Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 882
- 3,337
Nafahamu Arusha ni mji wa kitalii, Dkt. Samia Suluhu Hassan (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ameamua kwa makusudi kuipendelea Arusha hata akamtoa mwanaye wa pekee (Paul Makonda) ili aje aungane nanyi, angeweza kuniacha nikafanya kazi ya Uenezi na amesema mwenyewe nimeifanya vizuri lakini kwa kuwapendeni wakazi wa Arusha akasema Makonda nenda kaanzie pale alipoishia kaka yako Mongela (John Mongela, aliyekuwa Mkuu wa mkoa Arusha, ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu CCM Tanzania Bara)
"Na katika utalii tuna maeneo matatu (3), utalii wa kwanza ambao Dkt. Samia ameufanya ni kufanya 'Royal Tour' na alivyotoka Marekani kituo chake cha kwanza katika nchi yetu Tanzania alitua KIA (uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro) kuja kusema nanyi katika uzinduzi wa 'Royal Tour', alitaka kila kijana, kila mama, kila muuza mchicha amletee mtu mwenye pesa ili maisha yake yaende, na ndio maana leo hii utalii umevunja record"
"Katika eneo hilo (la utalii) ameniagiza nishirikiane na ndugu zetu wa uwekezaji (TIC) kuhakikisha tunaongeza Hoteli za kutosha Arusha, tukiongeza Hoteli maana yake tumeongeza ajira, tukiongeza ajira tunakuwa tumeongeza kipato kwa wakulima na hivyo tutaboresha maisha ya wananchi"
Paul Makonda ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Arusha amezungumza hayo wakati akizungumza na wananchi wa Arusha waliojitokeza kumpokea kwenye viunga vya ofisi ya Mkuu wa mkoa huo leo, Jumatatu Aprili 08.2024
Chanzo: Jambo TV
=======
Uteuzi kuwa Mkuu wa Mkoa Arusha

Uteuzi na Utenguzi: Paul Makonda ateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Ndalichako aondolewa uwaziri
- Arusha wajipanga kumpokea RC Makonda
- RC Makonda: Rais Samia ameipendelea Arusha, amemtoa mwanae wa pekee na kumleta Arusha
- RC Makonda: Nimekoswa koswa mara 3 kupoteza maisha
- Arusha: Makonda akutana na Mwamposa na kufanyiwa maombi
- Makonda: Watalii hawaji Arusha kulala wanakuja kula starehe, ni lazima Arusha iwe salama saa 24. Hao wadudu nitaongea nao
- Paul Makonda: Watu wa Arusha wanaweza kwenda popote kupambana, iko mikoa unakuta waganga wengi wa kienyeji. Kutambulisha polisi wa kitalii
- Makonda atembelea maeneo yaliyoathirika na Mafuriko jijini Arusha