa ambazo zinatosha kukamilisha majengo ya kituo cha afya. Sasa upewe mabilioni yote hayo na bado ukabidhi barabara ambayo baada ya mwaka tu imeharibika na kuhitaji mabilioni mengine ya ukarabati? Huu ni ushenzi ambao hauwezi kupewa nafasi ndani ya awamu ya sita, na kwa upande wetu tutatimiza kipande chetu Simiyu, " alimalizia.

#SISITUKO TAYARI KUHESABIWA TAREHE 23/08/2022,WEWE JEE?!

Daah, hivi huyu jamaa alikosea wapi aise mbona kama hili Taifa linahitaji viongozi wa aina wa kumtetea Rais, Chama na then Serikali.
 
Back
Top Bottom