RC Kunenge: Kariakoo ilikuwa kama Dubai, tujitahidi kuirejesha tuwavutie Wacongo na Wamalawi

RC Kunenge: Kariakoo ilikuwa kama Dubai, tujitahidi kuirejesha tuwavutie Wacongo na Wamalawi

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mh Kunenge amesema Dar es salaam ilikuwa kama Dubai ikizihudumia nchi za Afrika mashariki lakini haijulikani kitu gani kimeirudisha nyuma.

Kunenge amewataka watendaji wa jiji la Dar es salaam kuhakikisha Kariakoo inarejea kuwa Dubai ya Afrika mashariki kama ilivyokuwa enzi zile.

Chanzo: ITV

Maendeleo hayana vyama!
Watatue na tatizo la TRA.
Kunenge anaujua ukweli, na asizunguke mbuyu.
Mfanya biashara apipowekewa mazingira ya kulipa kodi kistaarabu hakuna litakalofanyika.
TRA ndio wameua Kariakoo tusitafute mchawi kwingine wakati mchawi tunamfahamu.
 
Inatakiwa ifikie stage kodi iwe haikusanyiki kabisa
Kaka sisi wafugaji wa kuku wa mayai tunajua principal; kuku lazima ale kwa siku gram 125 ya chakula ili na wee upate yai moja!
Sasa mlishe pumba tupu uone kama utapata hilo yai.

Sasa kuna watu hawampi kuku hata hiyo pumba afu eti wanategemea aendelee kutaga...thubutu!!
 
Eeh maana wamekusanya kodi wakamaliza akiba wakarudi kukusanya mitaji wakamaliza sasa wamekuja na mtindo wa fine. Hapo ndipo ambako wengi walifungasha virago 😂😂😂
 
Sio kodi tu kariakoo hawa wafanya biashara walikuwa wanakuja wanabadili pesa zao iwe kwacha iwe dollar masaa 24 kariakoo wanafanya biashara kwa uhuru matokeo kuporwa na kufungwa sehemu na kujenga mazingira magumu ya biashara ni lazima waende Bank na change ya baadhi ya pesa za kwao hazikubaliki ina maana inabidi wabadili mara 2 hapo wanapoteza pesa na urasimu watu hawataki hayo. Kariakoo wasinge pagusa ila wangeweka taratibu slowly kutoa vitambulisho wakati wa kuchange ila wangeachwa wafanye biashara kwa urahisi. Mambo mengi tumeyaharibu wenyewe, wakitoka madukani tu wanasumbuliwa watu wanakimbia. Kariakoo ilitakiwa kuwa free zone.
 
100% +✔️ hiki ndio kiini cha tatizo hongera sana mkuu
 
Kuna sehemu Dubai inaitwa Deira wengi waliofika wanapajuwa. Hii sehemu ndio utawakuta waafrica, wahindi na wengi tu ndio kama kariakoo yetu. Utakuta askari wako lakini hukuti wanamuuliza mtu kitu sio kwamba hawaoni wanawake wanaojiuza hapo wanaona kila kitu na ile nchi unajuwa sheria zake. Ila wanafunga macho muhimu usivunje sheria na wanalinda usalama ila waanacha movement zote free kabisa hawagusi mtu wanalinda mazingira ya biashara. Sasa jiulize kwanini wanafanya vile? wanajuwa hawa wanakuja kununua wanatoka sehemu tofauti bila hawa hakuna Deira ila ukikutwa unafanya ujinga huo sehemu zingine unakamatwa. Kariakoo ilitakiwa tuifanye kama Deira.
 
Back
Top Bottom