Punguza ujinga kidogo Mkuu.
Wewe unafikiri mtu yoyote anaweza tu kutoka na kujiamulia maamuzi yake kwenye hii nchi?. Ni lazima sheria zifuatwe na zikiwa hazijafuatwa ielezwe wazi.
Unafahamu kuwa anayeweza kutoa zawadi kwa mfichuzi (whistleblower) ni Mamlaka yenye uwezo wa kufanya upelelezi?
Na Tanzania swala la kufanya upelelezi kwenye makosa ya Jinai halipo kwa RC bali ni Polisi, Takukuru, FIU, TCRA, n.k zote zina mifumo ya kushughulikia makosa ya kijinai.
Sasa swali ni RC anatoa zawadi kwa hao wafichuzi chini ya sheria gani?, lazima hili liulizwe ili ifahamike ni pesa yake binafsi au pesa ya umma inayopaswa kufuata mtiririko sahihi.