RC Makalla: Machinga wote Dar walio katika hifadhi ya barabara, Wataondolewa na vibanda vyao kuanzia Septemba 13, 2021

Safi sana! jamaa wamegeuka kero kubwa katikati ya mji hata Mwenge pia! Nimeona hii kwa Le Mutuz!
Wewe unafikiri watauzia wapi kama sio katika katikati ya mji? Wewe upo pale Azam unafanya kazi unafikiri maisha ni rahisi tuu kama ulivyo andika? waende wapi? Makalla akifanikiwa kwenye hili ntakuletea zawadi pala Azam
 
Hii mara ya pili wanatoa hili agizo lakizo inaishia kuwa maneno bila vitendo, ukweli ni kwamba hili Jiji ni chafu kupindukia.
 
 
Safi ondoa hao wachafuzi wa jiji,

Jiji lilikuwa chafu kisa mwendazake anatafuta cheap political gains.
Watembee kwa miguu hadi Chattle, wakamlilie, as protest, potelea pote, Makalla safisha jiji, mifereji izibuliwe, maji taka yasijae mvua haziko mbali.

Mama Rais kaenda Rwanda, Mabeyo akaenda na Sirro nae katokea huko juzi, nafikiri wamepata maujuzi ya kutosha, jinsi ya kuifanya Daslaam ifanane na Kigali.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Wewe unafikiri watauzia wapi kama sio katika katikati ya mji? Wewe upo pale Azam unafanya kazi unafikiri maisha ni rahisi tuu kama ulivyo andika? waende wapi? Makalla akifanikiwa kwenye hili ntakuletea zawadi pala Azam
Acha jazba! Hukua na haja ya "kufoka" 😆namna hiyo relax! Ni utaratibu tu ..zile ni hifadhi za barabara, bila shaka unafahamu kwamba kuna maeneo rasmi ya kufanya shughuli zao, kwanini hawataki huko? Afterall, Mji utakua na kutanuka lini kama tukiendeleza mentality za namna yako?
 

Mpaka fire hydrants wakaziharibu au kuziziba kabisa
Mpaka fire hawazijui zilipo tena
 
Hakuna mwenye uwezo huo.

Hakuna mwenye kuweza kuwatoa wamachinga.

Makala hajawahi fanya jambo likakamilika.

Mkitaka mji uwe safi, Wamurudishe Makonda aje atunishe misuri yake. Wakishindwa huyo lambda Mtaka.

Kuwa ondoa machinga kunahitaji mtu atumie nguvu sana ama mipango mathubuti.

Machinga kama wa pale Mbezi huwezi ukawatoa hivihivi. Ni wengi mno afu hawana pa kwenda. Serikali ijipange. Ila Makala tu hawezi kwa kweli.
 
Narudia tena wewe unalipwa hapo hujui maana ya machinga.... machinga hawawezi kaa mbali ya wateja... wanatakiwa kuwa mjini... hayo maeneo unayo yataja ni yapi? machinga complex? Tusubiri afanikiwe nikuletee zawadi...... uwezi kuwatoa machinga mjini
 
Hebu tuone safari hii kama Makala atakuwa na meno
 
Hata pale stand mbezi hasa kwa Magufuli waliwatengea waingie ndani lakini wameondolewa pale mbele...... lakini si wote wameingia ndani... hivi machinga kama wa pale mbezi utawapeleka wapi kwa agizo la jumatatu tuuu? lazima waseme watawapeleka wapi.......
 
Inakuwaje wanyonge wanabugudhiwa?
Wawaomdoe kupitia kodi inayostahili kama walivyo wafanyabiashara wengine (kodi ya eneo, VAT, leseni za biashara, Fire, usafi na Ulinzi).
Wafute vitambulisho vya wamachinga.
 
Hapa ndugu yangu hauko sawa jiji ni lazima kila mtu afuate sheria na sio lazima kila mtu awe machinga utatengwa mtaa mmoja kwa shughuli hizo lakini sio kuharibu mji kwa kisingizio tutakuwa vibaka. Naomba siku nione Kariakoo mpaka posta kote hakuna vibanda barabarani hata kimoja biashara za kisasa na ziwekwe taa za solar barabara zote city centre mazingira safi ili maduka au biashara zichangie kodi wamachinga hawachangii kitu zaidi wanapoteza mapato serikali katika kudhibiti. Mkuu wa mkoa nakuunga mkono 100% fanya jambo ambalo wengi wameshindwa hili liwe kipaumbele mji lazima kuwe na sheria na nidhamu. Walivunjiwa watu nyumba za kuishi sembuse vibanda vya mbao. Makalla fanya kweli na wala usiwachekee usoni iko siku watu watakukumbuka kwa hili. Kwa taarifa tu hata JPM kabla ya umauti kumchukuwa alishaambiwa hii sio sawa lazima waondoke na ilikuwa operation tayari basi kifo kikatokea. Mkuu wa mkoa please kwa hili naku support 100%.
 
Masoko si yanajulikana.
 
Kuna haja ya kubuni masoko ya Wamachinga kwa baadhi ya barabara kuliko kujenga masoko makubwa yanayoishia kukosa wajasiriamali.
 
Ohooo yamekuwa hayo tena, urafiki wa sisi wamachinga na CCM ndiyo umefikia kikomo?
 
Chadema watageuka watetezi wa machinga na ndiyo hapo Amoss Makala atafukuzwa ukuu wa mkoa.
CCM watatawala na nguvu ya chama wala sio wamachinga ni huko mashambani ndio wananguvu. kuharibu mji kwa sababu za kisiasa sio sawa na nitashangaa Chadema wakipinga hapo ndio nitajuwa chama hakina dira wanarukia fursa tu mbele. Kuna mambo ya msingi ni lazima yaungwe mkono na wote bila kujali chama gani na moja ya hayo kuweka miji yetu kisasa na kufuata sheria za majiji au mikoa kwa maslahi mapana ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…