Nigrastratatract nerve
JF-Expert Member
- Sep 4, 2019
- 1,521
- 4,381
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema ng’ombe takribani 200 watatolewa kwa ajili ya kuchoma nyama, tukio linalolenga kuimarisha uhusiano kati ya wafanyabiashara wa mkoa huo na viongozi wanaoshiriki kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma.
“Ng’ombe kama 200 hivi watachinjwa, ni kuchoma nyama tu hakuna ugali wala wali, lakini tumewaita wafanyabiashara wote wa Mkoa wa Arusha” amesema Makonda
Ametangaza kufanyika kwa sherehe ndogo Agosti 29, 2024 kwa lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara wa Arusha na Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma.