RC Makonda atoa saa 24 kuwakamata Wabunge kama wazururaji endapo hawatarudi Bungeni. Wabunge wamjibu

RC Makonda atoa saa 24 kuwakamata Wabunge kama wazururaji endapo hawatarudi Bungeni. Wabunge wamjibu

Makonda wala hakuwa na nia ya kuwakamata hawa wabunge yy lengo lake LA kuwapanikisha limefaulu

Nimesikia Leo kila mbunge ametaja aliko mm nilijua wanejiquarantine Dodoma kumbe kweli wanazurura DSM..

Wao walimkosoa sana Rais kukaa Chato lakini nimewasikia Leo wakisema wako huru kukaa sehemu yoyote Tanzania

Lakini pia Makonda alitaka tu kuwaonyesha watu kuwa hawa jamaa zetu hawako Dodoma kama walivyodai

Makonda ametimiza lengo lake
Fanya kazi kiongozi,Acha mambo ambayo hayakusaidii wewe binafsi,Tafuta pesa
 
Mimi nimeshangaa spika akiwashambulia Upinzani eti tu wako Safe karantine..Hilo halina mantiki kwa watu wenye kufikiri mimi nilitegemea awambie wenzake waliobaki bungeni kwamba wakatwe posho zao kubwa kbwa wanazopata at least 10percent zksaidie kpambana na janga la Korona..Mkuu wa kiti cha bunge amedhani kupgia kelele hili la upinzani ndy kuwa wananchi wataona yy na wenzake ndy wazalendo hapana..mi naamini wamebana pale kwa sababu wameamua kuvuna njululu na sio uzalendo.
Nimeshangaa sana bunge Zima limeshindwa hata kutoa mchango wa kpambana na janga hili..hili bunge limejaa watu wasio na huruma na wawakilishi waliowapa kura na Kula yao..
Wakirudi majimboni tupige chini wote mazima tuanze moja!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema hawajawahi kuwa serious
Walutamba watakua dodo kwa karantjni ya siku 14,kumbe wote wanazurura huko Dad,ajabu walikua wanataka Dar ifungwe kwa kuwa ina wagonjwa wengj,lakini wao wamejazana huko wakila bata
 
Kitu cha kwanza kabisa unachotakiwa kujua ni kwamba, kwa wakati huu, wabunge walitakiwa kukutana kimtandao kutoka popote nchini.

Kujazana bungeni wakati Covid-19 ishaingia bungeni ni ujuha mkubwa sana.
kitu kinachowatoa udenda ni posho tuu hakuna cha zaidi, tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu wengine wanajijua hawatarudi hivyo bora kutafuna posho za makalio za kutosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah tunakoelekea sijui ni wapi, hili mweshimiwa alosema ni la utashi au ndo maswala ya siasaaa? ila nipo hapa naangalia hizi episodes zinavyozidi kuteremshwa
 
Mkuu wa mkoa woqite Tanzania ana mamlaka ya ukinzi na usalqma katika mkoa wake, msipime, Zitto anawaingiza "mkenge"
 
Mkuu wa Mkoa wa DSM, Paul Makonda ametoa saa 24 kwa Wabunge wote waliokimbia kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar es Salaam kula bata, kuhakikisha wanarudi Bungeni tofauti na hapo, watakamatwa kwa kosa la uzururaji kama wanavyokamatwa machangudoa wanaozurura usiku.

RC Makonda amesema kwa hawajaalika wazururaji jijini Dar es Salaam maana wanaweza kuhatarisha zaidi maisha ya wanaDSM kwa kuwaambukiza ugonjwa wa Corona. Amesema wabunge wanaopaswa kuwa Dar ni wale tu wenye kibali Maalum cha Spika wa Bunge.

Ikumbukwe kwamba Wabunge wa CHADEMA kwa pamoja walikubaliana kutoingia Bungeni kwa kile walichodai kwamba wanajiepusha dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona baada ya vifo vya ghafla vya wabunge watatu na watakaa karantini jijini Dodoma ili kuangalia mwenendo wa afya zao.


BAADHI YA WABUNGE WALENGWA BAADA YA KUSIKIA KAULI YA MAKONDA

Mbunge wa Kigoma Mjini na MwanaJF Zitto amjibu RC, asema
Mimi ni Mbunge wa Kigoma Mjini. Nipo Dar es Salaam. Sijakwenda Dodoma Bungeni Kwa sababu ninaamini kuwa Bunge lilipaswa kuahirishwa ili kupambana na Korona. Sitakwenda Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam hana Mamlaka yeyote ya kuniamulia niwe wapi katika Jamhuri ya Muungano

Sitakwenda Dodoma. Nitakaa Dar es Salaam kwa Uhuru kabisa. Najilinda dhidi ya Korona Mimi Binafsi na Familia yangu. Ninakaa nyumbani. Ninawalinda wapiga kura wangu wa Kigoma Mjini pia. Haya masaa 24 aliyotoa Mkuu wa Mkoa yaishe kwa Wabunge ni UPUUZI. ANIGUSE.


Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa naye amshukia RC Makonda
Nipo Dar Makonda jaribu kunikamata, mpuuzi wewe

Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya naye hakutaka kubaki nyuma
Wewe Bashite akili ndogo haitawali akili Kubwa usitafute kiki kupitia sisi ,sisi tupo Carantini tunajitambua, utaishia kukamata wabunge wa Chama chako na Mawaziri wenu ambao hawatulii Dodoma .Anza na Waziri wa Afya si Anakuwaga Dar ,kamata kama mzurulaji ..Acha kujitutumua .

Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche naye akaamua kuibuka na Mistari ya Biblia
Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu,
ukimtwanga kama nafaka kwa mchi,
hutauondoa upumbavu wake.
Mithali 27:22


Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akaamua kukumbushia kisa cha Mwamwindi kumuua Dkt. Kleruu
Kuna wakati nilisema hawa watoto wakiachwa waendelee hivi kuna siku wata chukua wake za watu kwa nguvu.Ujinga,kiburi utaingiza Nchi kwenye machafuko.Leo nime ikumbuka kesi hii,Republic vs Said Mwamwindi ya mwaka 1972.Said Mwamwindi alimuua RC Wilbert Kleruu

Kwamba imefika mahali RC Paulo anaweza kuwapangia watu tena Wabunge wapi wana stahili kuwa?Nani anawapa huu ujasiri?tunako elekea ni kubaya sana?Kwamba Wabunge wana fananishwa na Changudoa na wazururaji halafu Bunge litakaa kimya kwa sababu wanao fananishwa ni CHADEMA? HATARI SANA


Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' amejibu
Niko zangu DAR napata supu ya PWEZA ... Bashite is just a CLOWN


====

WABUNGE WAZURURAJI KUONDOSHWA DAR BAADA YA SAA 24.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo May 06 ametoa Saa 24 kwa Wabunge wote waliokimbia kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar es salaam "kula bata" kuhakikisha wanarudi Bungeni tofauti na hapo watakamatwa kwa kosa la Uzururaji kama wanavyokamatwa machangudoa wanaozurura Usiku.

RC Makonda amesema Mbunge anaepaswa kuwa Dar es salaam ni yule mwenye Kibali au Ruhusa ya Spika wa Bunge tofauti na hapo ni vyema wakafunga virago vyao na kurudi Bungeni ili kuepuka kukamatwa.

"Hakuna asiefahamu kuwa sasahivi tuko katika Mapambano dhidi ya Virusi vya Corona na sio uzururaji, ifahamike huu sio Mji wa wazururaji hivyo natoa Masaa 24 kwa Wabunge wote kurudi Dodoma tofauti na hapo tutawakamata kwa kosa la Uzururaji kama tunavyowakamata Machangudoa" alisema RC Makonda

Aidha RC Makonda amesema kwa Sasa ni kipindi muhimu cha mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali na wananchi waliwachagua kwenda kuwawakilisha Bungeni na kupigania maslahi yao hivyo kitendo cha kukimbia Vikao vya Bunge ni kutowatendea haki wananchi waliowachagua.

Hata hivyo RC Makonda amesema kinachomshangaza ni kuona Wabunge hao wamekimbilia Dar es salaam kufurahia Maisha badala ya kwenda Majimboni mwao kutembelea wananchi wanaokabiliwa na Mafuriko.

Pia soma > Wabunge wa CHADEMA wakubaliana kutohudhuria tena vikao vya Bunge kutokana na janga la COVID-9, Kujiweka Karantini kwa wiki 2

Bashite ni tatizo, upumbavu na ujinga anaoufanya huyu zero brain ni ule ambao nilioufanya miaka 25 iliyopita nilipokuwa primary school, nakumbuka nilikuwa na jeuri, kiburi na masifa ya kijinga kwa vile baba yangu alikuwa "Si" "O" pale 800's KJ.

Hebu jitafakari mara mbili bro mbingunikwetu unafeli wapi! Je unastahili kuendelea kuwepo hapo ulipo?

Kwanini kila siku ww tu? Una tatizo gani ww? Kama elimu huna si utumie hata kiakili chako kidogo, kabla hujaropoka kauli zako uwe unazitafakari kwanza na kuwauliza watu wenye uelewa wa masuala unayotaka kuyazungumzia
 
Back
Top Bottom