Mbulu
JF-Expert Member
- Apr 15, 2015
- 5,620
- 5,515
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hiyo tuseme wewe hutaki kutekeleza agizo hili?!?!Anasema tuvae barakoa wakati bado kuna mikusanyiko mikubwa wanaiangalia.
Hii idea ya kutumia viboko, mimi nilikuwa nafikiria itumike hata kwa watu wanaopatikana na makosa madogo madogo kiasi kwamba wanatakiwa kuwekwa mahabusu. Maana najiuliza sasa mahabusu sasa hivi watu wanaishije? Mwizi wa kuku aliyeko mahabusu achapwe viboko halafu aachiwe arudi nyumbani kwake badala ya kuendelea kuongeza msongamano wa watu kwenye mahabusu, atatuongezea wagonjwa wa corona bure
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Paul Makonda amesema kuanzia Aprili 20 siku ya Jumatatu kila mtu atakayepanda Daladala na anayekwenda kwenye eneo la manunuzi yeyote lazima awe amevaa Barako (Mask)
Poa siku hiyo ya Jumatatu ameelekeza biashara zote zifanyike katika mfumo wa 'Take Away', hivyo mtu akienda sehemu anunue na aondoke.
Mh. Mkuu wa Mkoa watu hawajamwelewa vizuri. Alichosema kwa sasa ni kuwa, kwa kuanzia, watu wavae barakoa wakiwa wanaelekea Sokoni au kwenye daladala. Na hii taarifa inaonyesha KAMA kwa sasa cases zinazopatikana za waathirika walio wengi ni kutoka kwenye mikusanyiko ya daladala na ya Sokoni, ila sasa sisi uelwa wetu ni mdogo. Asingeweza kusema moja kwa moja hivyo kwa sababu angesababisha taharuki, watu wangeacha kupanda daladala na kuanza kutembea, na sokoni pia ingekuwa shidaUkitaka kujua "UKAIDI WA WATANZANIA" kesho kuna viongozi wa dini watapanda madhabahuni kufanya ibada kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu.
Ili usiende kazini ausioKila mtu mdomo ukimuwasha anaongea chake. Bora rais aje atoe muongozo kama ni lockdown au curfew.
Kuliko huu utoto unao fanywa, mara take away mara kuvaa masendeu!
Sent using Jamii Forums mobile app
Fuata masharti unayoelekezwa. Unanunua chakula cha elfu tano kwa siku unaacha kununua barakoa ya elfu 2 kisa unataka msaada wa serikali. Tumeambiwa tujikinge, jilinde wewe ilinde na familia yako na fuata maagizo ya viongozi kama huwezi stay home Corona inaua
Aache watu wajilinde wanavyoweza wao,kama walisema hawawezi kuweka watz lockdown kwakua maisha yao ni ya kubangaiza, hio hela ya kubadilisha mask kila baada ya Masaa 4 wanatoa wapi?Fuata masharti unayoelekezwa. Unanunua chakula cha elfu tano kwa siku unaacha kununua barakoa ya elfu 2 kisa unataka msaada wa serikali. Tumeambiwa tujikinge, jilinde wewe ilinde na familia yako na fuata maagizo ya viongozi kama huwezi stay home Corona inaua
Jamani kwani huko kanisani au Misikitini tunalazimishwa kwenda? Tukae ndani na familia zetu Tu. Maana afya ni yetu. Mashehe,Mapadri na Wachungaji wakibaki wao watasali wao.
Kuna watu wanatamani sana ibada zisitishwe! Hawa bila shaka ni wachawi!! Maombi yakipamba moto wanashindwa kuruka na ungo!! Kipindi hiki si cha ksitisha ibada bali cha kuongeza ibada na Mungu atatuponya na janga hili!
Niwaombe vioongozi wetu wa kitaifa wabaki na msimamo huo wa kuruhusu ibada ili mradi marekebisho yafanyike kuondoa misongamano na watu wanawe kabla na baada ya ibada kwa mujibu wa maelekezo ya wataalamu.