RC Kafulila: Rais Samia anatupitisha njia ile ile ya Korea na Vietnam, tulikuwa nao sambamba kiuchumi miaka ya 1990's walituacha sasa tunawashika

Huko mkoani Tanga wafugaji na wakulima wamepigana usiku kucha huku kasimu majaliwa akipokea pesa kutoka oBC
 
Haha Kafulila anahangaika sana kama anataka kutaga vile.

Kwani ukuu wa mkoa haumtoshi??

Au anataka ateuliwe ubunge na kupewa uwaziri?
Kwa hiyo akienda kukagua miradi inayotekelezwa ndani ya mkoa wake anyamaze asi comment chochote? Acha ujinga mbona rais nae anaongea anapokagua miradi vipi anataka kuteuliwa na nani?
 
Kwa hiyo akienda kukagua miradi inayotekelezwa ndani ya mkoa wake anyamaze asi comment chochote? Acha ujinga mbona rais nae anaongea anapokagua miradi vipi anataka kuteuliwa na nani?
Vijana wa chadema wako choka mbaya kwa hoja, Wivu na ghubu vinawapa tabu sana
 
Kusema ukweli waAfrika tutaendelea kuwa kichwa cha wenda wazima.
Kwa Nini nasema hivi.
Utakuta viongozi badala ya kufanya Yale yanayowahusu Kwa mustakabali wa nchi na watu wake.
Mtu anaibuka kumsifia Rais wake Kwa yanayoenda. Pesa zitoke Kwa wafadhili hata kama mkopo, wananchi wanalipa Kodi
Lukuki na Tozo nyingi.
Yeye na wizara Fedha husika ni kupanga cha kuifanyia huku wakimega saizi yao pia.

Sasa nauliza hizo sifa Lukuki zanini? Mbona nchi za wenzetu hawana kumsifia Rais na wanatekekeza majukumu yao Kwa asilimia [emoji817] na kama ukishindwa kuwajibika unachia ngazi! Ndio maana KATIBA MPYA muhimu na wateuliwa wawe wanaomba na kusailiwa kazi.
Hii ya kuteuwa Leo kuapisha kesho ife viongozi wanabweteka na kuanza Misifa.
 
Mbona nimeisikiliza vizuri hii clip RCKafulila kamtaja Rais mara moja tu
 
Maendeleo yanaletwa na vitendo na wala siyo maneno.
Watendaji wa maendeleo ni wananchi na serikali huwezesha kwa kuweka sera na sheria wezeshi.
Ufafanuzi wa sera na sheria zenye kumsaidia mwananchi mmoja mmoja unatakiwa kutofautisha hali ya zamani na sasa.
 
Binafsi nafarijika Sana na kasi ya kimaendeleo inayofanywa na Rais,

Jambo la msingi ni watu kuwa na Uzalendo kwa pesa za Umma,

Pesa anazotoa Mama zikitafunwa hatutaona matokeo,

#VIVA SAMIA VIVA
😍😍Mama hakamatiki aise
 
Kwenye hili nakuunga mkono 😍😍
 
Kwa hiyo akienda kukagua miradi inayotekelezwa ndani ya mkoa wake anyamaze asi comment chochote? Acha ujinga mbona rais nae anaongea anapokagua miradi vipi anataka kuteuliwa na nani?
Afanye kazi sio kujisifia mitandaoni kwa ujinga ujinga kama huu unaofanya hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…