Mwanahabari wa Taifa
JF-Expert Member
- May 27, 2020
- 1,588
- 956
RAIS SAMIA ANAVYOIVUTIA KASI VIETNAM, KOREA KIMAENDELEO,
Mhe Mkuu wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila anasema,
Ujenzi wa Chuo cha VETA Simiyu ni moja kati ya vyuo 25 anavyojenga Mhe Rais Samia Suluhu Hassan, nchi nzima kuanzia mwaka jana,
Mhe Rais anatujengea jumla ya majengo 25 na sasa tupo zaidi ya asilimia 85 kuyakamilisha,
Uamuzi huu wa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kuwekeza zaidi katika ujenzi vyuo vya kati ni sehemu ya siri ya mafanikio ya mataifa kama Vietnam na Korea kusini,
Kwa msiofahamu mataifa haya tulikuwa nayo sambamba kiuchumi mpaka miaka ya 1990's
Chaajabu Mataifa haya leo yametupita zaidi ya mara tano,
Vyuo hivi vinajenga nguvu kazi kubwa yenye maarifa ya kuzalisha na hivyo kujenga uchumi mkubwa na jumuishi kwa kila mwenye nguvu ya kufanya kazi kuwa na maarifa ya kuzalisha.
Hivyo tunamshukuru Sana Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa fikra za kimapinduzi katika kuhakikisha vijana wengi wanapata fursa ya kupata maarifa na kujenga nchi yao kwa kuzalisha ajira na kujiajiri,
Leo kuna miradi mingi ya ujenzi kila kona ya nchi na yote inahitaji mafundi wa aina mbalimbali.
Hapa Simiyu tunaishiwa vijana wenye stadi za ufundi mpaka tunaenda kuchukua Vijana Mwanza.
Chuo hiki kitajenga vijana wengi wa kutumia fursa hizi alimaliza kwa kusema Mhe RC Kafulila alipokuwa kwenye ukaguzi wa ujenzi wa chuo cha VETA-SIMIYU