RC Kunenge: Kariakoo ilikuwa kama Dubai, tujitahidi kuirejesha tuwavutie Wacongo na Wamalawi

Achana na Kariakoo ya miaka ya nyuma bhana.
 
Hivi lile vurugu la wamachinga kule Kariakoo nani atakwenda..
 
Nani ameiharibu ?
 
Kunenge, naweza mwamini kuliko Makonda. Lakini kama mfanyabiashara akiwa na balance kidogo tu anatakiwa atoe maelezo, hiyo Dubai itarudishwa na hela za kununulia pipi? Imani ya wafanya biashara mchini haitarejeshwa kwa matamshi ya jukwaani pekee.
 
Enzi za J.M Kikwete!Kilichoididimiza Dar ndicho kile kile kinachoumaliza uchumi wa Tanzania.R.C alitakiwa afahamu hilo na amshauri asiyeshaurika.
 
Baada ya miaka mitano ya mateso, hatimaye sasa tunaanza kuimba wimbo mmoja. Hivi wale jamaa waliokuwa wanatoa Takwimu za idadi ya makampuni na biashara zilizoanzishwa kwa kipindi fulani wameenda wapi???
Nilishangaa walipomtumbuwa Waziri mzuri aliyekuwa anajua takwimu za viwanda vipya kila mwezi. Huyu angeendelea 2025 tungekuwa na viwanda 100,000.
 
Watatue na tatizo la TRA.
Kunenge anaujua ukweli, na asizunguke mbuyu.
Mfanya biashara apipowekewa mazingira ya kulipa kodi kistaarabu hakuna litakalofanyika.
TRA ndio wameua Kariakoo tusitafute mchawi kwingine wakati mchawi tunamfahamu.
Mtasema yoteeee!
 
Usitegemee lolote toka kwa watu wanaowaza kinyumenyume. Mtanzania anaishi Malawi miaka 3 anakusanya mtaji mil.100 anaamua kurudi nyumbani, akifika mpakani anapewa kesi ya uhujumu Uchumi na fedha yote inataifishwa, sasa sijui kaujumu uchumi wa nchi gani?
 
Machinga waondolewe mbele ya biashara za wafanyabiashara wengine.Njia ziwe wazi kila mtu atumike inakostahili..
Ndg Alvin nakubaliana na wewe kabisa. Machinga asilimia kubwa wanauwezo wa kulipa kodi na ndiyo wengi wametoa vitu madukani na kuahamishia kwenye umchinga. waliobaki madukani biashara wameshindwa fanya na kusababisha mzunguko mdogo ambao kwao umeleta pia changamoto za kulipa mikopo.Sasa wadau wengi naona wamewaangushia lawama TRA bila kuangalia chanzo hasa ni kipi. kama kodi toka enzi na enzi zilikuwepo na TRA ilikuwepo toke 2006 ikiendelea na jukumu lake la kukusanya mapato ya serikali. Nilichokiona kwa sasa TRA ni kuongeza umakini katika kusimamia sheria na ufatiliaji wa kodi. Zamani tulizoea ona mtu baa anazungusha ofa na hakuwa na wasiwasi wa kulipa sababu pesa alikuwa nayo hivo wamiliki wa mabaa walifaidika sana na wateja kama hawa.Sasa hivi utakuta watu wanakunywa maji hakuna tena zungusha unategemea mwenye baa atapata tena mapato au atafunga biashara maana kuna wahudumu wanadai,umeme maji nk. Sasa hapo napo utasema ni TRA? Ninarafiki yangu yupo kariakoo anasema anaweza kaa siku nzima hata salamu asipate sasa napo sijui ni TRA au? Mkuu wa Mkoa nampongeza kwa kauli yake maana kuna mengi yamechangia tozo,sijui ulinzi shirikishi,taka,Liseni n.k.
 
Hujawahi hata kufanya biashara ya kumbikumbi unajua kupokea tu kww kimya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…