RC Makalla: Kuanzia usiku wa leo hakuna Panya Road atasalimika, operesheni inayoanza si salama kwao

RC Makalla: Kuanzia usiku wa leo hakuna Panya Road atasalimika, operesheni inayoanza si salama kwao

Dar ina watu zaidi ya million 3, watu chini ya 300 wanasumbua vipi? Fursa hii, nna wanangu kama 7 hivi wanaiweza hii kazi, wapewe tu leseni ya kazi maalum alafu the rest mtaona hapo hapo. Vitoto vidogo haviwezi kusumbua watu.
Wanao cha mtoto hiyo tenda wanipe mimi bonge la nyau hao panya wataita maji mma ngoja niishie hapo.
 
Dar ina watu zaidi ya million 3, watu chini ya 300 wanasumbua vipi? Fursa hii, nna wanangu kama 7 hivi wanaiweza hii kazi, wapewe tu leseni ya kazi maalum alafu the rest mtaona hapo hapo. Vitoto vidogo haviwezi kusumbua watu.
Ingekuwaga hivyo kusingekuwaga na hata mwizi wa ndala.
Sheria na vikund vya haki vya binadamu kelele zake si za.kitoto
 
Safi sana ila ingekuwa vyema angesema kuanzia leo Mama, Baba na walezi ambao wanajua watoto wao watukutu na wanatabia za kihalifu wasipowaona watoto wao waende Munchwari na ICU na labda vituo vya Polisi. Wajinga sana hawa Panya Road.
Ikumbuke kauli ya pinda ile ya atakayeua nae auawe ilivyomshukia hadi akalia.
Kunakauli haziwez semwa hadharan
 
Tatizo la sisi Tanzania na vyombo vyetu vya usalama katika operation kama hii anayehusika na asiyehusika wote watakua kitu kimoja,akili na busara inakua asilimia 1
Kikubwa ni ushauri kwa jeshi la polisi
Sio kila mtu atakaekua nje usiku ama wakiongozana wawili watatu basi ni panya road
Busara iwe mbele
 
Kinyume cha hiyo kauli. Wachache watasalimika ila wengi wao hawatorudi.
Kwenye kuokoa kuna wanaopona na kufa, so issue ya watakaorudi ni nafuu warudi na vilema vya kudumu, mfano mtu anarudi akiwa hana pua, masikio na vidole vya miguuni, nyonga imelegezwa kama mlenda!.
 
USA walifanikiwa kuwapunguza gangs kwa njia zifuatazo.
1.Kuwakamata wezi Sugu na kuwapeleka Jeshini kule wanapewa mafunzo ya vita kisha wanapelekwa vitani mstari wa mbele wakamalizwe wakipona SAwa.
2.Kuwasaka maskani yao na kuwaua.
3.Kuwageuza dabo agent yaani kuwaajiri wawe informer wanaenda kwenye tukio kisha wanauza ramani kwa police, wanatengenezwa mazingira ya kutoroka lakini wale wengine wanamalizwa palepale.
Solution.
Serikali iwakamate panya wote wapelekwe kambini wakafundishwe vita kisha wapelekwe nchi za vita wakapambane na waasi, hii pia ni njia nzuri ya kuwamaliza panya.

Tanzania haiwezi kufanya kitu kama hicho. Na haitatokea katika tawala za raisi yeyote yule.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema "Kuanzia leo, baada ya tamko langu leo, usiku wa leo na kuendelea hakuna 'Panya Road' atasalimika katika mkoa wa Dar, oparesheni inayoanza usiku wa leo si salama kwa 'Panya Road', oparesheni inayoanza leo inaenda kuua uti wa mgongo wa mtandao mzima wa 'Panya Road"

Ameongeza "Niwasihi wazazi kwamba operesheni hii haitowaacha watoto wao wahalifu, kama mzazi ulizoea kupata zawadi kwa mtoto, TV bila kujua kipato chake, akudanganye 'amebeti', kawatafuteni watoto wenu kwenye vituo vya Polisi kuanzia kesho"

Amesisitiza "Kila Wilaya kwa mikoa ya Kipolisi, kutoa taarifa za kila siku za Operesheni ondoa 'Panya Road' na kudhibiti uhalifu katika mkoa wa Dar es Salaam kila siku, toeni taarifa tusipotoa taarifa watazitoa taarifa mbaya"

Ameyasema hayo siku moja baada ya kundi hilo la uvamizi kuvamia na kujeruhi watu 19 katika Maenel ya Mtongani, Kunduchi mkoani humo
operesheni kimyakimya ye kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama hakutakiwa kusema wangefanya kama ambush
 
Hii kauli inatia shaka sn..

Katika nchi za kiafrika,ukisikia kiongozi ameongea kauli km hii, kinachofuata hapo ni mateso Kwa wanaohusika na wasiohusika..nguvu unayotumika inakuwa nyingi sn alafu akili kisoda

Wengi waneuawa Kwa staili hii Kwa kisingizio cha neno "tunafanya operation maalum"

Hapa mzazi km Una mtoto wako wa kiume kuanzia 8-21 years,wiki hii mkataze mitoko ya jioni hasa mambo ya mipira ya 'chandimu'..polisi wanasomba wote wanakuwa ktk vikundi vikundi,mtajieleza mkifika kituoni

Naongea Kwa experience kubwa Kwa sababu nimekulia uswahili Temeke,tandika,Sheraton,maputo,relini,buza na viunga vyake..Enzi za Yule Askari mbabe wa kuitwa Tyson,jamaa anawakamata,kisha anawatembeza Kwa miguu na Pingu hawafungi alafu anauliza ambae anajiona ana ubavu wa kupigana na Mimi ajitokeze,akinishinda namruhusu asepe..sijui Yuko wapi Yule jamaa siku hizi

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Watembee na vitambulisho
 
Mawazo ya kipuuzi kbs na mawazo km haya ndy wanakuwa Nayo polisi baadhi wakishapewa kazi ya kuingia mtaani kutafuta wahalifu..

Enzi hizo za wahuni wa Temeke Mimi nimewahi kusombwa polisi kisa tupo kitaani tunacheza draft na polisi wanatafuta vikundi vya kihalifu

Wangekuwa na mawazo km yako wengi tungekufa bila hatia

Km umezaliwa uswahilini wanakotokea hawa panya road,mburahati,kigogo,manzese,tandika nk haiwezi kuepuka kukutwa na majanga ya kihalifu ktk safari ya maisha yako..

Hao watoto wamejikuta Tu wamezaliwa uswahilini,hawakujichagulia wao wenyewe ingawa uhalifu ni Jambo walilolichagua..Polisi wakiingia mtaani wanachojua wanaenda kukamata panya road uswahilini,sasa mara kadhaa inatokea wanakamatwa na wasiohusika..Je,kuua ni solution?? Fikiria tena mkuu!!

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Wewe unataka iweje labda ndugu? Raisi katoa onyo jana Leo wanakata watu mapanga.

Hawa tusiwarembee jina kwa kuwaita eti panya nyoko, hawa ni majambazi na wanafanya wizi wa kutumia siraha. Alafu unataka wabembelezwe?

Mapori yapo mengi tu, nashauri watenge pori la kuwazika huko.
 
Kule Kenya wakati Kibaki (R.I.P.) anaingia Madarakani, alikuta tatizo kubwa la chokoraa , watoto wa mtaani.

wakifanya uhalifu kwenye mitaa ya Nairobi na Viunga vyake, ilikuwa ni tatizo kweli siyo mchezo.
Alikaa na taasisi mbali mbali kuona namna ya kummaliza hilo tatizo,

Vilianzishwa vituo mbali mbali wakakusanywa ,wakapewa elimu ikawaingia ,wengi walikuwa na urahibu wa kuvuta (Gam) yaani chupa ya plastic ndogo inawekwa gundi patex inachanganywa na petrol,walikuwa ni hatari sana ukikutana nao kwenye anga zao.
Baada ya kuwakusanya walipelekwa kwenye vituo vya ufundi vilivyokuwa vimeanzishwa kila mmoja kwa namna alivyopenda awe kama ni fundi Magari, Selemara,Uchomeleaji nk.
Hii kitu ilisaidia sana kupunguza uhalifu kwenye jamii na wengi walipungua mtaani.

Naona na hapa kwetu inahitajika hekima siyo nguvu tu ili kummaliza hili tatizo ,huenda hawa wanafanya hivi sababu ya hali zao kimaisha .

Ndiyo wakamateni wawekwe sehemu waulizwe kwa nini wanafanya uhalifu wa namna hii vijana bado wadogo wanahitaji msaada kwa kweli.

Wasaidiwe zipo taasisi zinazoshughulikia haya mambo , wapelekwe vyuo vya ufundi wapate ujuzi wao wa kuwasaidia ili kuachana na uhalifu wa namna hii.

Lakini suala la kuwaua ,utaua na wengine wasio na hatia, hapa hekima kubwa itumike ni watoto wetu hawa , ni wadogo zetu hawa, ni wajukuu zetu hawa, tunaishi nao mtaani tunawafahamu tuwashauri.

Huenda ni urahibu wa Madawa ya kulevya unapelekea yote haya .
Kama ni watoto wenu mnaishi nao mtaani na mnawajua, mmeshawahi kufanya icho ulichoshauri? Kwann mko kimya? Ninyi ndo mnawatuma wapore na kukata watu mapanga si ndio?

Hao ni wezi kama wezi wengine watajifunza wakiwa gerezani.
 
View attachment 2208639

Yaani mbinu nzuri ingekuwa ile ya kipindi cha Augustino, mzazi au ndugu unapewa taarifa kachukue maiti sehemu fulani au mochuari.

Hiyo ya nenda kituo cha polisi imekaa kama ina upendo fulani hivi!.
Hata ivo amechelewa sana! mpaka nikawa najiuliza ivi kamati ya ulinzi na Usalama mkoa haioni hili tatizo ikiongozwa na RC.

Ilikuwa ni aibu kwa RC kiukweli!? kwanza hakupaswa kusubiri tamko la Mama! wanachi wake wameumizwa sana.

Na sikuona haja ya kutoa taarifa kwa uma, sabab hao vijana watafichwa/Jificha! hiii ilifaa iwe kimya kimya, then badae wanakuja na report ya kazi ilivyofanyika.

Wengi watajificha!
 
Enzi ya Magu kulikuwa na kikosi maalum kilichokuwa kinaingia kazini jioni kuanzia saa 10 mpaka asubuhi. Hao walipewa mamlaka ya kuondoa uhai wa yoyote yule aliyeitwa jambazi au mwizi maarufu. Nafikiri kikosi hiki kirudi kwa "the last dance"
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema "Kuanzia leo, baada ya tamko langu leo, usiku wa leo na kuendelea hakuna 'Panya Road' atasalimika katika mkoa wa Dar, oparesheni inayoanza usiku wa leo si salama kwa 'Panya Road', oparesheni inayoanza leo inaenda kuua uti wa mgongo wa mtandao mzima wa 'Panya Road"

Ameongeza "Niwasihi wazazi kwamba operesheni hii haitowaacha watoto wao wahalifu, kama mzazi ulizoea kupata zawadi kwa mtoto, TV bila kujua kipato chake, akudanganye 'amebeti', kawatafuteni watoto wenu kwenye vituo vya Polisi kuanzia kesho"

Amesisitiza "Kila Wilaya kwa mikoa ya Kipolisi, kutoa taarifa za kila siku za Operesheni ondoa 'Panya Road' na kudhibiti uhalifu katika mkoa wa Dar es Salaam kila siku, toeni taarifa tusipotoa taarifa watazitoa taarifa mbaya"

Ameyasema hayo siku moja baada ya kundi hilo la uvamizi kuvamia na kujeruhi watu 19 katika Maenel ya Mtongani, Kunduchi mkoani humo
Muda huu tunavyoongea wako Tabata wanapiga kazi
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema "Kuanzia leo, baada ya tamko langu leo, usiku wa leo na kuendelea hakuna 'Panya Road' atasalimika katika mkoa wa Dar, oparesheni inayoanza usiku wa leo si salama kwa 'Panya Road', oparesheni inayoanza leo inaenda kuua uti wa mgongo wa mtandao mzima wa 'Panya Road"
Rubbish
Too many unnecessary and meaningless words
Wee RC watu wanataka amani siyo maneno, nguvu na muda unavyotumia jukwaani ungevitumia front line ungeonekana una akili na serious
 
Back
Top Bottom