natoa hoja hapa msimu huu wa CORONA.
Kanisa:
-shika pua yako iambie usinuse harufu mbaya
-shika mdomo wako uambie usinene mabaya
-shika macho yako yaambie yasitazame uovu
-mgeukie mwenzako mwambie kwa sauti (paza sauti mwambie usiwe kama popo)
-mshike mkono jirani yako mwambie umependeza
-shika kichwa chako tamka kipate akili
-asiyependa kukusanyika pamoja ibadani ni mchawi
-mpinga kristo yupo, kama hutaki kuhudhuria ibada wewe ni mpinga kristo
-hakuna lisilowezekana kwa Mungu kila ugonjwa unapona
serikali:
-usishike pua, macho wala mdomo
-msishikane mikono
-mkae mbali mbali angalau mita moja
-msikusanyike
-mvae mask
kanisani:
-imba toa sauti, omba kwa sauti usiombee tumboni toa sauti(watu wanapayuka mate yao yanaruka na kusambaa hovyo)
--hawavai balakoa
-wanatazamana na kushika hivyo vilivyokatazwa na serikali kuvishika
-wanakaa karibu sana chini ya robo mita
-wanaimba kwaya na kucheza miziki
-wanasali zaidi ya lisaa limoja
-watu wanafanya maombi kwa sauti kubwa wanarushiana mate, wanasali mara wanyenyue mikono juu mara washushe mara wapige magoti mara warukeruke...purukushani zote hizi wanazifanya wakiwa hawajavaa balakoa mwishoe wanakohoa kwa jasho na vumbi pamoja na kupiga chafya pasipo kuziba midomo. hawa watu wakitoka huko wanakuja mitaani tunajumuika nao katika shughuri za kijamii....si watalimaliza taifa lote endapo mwenye ugonjwa atakatiza miongoni mwao
NB: tuwe serious katika kupambana na majanga, kwanini serikali na dini vinavutana..yupi ni mpinga kristo na yupi ni mpinga uzima?