RC Makonda: Yeyote anayeenda katika eneo la manunuzi lazima avae barakoa. Kwenye misongamano watu wakae umbali wa mita 2

RC Makonda: Yeyote anayeenda katika eneo la manunuzi lazima avae barakoa. Kwenye misongamano watu wakae umbali wa mita 2

Bams,
Pale Congo Street na sehemu kubwa ya Kariakoo kuna take away kweli?. Kuna logic gani ukazuia watu kukaa bar lakini ukaruhusu Kariakoo watu warundikane? Au corona itawahurumia wanaokusanyika Kariakoo? Pia kuna lugha siku hizi utasikia eti pasiwe na mkusanyiko usio wa lazima! Mikusanyiko ya lazima ndo ipi? Be serious!
 
Barakoa moja itakufaa nini iwapo yakupasa kubadili kila masaa 4-6, endelea kujikinga bwashee usitegemee serikali yetu pendwa hii.... jemedari mkuu kukimbia vita ikufikirishe kitu.
 
Dah. Tunapigwa mchana kweupeee. Barakoa ni dili. Zile za msaada ziko wapi??
 
Halafu tunaambiana hii ni donor country, ni matumizi mabaya ya msamiati .
 
Swali lisilo na jibu ni iweje serikali inayoweza kugawa bure vibendera vya mkononi kwenye mikutano na sherehe leo eti ishindwe kugawa bure barakoa! Inao uwezo kinachokosekana labda ni utashi. Gharama za kutengeneza kibendera kimoja na kijiti chake ni zaidi ya kijitambaa cha barakoa na kikamba chake.
Nb.
Pascal Mayalla naomba tuanzie hapa mjadala.
 
... ila zimepanda bei; 2000/pc! Kuendana na maelezo ya Naibu Waziri Afya kwamba vitambaa vina uwezo mdogo kukinga maambukizi hakuna namna inabidi kutumia special ila bei yenyewe ndio hivyo imeshiba ukizingatia kwa siku unahitaji angalau tatu (6,000/=). Kazi ipo!
 
Ni kama mmeamua kutuaacha wananchi kila mtu ajihangaikie kivyake, kama chama tu tuna uwezo wa kugawa Tshirt, kofia, khanga, vipeperushi, mabango na posho nchi nzima kipindi cha kampeni.. Serikali inashindwa ku-waorganize wafanyabiashara wakubwa na wadau wengine wa afya kushirikiana na serikali tukapata Barakoa bure kabisa kwa kila mwananchi? kama mmeshindwa kwa nini msitoe msamaha wa kodi kwa hizi bidhaa ili zipatikane kirahisi kipindi hiki na kwa bei nafuu angalau ya tsh 500? Angalia sasa watu wanakimbilia kusafiri kurudi kijijini bila kupimwa nyie serikali ni kama hampo, siku si nyingi huko vijijini nako ugonjwa unaenda kutapakaa.. Jamani hivi nini kazi yenu?

Hao migambo na polisi mnaoweka kukamata wasiovaa Barakoa ni wa nini wakati upatikanaji wake bado ni kizungumkuti? Gawa kwa watu halafu wakamate wasipovaa, sio kama mnavyotaka kufanya hivi sasa..,Katibu mkuu wangu bashiru saidia kuwashauri hawa watu maana mpaka sasa raia hawajui wafuate lipi,ummy alishawahi kusema wanaotakiwa kuvaa barakoa ni wale waliopatwa na maambukizi tu juzi makonda kasema watu wavae barakoa hata za vitambaa vya khanga, naibu waziri wa afya akatoa kauli bungeni kwamba kuna barakoa maalum kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya corona sio kuvaa yoyote watu hawajui washike lipi?

viongozi wetu kuweni serious, ni kama mmewatelekeza watanzania na sasa kila mmoja anapambana kivyake..., angalieni hapo kenya tu serikali inagawa hivi vifaa vyote bure, kwa nini sisi? Jamani 😭😭
 
Wanataka au mnataka ugonjwa uenee zaidi ili uchaguzi usifanyike na au mpate visingizio vya kushindwa kutimiza ahadi zenu
 
Back
Top Bottom