Mkuu wa Mkoa wa DSM, Paul Makonda ametoa saa 24 kwa Wabunge wote waliokimbia kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar es Salaam kula bata, kuhakikisha wanarudi Bungeni tofauti na hapo, watakamatwa kwa kosa la uzururaji kama wanavyokamatwa machangudoa wanaozurura usiku.
RC Makonda amesema kwa hawajaalika wazururaji jijini Dar es Salaam maana wanaweza kuhatarisha zaidi maisha ya wanaDSM kwa kuwaambukiza ugonjwa wa Corona. Amesema wabunge wanaopaswa kuwa Dar ni wale tu wenye kibali Maalum cha Spika wa Bunge.
Ikumbukwe kwamba Wabunge wa CHADEMA kwa pamoja walikubaliana kutoingia Bungeni kwa kile walichodai kwamba wanajiepusha dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona baada ya vifo vya ghafla vya wabunge watatu na watakaa karantini ili kuangalia mwenendo wa afya zao.
Yangu macho tu!