RC Makonda awasimamisha Kazi watumishi 13 Arumeru kwa ubadhirifu wa tsh million 600, yumo Mganga mkuu wa Halmashauri!

Mkuu nimemshangaa sana huyo jamaa na nimemueleza. Anaona bora Makonda akae ofisini ale mshahara kama wengine kuliko kuzunguka kwa wananchi ili asimzidi Nchimbi, Majaliwa na Raisi wake anayeshinda anazunguka angani kesho South Korea. Mpaka unajiuliza hii ni roho mbaya au ndo uchawi wenyewe!?,watu hawafikirii shida za watu wanawaza politics tu, na unakuta huyu jamaa ana ndugu zake kibao wenye shida kibao na waliodhurumiwa ila yeye anawaza siasa tu.
 
Tatizo sio CCM wala Chadema, tatizo ni ubinafsi wa mtu mweusi, hicho chama kingine kitaleta watu kutoka Ujerumani au Japan!?,hujui hata ndani ya vyama vya upinzani kuna ufisadi mkubwa!?,nitajie nchi moja ya watu weusi duniani ambayo ilibadilisha chama na kuweka chama kingine Cha upinzani kikaleta mabadiliko ya kudumu. Mfano Kenya walibadilisha chama shida zikabaki zilezile kwa raia, wakaleta katiba mpya shida zikabaki zilezile, hizo ni hisia za watu vichwani, hata wakichukua nchi chadema mambo ni yaleyale tu labda walaji ndo watabadilika tu.
 
Huyu dogo tukiacha wivu na husda, yupo vizuri. Kuna mambo nchi hii yanahitaji watu wa namna yake.

Bahati mbaya sana hata walio juu yake wengi vihiyo tu.
 
Yaani viongozi ni wauaji indirect mtu akikataa aje nimuonyeshe.

Kuna mtu anakodi software ya kufuatilia umeme kukatika kwa 78 bilioni ,iyo tungenunua ambulance ngapi,madawa hospital,madawati,vitabu,maji safi na salama kwa wananchi wangapi
 
Ana trend kumpita katibu wa chama waziri mkuu na mwenye kiti wake wasipo mdhibiti kwasasa atakua naushawishi mkubwa wakati wa uchanguzi........raia wetu sio critical thinkers 80% itamuamini na kumsikiliza.
Atiwe gerezani
 
HAIISHI MPAKAMIISHE.....WELLdONE MAKONDAA
 
Punguza kiherehere CHADEMA imeingiaje hapa?. Ongelea CCM waliopo madarakani, acha porojo. Unajifanya huoni yanayoendelea Sasa hivi umekazania CHADEMA wakiiingia bla blaa bla....., umekuwa nani wa kujua kesho, wakati hata saa moja usiku hujui Nini kitakutokea. Stupid
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha mh Paul Makonda amewasimamisha Kazi Watumishi 13 wa sekta ya Afya akiwemo boss Wao Dr Mbuya kwa ubadhirifu wa Fedha za Umma tsh million 600

Source Mwananchi

Vijana Msilale bado Mapambano πŸ˜‚πŸ”₯
Balaa
 
Huyu dogo ndiye kiongozi anayetrend kwa kazi nzuri mpaka sasa

Misuse of resources kumfungia arusha pekee
Siyo rahisi sana kupambana na ufisadi.

Ukizama ndani sana utagundua kwamba chanzo cha ufisadi ni wananchi wenyewe na siyo watumishi wa Umma.
 
Huyu chalii anapambana sana tukiacha chuki he deserves it all nashangaa why people hate on him!? Au ndio anabana magape ya wapgaji
Muulize hilo swali mke wa Ben Sanane akikujibu muulize na Roma msanii aliyekimbilia Marekani. Halafu muulize na aliyekuwa mkuu wa CIA na waziri wa mambo ya nje wa Marekani alimainiaha nn kusema Bashite ananyima watu haki ya kuishi
 
Ana trend kumpita katibu wa chama waziri mkuu na mwenye kiti wake wasipo mdhibiti kwasasa atakua naushawishi mkubwa wakati wa uchanguzi........raia wetu sio critical thinkers 80% itamuamini na kumsikiliza.
Iko vile na hakuna namna ya kuibadilisha hiyo kitu kwa sasa πŸ‘

Watu wanadhani kwamba Makonda anapewa sapoti na watu wasiokuwa na Akili ,
Lakini kumbe wanaomsapoti Makonda wanaamini kwamba Angalau huyu jamaa anaonyesha kujali na kukerwa na ubadhirifu unaofanyika πŸ‘
Na ana uthubutu wa kuchukua hatua zinazostahiki bila kusita πŸ‘

Watu wamechoka na maneno maneno matupu wanataka kuona hatua zinachukuliwa kwa wabadhirifu. πŸ‘πŸ˜³πŸ™„πŸ€ 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…