RC Makonda atoa saa 24 kuwakamata Wabunge kama wazururaji endapo hawatarudi Bungeni. Wabunge wamjibu

RC Makonda atoa saa 24 kuwakamata Wabunge kama wazururaji endapo hawatarudi Bungeni. Wabunge wamjibu

Hauna ushuru mdomo,, ila chunga ulimi usilete mgogoro
 
Mkuu wa Mkoa wa DSM, Paul Makonda ametoa saa 24 kwa Wabunge wote waliokimbia kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar es Salaam kula bata, kuhakikisha wanarudi Bungeni tofauti na hapo, watakamatwa kwa kosa la uzururaji kama wanavyokamatwa machangudoa wanaozurura usiku.

RC Makonda amesema kwa hawajaalika wazururaji jijini Dar es Salaam maana wanaweza kuhatarisha zaidi maisha ya wanaDSM kwa kuwaambukiza ugonjwa wa Corona. Amesema wabunge wanaopaswa kuwa Dar ni wale tu wenye kibali Maalum cha Spika wa Bunge.

Ikumbukwe kwamba Wabunge wa CHADEMA kwa pamoja walikubaliana kutoingia Bungeni kwa kile walichodai kwamba wanajiepusha dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona baada ya vifo vya ghafla vya wabunge watatu na watakaa karantini ili kuangalia mwenendo wa afya zao.

Yangu macho tu!
 
Huyu naye!!!! Uwakamate Kwa kuacha kazi waliotumwa na wananchi???

Hao wataadhibiwa na wananchi waliowatuma sio wewe bhana!! Inaonyesha Kwamba Kusoma sio kubadirika kumbe
 
ZITTO AMJIBU MAKONDA “SIRUDI DODOMA”.

Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amemjia juu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda muda mchache uliopita ametoa saa 24 kwa wabunge wote walio Dar es Salaam bila kibali cha spika kurudi Dodoma kabla ya kukamatwa kwa uzururaji.

“Mimi ni Mbunge wa Kigoma Mjini. Nipo Dar es Salaam. Sijakwenda Dodoma Bungeni Kwa sababu ninaamini kuwa Bunge lilipaswa kuahirishwa ili kupambana na Korona. Sitakwenda Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam hana Mamlaka yeyote ya kuniamulia niwe wapi katika Jamhuri ya Muungano”.Ameandika Zitto Kabwe kwenye Ukurasa wake wa Twitter.

Screenshot_20200506-121305.png


Zaidi soma: RC Makonda kuwakamata Wabunge kama machangudoa au wazururaji endapo hawatarudi Bungeni - JamiiForums
 
Huyu ni mpumbavu na anafanya vitu kumfurahisha mtu fulani huu ni ujinga na upuuzi wa kukemewa na kila mwenye akili timamu kwani yeye ni nani hadi ampangie mtu sehemu ya kuwa ndani ya JMT

Its not over until its over...[emoji769]
 
Kuna mambo ya msingi na ya muhimu kufanywa na RC wa Dar kuliko kukimbizana na watu wenye biashara zao na makao yao Dar. Hivi utawala wa sheria bado upo nchi hii?
 
Nyie wahuni lazima mkamatwe mmekimbia kujadili bajeti ya Wananchi mnashida club Chakaza,
 
Ameshiba huyo,katiba ina mpa uhuru wa kila raia kuishi sehemu yeyote atakayo endapo atakuwa hajahukumiwa na mahakama.

Tuone atamkamata nani? Labda anatafuta cheo kipande.
 
Back
Top Bottom