RC Makonda: Anayemjua mwizi aje ofisini kwangu kusema, nitampa laki moja

Ndio ni mwenyekiti wa kamati, ila swali ni nani anayepeleleza makosa ya jinai?

Tuna vyombo vya ulinzi na mamlaka za kusimamia sheria zinavyofanya hiyo kazi sio kamati.

Hiyo ni sheria sio utashi binafsi wa mtu
Hizi ni kiki na kuna wajinga wanamuelewa sana, shida ya hii nchi mkuu ni Ujinga, Taifa lina ujinga acha kabisa, yaani watu kama Makonda wanaonekana ni kama wakina Elon Musk vile, tatizo ni ujinga.
 
Makonda kasema, atapeleleza, au Kawataka Wananchi wamletee Taarifa Mkoani ambapo kutakuapo tayari wahusika wanaoshighulikia ?.


Na hata kama hawatakuwepo, unadhan Taarifa hizo atazikumbatia??.
TAKUKURU imevunjwa? ilitakiwa kwa hilo tamko lake lei Mkuu wa TAKUKURU aachie ngazi kabisa, Nchi imejaaa wajinga sana ndio maana watu kama Makonda wanaonekana ni Big brain kumbe hakuna kitu.
 
Hizo sheria weka pembeni mama, labda kwa vile hujawahi kukumbana na kadhia ya majambazi,wauwaji au wabakaji
Watajwe matukio yao yafwatiliwe na kufufuliwa!!
Naunga mkono hoja
 
Yeye mwenyewe ni mwizi no 1
 
Watanzania mbona hamfahamu taratibu na sheria zenu wenyewe?.

Vyombo vinavyopeleleza makosa ya jinai unakijua?. Sasa hivyo vyombo ndio vyenye huo uwezo kisheria.

Kasome hiyo sheria niliyoitaja hapo juu.
Makonda anatafuta umaarufu tu wala hana lolote
 
Makonda ni chizi haswa
 
Yule ni mla unga huwa anaamka tu na lake kichwani
 
Jitathmini
 
Kwani hufahamu kuwa RC ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa,?

Hufahamu kuwa wafichuzi wanaenda Ofisi ya RC ambayo ina nyenzo zote ulizo zitaja hapo??
Sasa unaenda kumfichua muhalifu bila evidence yoyote? mnatafuta kushtakiwa bila sababu yoyote ile.
 
Alitokea Mbunge mmoja akawa anatoa zawadi ya baiskeli (phoenix) kwa mwananchi atakayefichua mtu anayefanya mapenzi na wanafunzi. Ile approach ilikuja kumletea shida sana na haikutekelezeka, RC ajifunze pia.
 
Hizo sheria weka pembeni mama, labda kwa vile hujawahi kukumbana na kadhia ya majambazi,wauwaji au wabakaji
Watajwe matukio yao yafwatiliwe na kufufuliwa!!
Naunga mkono hoja
Sheria zikiwekwa pembeni,hilo jambo linabaki kuwa ni la utashi wa Mkuu wa mkoa aliyepo..je akija mwingine ambaye hataki kufanya hayo anayo fanya makonda itakuaje? Tunataka iwe endelevu.
 
Hata sijqsikiliza ila hii ni ramli chonganishi
 
Tatizo hii nchi inawajuaji wajinga wengi sana ambao ujuaji wao ukifafilia haujawahi kuwasaidia chochote wao wenyewe achilia mbali familia au taifa.

Mnafahamu kabisa kashfa za Jeshi letu la kaki, mnafahamu namna wanavyofanya kazi bila weledi, ni jukumu lao kushughulikia uhalifu je nani anaweza kuwapelekea taarifa za uhalifu?
 
Sasa unaenda kumfichua muhalifu bila evidence yoyote? mnatafuta kushtakiwa bila sababu yoyote ile.
Sikiliza tena alichokisema RC. mbona unawaza juu juu tu, huyo RC yeye haelewi kuwa kuna watu wanaweza kudanganya?? due deligence itahusika,
 
Mgeni wa Jiji chuki kwa Makonda ndiyo inamsumbua,haya yote anayajua sema kaamua tu kujitoa ufahamu pale anapo mjadili Makonda, anamjadili kama Makonda na si kama Mkuu wa Mkoa na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…