RC Makonda na Mwanasheria wa Arusha wameshirikiana kumdhalilisha huyu mama

RC Makonda na Mwanasheria wa Arusha wameshirikiana kumdhalilisha huyu mama

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
Huu ni udhalilishaji, na wakili wa TLS ameshirikiana na Makonda kudhalilisha huyu mama.

Wanasheria wa Halmashauri hawaendi Mahakamani, kwa mujibu wake, kwa sasa Ofisi ya wakili mkuu iliyopo DSM ndio wanafanya hiyo kazi.

Yeye anasema walishawaandikia ofisi ya Wakili Mkuu kuchukua hatua hizo kwasababu kwa sasa wao hawaendi Mahakamani. Lakini bado anadhalilishwa.

 
Huu ni udhalilishaji, na wakili wa TLS ameshirikiana na Makonda kushalilisha huyu mama.

wanasheria wa halmashauri hawaendi Mahakamani, kwa mujibu wake, kwa sasa Ofisi ya wakili mkuu iliyopo DSM ndio wanafanya hiyo kazi. yeye anasema walishawaandikia ofisi ya wakili Mkuu kuchukua hatua hizo kwasababu kwa sasa wao hawaendi Mahakamani. Lakini bado anadhalilishwa.

View attachment 3002024
Tuliza nchecheto uandike vizuri yaeleweke
 
Tuliza nchecheto uandike vizuri yaeleweke
kitu gani hujaelewa hapo kaka. clip inajieleza. wanaoendesha kesi za madai sio wanasheria wa halmashauri, ni wakili mkuu ofisi yake ni tofauti na ya halmashauri, ila amesulubishwa dada wakili arusha, hapo una semaje?
 
kitu gani hujaelewa hapo kaka. clip inajieleza. wanaoendesha kesi za madai sio wanasheria wa halmashauri, ni wakili mkuu ofisi yake ni tofauti na ya halmashauri, ila amesulubishwa dada wakili arusha, hapo una semaje?
Huyo Dada kesi yake inahusu nini kwani? Wengine wageni kwenye hilo Sakata
 
Ulifatilia mwanzo Hadi mwisho wa huo mjadala ??.
Naijua hiyo habari yote, ila najua wewe hauijui na hauna akili ndio maana unakimbilia kutukana. hustahili hata kuzingatiwa kwa lolote kwenye majadiliano kwasababu akili zako ni kama za yule mnayemtetea. zero brain.
 
naijua hiyo habari yote, ila najua wewe hauijui na hauna akili ndio maana unakimbilia kutukana. hustahili hata kuzingatiwa kwa lolote kwenye majadiliano kwasababu akili zako ni kama za yule mnayemtetea. zero brain.
Mjinga Mmoja wee, Mikutano yote ya Makonda Naifatilia , hamna mkutano aloufanya Makonda nisiutizame kwenye hizi siku sita zake.

Hamna udhalilishaji ambos keshawah ufanya.

Bichwa lako kubwa ulolijaza matope na ujinga, mpaka unaishia kutumia unafiki ,majungu , kutafasiri sawasawa na matope yako ya kichwan.

Usilazimishe Wananchi tuelewe huo ujinga wako.

Dunia ya Sasa, Uongo na majungu havina nafasi.
 
Mjinga Mmoja wee, Mikutano yote ya Makonda Naifatilia , hamna mkutano aloufanya Makonda nisiutizame kwenye hizi siku sita zake.

Hamna udhalilishaji ambos keshawah ufanya...
Mbona haujibu hoja, unatukana, angalia hiyo clip halafu sema ni ujinga gani unatukania
 
Huu ni udhalilishaji, na wakili wa TLS ameshirikiana na Makonda kudhalilisha huyu mama.

Wanasheria wa Halmashauri hawaendi Mahakamani, kwa mujibu wake, kwa sasa Ofisi ya wakili mkuu iliyopo DSM ndio wanafanya hiyo kazi. Yeye anasema walishawaandikia ofisi ya Wakili Mkuu kuchukua hatua hizo kwasababu kwa sasa wao hawaendi Mahakamani. Lakini bado anadhalilishwa.

View attachment 3002024
Ungeanza kutuletea mwanzo wa hiyo clip uone uozo huyo mwanasheria mjivuni na mbinafsi unayetaka kumtetea wewe hapo.

Weka tangu ilipoanza, siyo kuikata clip kuchagua maneno ili
Kueneze chuki zako hapa.
 
kitu gani hujaelewa hapo kaka. clip inajieleza. wanaoendesha kesi za madai sio wanasheria wa halmashauri, ni wakili mkuu ofisi yake ni tofauti na ya halmashauri, ila amesulubishwa dada wakili arusha, hapo una semaje?
Kwa uwezo alioonesha hapo kulingana na maelezo yake, hakupaswa kumuwakilisha mkuu wake wa idara.
 
Ungeanza kutuletea mwanzo wa hiyo clip uone uozo huyo mwanasheria mjivuni na mbinafsi unayetaka kumtetea wewe hapo.

Weka tangu ilipoanza, siyo kuikata clip kuchagua maneno ili
Kueneze chuki zako hapa.
ukiangalia clip, labda kama hauna bando, sijalalamikia wengine wote, ila eneo la uyo mama kwamba akitaka kufafanua bashite hampi nafasi. Kuna kesi imeonekana walishindwa na walitakiwa wakate rufaa, wanaotakiwa kuandaa nyaraka na kukata rufaa sio huyo mwanasheria, ni Ofisi ya Wakili MKuu. bashite anaonekana hajui nini maana ya wakili mkuu, anaendelea kumkandamiza huyo mama kwamba kwanini hajakata rufaa hadi leo, wakati Mama ameshamwabia tuliandika barua kwa WAKILI MKUU kumpa update na yeye ndiye alitakiwa akate rufaa kwasababu hao wanasheria wa halmashauri kwa sasa hawaendi Mahakamani, wanawakilishwa na Wakili Mkuu.

kwa msio jua, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, ukiondoa pale kwa feleshi, kuna matawi mawili, tawi la kwanza ni la jinai ambako yupo DPP, na tawi la pili kuna WAKILI MKUU ambako ni kesi za madai zote. hizo kesi za halmashauri ni za madai, hata kama wewe ni mwanasheria wa halmashauri au wa taasisi yeyote ya kiserikali huwezi kwenda mahakamani kwenye jambo la madai, serikali imeunda taasisi ya WAKILI MKUU, huyo ndiye anaiwakilisha serikali kwenye kesi zooote za madai.

sasa mama anamwambia bashite tulishaandika barua kwa wakili mkuu, na bashite bado anaendelea kumng'ang'ania kwamba kwanini haujakata rufaa, rufaa ipi sasa wakati anayekata rufaa sio halmashauri bali ni Wakili Mkuu ambaye ofisi yake ipo hapa hapa DSM?
 
Kwa uwezo alioonesha hapo kulingana na maelezo yake, hakupaswa kumuwakilisha mkuu wake wa idara.
watu wakisikia mtu anaitwa wakili mkuu wanafikiri ni mkuu wa kitengo cha mawakili palepale halmashauri ya arusha. kwa kiingereza anaitwa "solicitor general", ofisi zake zipo dsm hapa, kesi zote za halmashauri na taasisi za serikali kama ni za madai, huyo ndiye anasimama.

Hao wanasheria wa halmashauri hawaendi mahakamani, na mama kasema walimwandikia barua wakili mkuu ili aende mahakamani akate rufaa, lakini bashite kwa vile hajui nini maana ya wakili mkuu anafikiri labda yupo katika ofisi ile ile pale arusha kwa huyo huyo mwanasheria, anaendelea kumwuliza mbona hujakata rufaa, akate rufaa kwani yeye ni wakili mkuu?

Solicitor general si yuko dsm na ameandikiwa barua, dada yupo halmashauri ya arusha, na bado yeye ndiye analaumiwa wakati hatakiwi kuappear mahakamani.
 
ukiangalia clip, labda kama hauna bando, sijalalamikia wengine wote, ila eneo la uyo mama kwamba akitaka kufafanua bashite hampi nafasi. Kuna kesi imeonekana walishindwa na walitakiwa wakate rufaa...
Pamoja nankueleza yote hayo, bado huyo mwanasheria kwa uwezo alioonesha hakupaswa kumuwakilisha mkuu wake wa idara.
 
Pamoja nankueleza yote hayo, bado huyo mwanasheria kwa uwezo alioonesha hakupaswa kumuwakilisha mkuu wake wa idara.
Mkuu wake wa idara yupi? fafanua. Ofisi ya Halmashauri yeye alipo, ni taasisi tofauti kabisa na OFisi ya solicitor general (wakili Mkuu) wanaoendesha kesi zote za madai za serikali. huyo wakili wa halmashauri mwajiri wake ni DED, wakati solicitor general hahusiani kabisa na employment ya halmashauri hapo, nadhani yeye anajitegemea.
 
watu wakisikia mtu anaitwa wakili mkuu wanafikiri ni mkuu wa kitengo cha mawakili palepale halmashauri ya arusha. kwa kiingereza anaitwa "solicitor general", ofisi zake zipo dsm hapa...
Kwa maelezo ya huyo wakili mwakilishi wa TLS, Ofisi ya wakili mkuu ilitekeleza wajibu wake vizuri tu, ni wazi, kwa maelezo yale, walipoandikiwa barua hiyo, walitekeleza jukumu lao kwa kukata rufaa, makosa yanaoneka hapo ni kutokuwasilisha "notice" ya rufaa kwa wadai, msingi mkuu uliofanya mahakama ya rufaa kuitupa hiyo rufaa.

Utufafanulie hapa, ni jukumu la kuwasilisha hiyo "notice" ya rufaa kwa wadai ni jukumu la nani, ofisi ya mwanasheria wa halmashauri au ofisi ya wakili mkuu?
 
Mkuu wake wa idara yupi? fafanua. Ofisi ya Halmashauri yeye alipo, ni taasisi tofauti kabisa na OFisi ya solicitor general (wakili Mkuu) wanaoendesha kesi zote za madai za serikali. huyo wakili wa halmashauri mwajiri wake ni DED, wakati solicitor general hahusiani kabisa na employment ya halmashauri hapo, nadhani yeye anajitegemea.
Ni wazi wewe umepandisha hiyo "clip" bila kuangalia na kisikiliza kwa umakini majibizano yao. Irudie tena vizuri, uje hapa.
 
Kwa maelezo ya huyo wakili mwakilishi wa TLS, Ofisi ya wakili mkuu ilitekeleza wajibu wake vizuri tu, ni wazi, kwa maelezo yale, walipoandikiwa barua hiyo, walitekeleza jukumu lao kwa kukata rufaa,...
nadhani yule mwenye mandate kuappear Mahakamani ndiye mwenye wajibu huo. Ofisi ya Wakili Mkuu ndiyo ilikuwa na wajibu huo. Kama wanasheria wa halmashauri hawana mandate kuappear Mahakamani, Mahakama itaamuaje jambo kuwarushia zigo wao wakati sio party kwenye kesi?

Yaani jambo lolote la kesi ya madai likiikuta taasisi yeyote ya serikali, ile taasisi inatakiwa kurusha zigo hilo kwa wakili mkuu, yeye ndiye atafanya kila kitu na amewekwa mahsusi kwa ajili ya hilo. hata kama kuna kitu halmashauri watatakiwa kufanya, ni kwa maelekezo ya wakili mkuu.
 
ukiangalia clip, labda kama hauna bando, sijalalamikia wengine wote, ila eneo la uyo mama kwamba akitaka kufafanua bashite hampi nafasi. Kuna kesi imeonekana walishindwa...
Unganisha na clip zingine za siku hiyo kuona namna mama huyo mwanasheria anavyolalamikiwa kuminya haki za watu bhana!

Sasa kama procedure ndo'hiyo, je imebadilisha mwisho wa muda wa kukata rufaa?

Sheria inasemaje kuhusu haki ya mtu aliyeshinda kesi ambayo haijakatiwa rufaa?

Huo mkoa inaonekana kuna cyndcate kubwa sana ya watumishi wa umma ya kukandamiza haki za watu kwa mbinu chafu za rushwa.

Kama ulisikiliza vizuri, kuna Wilaya fulani, mtu kashinda kesi ya kiwanja sijui shamba, kila akifuata tararibu za kukazia hukumu, anakumbana na vikwazo vya kulindana kutoka kwa Ocd miaka nenda rudi!

Mi naona Mh. Makonda yupo sahihi kufurumua uozo wote uliojificha kwa migongo ya vyeo na jinsia za watumishi wa umma.

Nimekujibu randomly kwa kuwa sina kifaa cha kuweza kuapload hizo clips ili twende na vielelezo kwa ninayoyasema.

Huyo unayemsema kadhalilishwa, hajadhalilishwa lolote, zaidi yake mwenyewe kudhalilisha watu wengine kwa kuwanyima kuwalipa haki zao.

Tuacheni kuangalia ujinsia wa staff na kuutanguliza mbele badala ya kuangalia na kuchambua kiini cha tatizo kinachokuwa kimeletwa mezani.
 
Unganisha na clip zingine za siku hiyo kuona namna mama huyo mwanasheria anavyolalamikiwa kuminya haki za watu bhana...
usichojua na ninachosema ni kwamba, mwenye wajibu wa kukata rufaa hakuwa huyo mama, ni wajibu wa WAKILI MKUU, hiyo ni ofisi nyingine kabisa yenye mwajiri mwingine kabisa inajitegemea na serikali imeiunda ili kesi zote za madai za uma hao wanasheria wa halmashauri wasiende, aende WAKILI MKUU, ndio maana alikuwa anahangaika kumwambia walimwandikia WAKILI MKUU barua ili afanye hizo taratibu kwasababu wanasheria wa halmashauri hawana mamlaka kwenda mahakamani, wanatakiwa kuwakilishwa na WAKILI MKUU.
 
Back
Top Bottom